URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

Ndg. Zigizaga,

Uchaguzi wa Urais si jambo la uzoefu tu, kwa zaidi ni jambo la dhamira ya kuleta mapinduzi ya hali ya maisha ya kesho (elections are about the future, not the past). Hivyo naelezea future ya Tanzania itakuwaje kama nikiwa Rais, nipime kwa hilo.

Hata hivyo, ukitaka rekodi yangu, tazama miaka mitano ya ubunge wangu, tazama pia miaka mitano ya kufanya kazi kwenye kampuni (biashara), miaka mitano ya kuwa mwanaharakati, mwanazuoni na mtafiti. Tazama pia rekodi yangu ya uongozi kwenye chama. Tazama pia formative years na namna nilivyoandaliwa na mfumo kuwa kiongozi. Ukiona sitoshi, ninyime kura yako. Ukiona natosha nipigie debe wakati ukifika.

Ni kitu gani kilichokufanya kushindwa kuboresha au hata kutoa mchango katika swala nzima la kuboresha elimu kwa muda wa miaka 5 uliyokaa bungeni?

Wewe ni Mbunge wa CCM, Je mmeshindwa nini kuboresha elimu kifiia kiwango ambacho unaona kina manufaa kwa taifa? Na kama CCM mmeshindwa kuboresha elimu kwa kipindi cha miaka 50 ni kwanini tuwaamini tena miaka mingine 5?
 
Maunvi mzigo umeshakuwa mzito kwake! Hana jipya tens Jana kabolonga ile mbaya!

Yeye anadhani huo umati ndiyo kukubalika!
Ameithibitishia dunia kuwa ni fisadi mkubwa. Hizo pesa za kutayalrisha mkutano kapata wapi. Kama kweli anaipenda Tanzania, si angetoa msaada kwa ALBINO akawajengea shule? pesa alizotumia kutangaza nia zingetosha kabisa.
Inahuzunisha sana, vijana mnataka kupeleka balaa ikulu. Kwanza hakumbuki fadhila, atawaacha kwenye mataa tu.
 
URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

Kwenye awamu ya nne tumeshuhudia Serikali ya CCM ikijenga shule nyingi na kuzalisha na kuajiri walimu wengi kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi yetu. Tumeshuhudia vyuo vingi vya elimu ya kati vikipanda hadhi na kuwa vya elimu ya juu, na tumeshuhudia idadi ya wahitimu wenye elimu ya chuo kikuu wakiongezeka mwaka hadi mwaka. Sambamba na jitihada hizi, tumeshuhudia wahitimu wakifanya usaili wa mchujo wa awali kwa ajili ya nafasi za kazi kwenye uwanja wa Taifa. Tumeshuhudia baadhi ya taasisi zikilalamikiwa kwa kutoa ajira kwa undugunaizesheni. Hii inatanabaisha kuwa tuna tatizo si tu la kukosa elimu yenye kutoa ujuzi wa kujiajiri bali pia tuna wasomi wengi wenye elimu ya juu kushinda mahitaji ya soko la ajira. Tumeshuhudia shule za kata zikitoa wahitimu wenye ubora ambao wamekuwa wakisonga mbele zaidi kwenye masomo yao, huku wengine wengi wakifeli . Ni lazima tufanye paradigm shift.

Ni wazi kwamba hatupaswi kuendelea kuwekeza kwenye kusomesha watu wetu kwenye elimu ya juu kwa kipindi hiki, pengine tujikite zaidi kuwekeza kwenye kuongeza ubora na kwenye utafiti na teknolojia.

Nini tunahitaji kwenye elimu sasa?

Tunahitaji:

(1.) Kuongeza ubora wa shule zetu kwa kujenga maabara, maktaba, mabweni, viwanja vya michezo, karakana (zinapohitajika) na nyumba za walimu. Pia kuhakikisha shule zote nchini zinakuwa na umeme, maji na mtandao mzuri wa mawasiliano ili kuongeza ari ya walimu kuishi kwenye maeneo yote bila kuchagua (retention scheme).

(2.) Kuboresha mitaala ili kuifanya elimu yetu iwape wanafunzi si tu elimu ya ufahamu bali pia ya ujuzi na uvumbuzi; na zaidi component ya elimu ya ujasiriamali na communication skills ni lazima.

(3.) Tuanzishe mfumo wa motisha kwa walimu wetu kulingana na jiografia na mazingira wanapofanyia kazi (differential incentives scheme). Walimu wanaofundisha maeneo ya mbali na makao makuu ya wilaya na wanaofundisha kwenye maeneo yasiyo na huduma mbalimbali muhimu ni lazima walipwe posho maalum zaidi ya wenzao wanaofundisha maeneo ya mijini.

(4.) Kuwa na mpango wa dharura wa kuanzisha shule za VETA kwa kuamua kuzigeuza baadhi ya shule za sekondari kuwa za VETA na kuziwezesha zipate vifaa na wakufunzi wenye ujuzi ili zianze mara moja kutoa mafunzo kwa vijana waliohitimu darasa la saba na hawakupata fursa ya kusonga mbele, na kwa wale waliohitimu kidato cha nne na hawakupata fursa ya kusonga mbele, na hivyo hivyo kwa waliohitimu kidato cha sita. Mpango huu utatoa fursa ya kupata vijana wengi wenye ujuzi kwa haraka kwa ajili ya kujenga vijiji na miji yetu (mafundi uashi, ubunifu wa mavazi, ushonaji nguo, useremala, mafundi bomba, umeme, madereva, mafundi mitambo, mabwana shamba vijijini n.k.). Shule za VETA zitatoa fursa kwa vijana waliopoteza matumaini, zitawapa ujuzi wa kujiajiri, lakini pia wahitimu wa VETA wanahitajika sana kwenye ajira za sekta binafsi.

(5.) Kurekebisha mfumo wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa kuweka mfumo ambao unatoa usawa (equity) kwa mwanafunzi kulingana na hali ya uchumi wa familia yake na si kigezo cha kozi anayosoma pekee (mfano mwanafunzi mtoto wa mbunge ama wa waziri analipiwa gharama zote bure wakati mtoto wa maskini anayesomea biashara anatakiwa kujilipia aidha ada yote ama sehemu ya ada hiyo).

Naomba kujua profile yako ya elimu na je hi Dr. unayoitwa ni ipi? je MD au PHD
 
Hapo namba moja umesahau kitu muhimu kuliko vyote, VYOO, tunahitaji mashuleni vyoo vingi na bora.

.........Duuuh!! CCM mna mambo nyie watu!!!. Unamuambia huyo jamaa ajenge vyoo vingi na bora kabla hajawa Rais wakati JK kashindwa aliekuwepo madarakani.

Hii nchi ni kituko aisee!!
 
.......mmmh! nina mashaka sana na uchaguzi wa mwaka huu. HKigwangalla wakati unagombea nafasi ya kupitishwa na Chama kugombea ubunge nasikia mlikuwa mnatafutana na bastola na Bashe, sasa hivi unautaka Urais si utakuwa umenunua Kifaru na mabomu?
 
.........Duuuh!! CCM mna mambo nyie watu!!!. Unamuambia huyo jamaa ajenge vyoo vingi na bora kabla hajawa Rais wakati JK kashindwa aliekuwepo madarakani.

Hii nchi ni kituko aisee!!

Soma tena sentensi yangu halafu unioneshe ni wapi nime"muambia huyo jamaa ajenge vyoo"?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Ndg. Zigizaga,

Uchaguzi wa Urais si jambo la uzoefu tu, kwa zaidi ni jambo la dhamira ya kuleta mapinduzi ya hali ya maisha ya kesho (elections are about the future, not the past). Hivyo naelezea future ya Tanzania itakuwaje kama nikiwa Rais, nipime kwa hilo.

Hata hivyo, ukitaka rekodi yangu, tazama miaka mitano ya ubunge wangu, tazama pia miaka mitano ya kufanya kazi kwenye kampuni (biashara), miaka mitano ya kuwa mwanaharakati, mwanazuoni na mtafiti. Tazama pia rekodi yangu ya uongozi kwenye chama. Tazama pia formative years na namna nilivyoandaliwa na mfumo kuwa kiongozi. Ukiona sitoshi, ninyime kura yako. Ukiona natosha nipigie debe wakati ukifika.

Rekodi inaonesha umelelewa kwenye mfumo na chama cha kifisadi. Sioni kipya utakacholeta ukiwa ndani ya CCM zaidi ya kuendeleza wizi.

Labda uweke nia kwa fasheni ya kuweka nia ila sioni mtu ndani ya CCM mwenye uwezo wa kwenda kinyume na mfumo aliolelewa nao.
 
URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!


(5.) Kurekebisha mfumo wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa kuweka mfumo ambao unatoa usawa (equity) kwa mwanafunzi kulingana na hali ya uchumi wa familia yake na si kigezo cha kozi anayosoma pekee (mfano mwanafunzi mtoto wa mbunge ama wa waziri analipiwa gharama zote bure wakati mtoto wa maskini anayesomea biashara anatakiwa kujilipia aidha ada yote ama sehemu ya ada hiyo).

Kigwa, wewe mwenyewe ni daktari lakini huwa nnapata kigugumizi hata kukuita Daktari.

"equity" toka lini ikawa ni usawa?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Hapo namba moja umesahau kitu muhimu kuliko vyote, VYOO, tunahitaji mashuleni vyoo vingi na bora.

Mmeshindwa kujenga vyoo miaka 50 iliopita iweje leo huyu msukuma aweze kutujengea vyoo shule zote kwa miaka mitano?
 
Kuna watu mnataka kuufanya urais ni kama kuwa katibu kata. Wekeni heshima kwenye hiko cheo, hiyi ni dharau kwa watanzania.
 
Kigwa, wewe mwenyewe ni daktari lakini huwa nnapata kigugumizi hata kukuita Daktari.

"equity" toka lini ikawa ni usawa?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

.......Usimshangae huyo, hizo ndo akili zenu zinavyowatuma kuandika. CCM hamna tofauti sana kichwani.
 
Sasa hapo iko wapi Kigwa "akajenge" kama ulivyoandika mwanzo?

Hivi hizo shule huwa mnakwenda kusomea ujinga?
........Wee kweli umezeeka, ni afadhali uwe umezeeka macho tu kuliko akili na vingine. Wapi nilimtaja Kigwa kwenye comment yangu ya mwanzo?

Kumbe uzee ndo unavyokuwa hivi?
 
........Wee kweli umezeeka, ni afadhali uwe umezeeka macho tu kuliko akili na vingine. Wapi nilimtaja Kigwa kwenye comment yangu ya mwanzo?

Kumbe uzee ndo unavyokuwa hivi?

Huo "uijnga" wa "kujenga" katika huu upunguani wako umeusahau?

.........Duuuh!! CCM mna mambo nyie watu!!!. Unamuambia huyo jamaa ajenge vyoo vingi na bora kabla hajawa Rais wakati JK kashindwa aliekuwepo madarakani.

Hii nchi ni kituko aisee!!

Hivi hiyo shule ulienda kusomea ujinga?
 
...Kuna watu naona jamii forum inawapa gut za kusema wawe marais kisa amebonyezewa like mbili tatu, yaani kigwangala ndugu yangu hata watanzania wote wakihamishiwa kenya ukabaki wewe na ukoo wako huwezi kuwa rais kwasababu wewe sio president material! Kigwangala ndugu yangu kwanini unahangaika uspoteze muda umekopi speech ile umeitoa humu tukakwambia mbona unafanya plagiarism lakini hukomi, kigwangala kaka. Tafadhali tafuta ubunge kwa dhati maana hata uwaziri hujawahi kuupata!
 
Ndg. Zigizaga,

Uchaguzi wa Urais si jambo la uzoefu tu, kwa zaidi ni jambo la dhamira ya kuleta mapinduzi ya hali ya maisha ya kesho (elections are about the future, not the past). Hivyo naelezea future ya Tanzania itakuwaje kama nikiwa Rais, nipime kwa hilo.

Hata hivyo, ukitaka rekodi yangu, tazama miaka mitano ya ubunge wangu, tazama pia miaka mitano ya kufanya kazi kwenye kampuni (biashara), miaka mitano ya kuwa mwanaharakati, mwanazuoni na mtafiti. Tazama pia rekodi yangu ya uongozi kwenye chama. Tazama pia formative years na namna nilivyoandaliwa na mfumo kuwa kiongozi. Ukiona sitoshi, ninyime kura yako. Ukiona natosha nipigie debe wakati ukifika.
HK nikupe ushauri kidogo jifunze kutoka kwa wenzako jinsi wanavyo weza kujibu hoja za watu wanao tofautiana kima wazo! Acha panic na jeuri!!
 
Back
Top Bottom