URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

HKigwangalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
722
Reaction score
971
URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

Kwenye awamu ya nne tumeshuhudia Serikali ya CCM ikijenga shule nyingi na kuzalisha na kuajiri walimu wengi kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi yetu. Tumeshuhudia vyuo vingi vya elimu ya kati vikipanda hadhi na kuwa vya elimu ya juu, na tumeshuhudia idadi ya wahitimu wenye elimu ya chuo kikuu wakiongezeka mwaka hadi mwaka. Sambamba na jitihada hizi, tumeshuhudia wahitimu wakifanya usaili wa mchujo wa awali kwa ajili ya nafasi za kazi kwenye uwanja wa Taifa. Tumeshuhudia baadhi ya taasisi zikilalamikiwa kwa kutoa ajira kwa undugunaizesheni. Hii inatanabaisha kuwa tuna tatizo si tu la kukosa elimu yenye kutoa ujuzi wa kujiajiri bali pia tuna wasomi wengi wenye elimu ya juu kushinda mahitaji ya soko la ajira. Tumeshuhudia shule za kata zikitoa wahitimu wenye ubora ambao wamekuwa wakisonga mbele zaidi kwenye masomo yao, huku wengine wengi wakifeli . Ni lazima tufanye paradigm shift.

Ni wazi kwamba hatupaswi kuendelea kuwekeza kwenye kusomesha watu wetu kwenye elimu ya juu kwa kipindi hiki, pengine tujikite zaidi kuwekeza kwenye kuongeza ubora na kwenye utafiti na teknolojia.

Nini tunahitaji kwenye elimu sasa?

Tunahitaji:

(1.) Kuongeza ubora wa shule zetu kwa kujenga maabara, maktaba, mabweni, viwanja vya michezo, karakana (zinapohitajika) na nyumba za walimu. Pia kuhakikisha shule zote nchini zinakuwa na umeme, maji na mtandao mzuri wa mawasiliano ili kuongeza ari ya walimu kuishi kwenye maeneo yote bila kuchagua (retention scheme).

(2.) Kuboresha mitaala ili kuifanya elimu yetu iwape wanafunzi si tu elimu ya ufahamu bali pia ya ujuzi na uvumbuzi; na zaidi component ya elimu ya ujasiriamali na communication skills ni lazima.

(3.) Tuanzishe mfumo wa motisha kwa walimu wetu kulingana na jiografia na mazingira wanapofanyia kazi (differential incentives scheme). Walimu wanaofundisha maeneo ya mbali na makao makuu ya wilaya na wanaofundisha kwenye maeneo yasiyo na huduma mbalimbali muhimu ni lazima walipwe posho maalum zaidi ya wenzao wanaofundisha maeneo ya mijini.

(4.) Kuwa na mpango wa dharura wa kuanzisha shule za VETA kwa kuamua kuzigeuza baadhi ya shule za sekondari kuwa za VETA na kuziwezesha zipate vifaa na wakufunzi wenye ujuzi ili zianze mara moja kutoa mafunzo kwa vijana waliohitimu darasa la saba na hawakupata fursa ya kusonga mbele, na kwa wale waliohitimu kidato cha nne na hawakupata fursa ya kusonga mbele, na hivyo hivyo kwa waliohitimu kidato cha sita. Mpango huu utatoa fursa ya kupata vijana wengi wenye ujuzi kwa haraka kwa ajili ya kujenga vijiji na miji yetu (mafundi uashi, ubunifu wa mavazi, ushonaji nguo, useremala, mafundi bomba, umeme, madereva, mafundi mitambo, mabwana shamba vijijini n.k.). Shule za VETA zitatoa fursa kwa vijana waliopoteza matumaini, zitawapa ujuzi wa kujiajiri, lakini pia wahitimu wa VETA wanahitajika sana kwenye ajira za sekta binafsi.

(5.) Kurekebisha mfumo wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa kuweka mfumo ambao unatoa usawa (equity) kwa mwanafunzi kulingana na hali ya uchumi wa familia yake na si kigezo cha kozi anayosoma pekee (mfano mwanafunzi mtoto wa mbunge ama wa waziri analipiwa gharama zote bure wakati mtoto wa maskini anayesomea biashara anatakiwa kujilipia aidha ada yote ama sehemu ya ada hiyo).
 
Hivi HK, mmekuwa wapinzani ghafla?? Maana mnayo ongea hivi sasa tulizowea kuyasikia CHADEMA, CUF, NCCR na NLD sasa tuambieni nyie ni wagombea kwa chama gani maana mmejivua ufahamu na kuwa wapinzani. Watanzania sio wajinga tena.
 
Hamis Kigwangala kwa kudandia hoja za watu hujambo.. atleast uwe una acknowledge basi kuwa Lowassa ameipa elimu kipaumbele 1,2,3... CHADEMA waliiweka kwenye ILANI yao ya 2010... Wewe vipaumbele vyako ni nini? au utaungana na Wassira na Nchemba kujaribu kuzuia mafuriko kwa mkono?... Mtajitahidi sana ku-neutralise speed ya Lowassa lakini nawahakikishia hamtaweza... Membe hakubaliki ... nasikia Kamani nae yuko Mbioni kutangaza nia kwaniaba ya Membe ...
 
Kigwangala kale maharage ulale! Una rekodi gani ya kujivunia katika taifa hili mpaka tukuamini tukupe nchi hiii! Hili ni suala zito siyo kukurpuka tu her nataka niwe rais! Eleza sasa ulichofanyia taifa ili tukuamini kama VIP kale maharage ulale
 
Maunvi mzigo umeshakuwa mzito kwake! Hana jipya tens Jana kabolonga ile mbaya!
Kabolonga kwako. Msemo wa "Mzigo mzito mpe mnyamwezi" hauko applicable kwa huyu dogo hata kama ni mnyamwezi.
 
Hata umupake mafuta ya ng'ombe Edo amelemeti! Nyie ndo mnamdanganya mnapiga madili yako! Siku zinakuja mtamkimbia
 
Bora Edo kuliko huyu mwenye bandiko. Nchi hii ina watu wa hovyo sana, wengine kama hawa kuwahi kuwa KAKA WAKUU huko shule za msingi wanadhani na Uraisi wanaweza. Hovyooo.....
 
Hamis Kigwangala kwa kudandia hoja za watu hujambo.. atleast uwe una acknowledge basi kuwa Lowassa ameipa elimu kipaumbele 1,2,3... CHADEMA waliiweka kwenye ILANI yao ya 2010... Wewe vipaumbele vyako ni nini? au utaungana na Wassira na Nchemba kujaribu kuzuia mafuriko kwa mkono?... Mtajitahidi sana ku-neutralise speed ya Lowassa lakini nawahakikishia hamtaweza... Membe hakubaliki ... nasikia Kamani nae yuko Mbioni kutangaza nia kwaniaba ya Membe ...

Kivipi? Hii hoja nimeandika kwenye #Kigwanomics miaka minne iliyopita, nenda kasome.

Bila shaka Mhe. Lowassa ama washauri wake waliisoma mle na kumuandikia, siyo mbaya akinukuu, maana kitabu ni public document, siyo siri. Na siwezi kulalamika hata kidogo, maana niliandika ili watu wasome na watumie.

Hata hivyo mimi elimu si kipaumbele cha kwanza, cha kwanza ni kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha ajira nyingi kupitia kilimo, viwanda na biashara - vyote vikiwa linked na kilimo (#AjiraKwanza), cha pili ni kuboresha huduma za jamii na cha tatu ni Kudumisha utawala bora. Tuna tofauti kidogo. Pole.
 
Umasikini Nzega kabla hujawa mbuge hali ilikuaje? Baada ya wewe kuwa mbunge miaka hii mitano ni kwa asilimia ngapi umesaidia kuupunguza?
 
Kigwangala kale maharage ulale! Una rekodi gani ya kujivunia katika taifa hili mpaka tukuamini tukupe nchi hiii! Hili ni suala zito siyo kukurpuka tu her nataka niwe rais! Eleza sasa ulichofanyia taifa ili tukuamini kama VIP kale maharage ulale
Ndg. Zigizaga,

Uchaguzi wa Urais si jambo la uzoefu tu, kwa zaidi ni jambo la dhamira ya kuleta mapinduzi ya hali ya maisha ya kesho (elections are about the future, not the past). Hivyo naelezea future ya Tanzania itakuwaje kama nikiwa Rais, nipime kwa hilo.

Hata hivyo, ukitaka rekodi yangu, tazama miaka mitano ya ubunge wangu, tazama pia miaka mitano ya kufanya kazi kwenye kampuni (biashara), miaka mitano ya kuwa mwanaharakati, mwanazuoni na mtafiti. Tazama pia rekodi yangu ya uongozi kwenye chama. Tazama pia formative years na namna nilivyoandaliwa na mfumo kuwa kiongozi. Ukiona sitoshi, ninyime kura yako. Ukiona natosha nipigie debe wakati ukifika.
 
Bora Edo kuliko huyu mwenye bandiko. Nchi hii ina watu wa hovyo sana, wengine kama hawa kuwahi kuwa KAKA WAKUU huko shule za msingi wanadhani na Uraisi wanaweza. Hovyooo.....
Ndg. Zigizaga,

Uchaguzi wa Urais si jambo la uzoefu tu, kwa zaidi ni jambo la dhamira ya kuleta mapinduzi ya hali ya maisha ya kesho (elections are about the future, not the past). Hivyo naelezea future ya Tanzania itakuwaje kama nikiwa Rais, nipime kwa hilo.

Hata hivyo, ukitaka rekodi yangu, tazama miaka mitano ya ubunge wangu, tazama pia miaka mitano ya kufanya kazi kwenye kampuni (biashara), miaka mitano ya kuwa mwanaharakati, mwanazuoni na mtafiti. Tazama pia rekodi yangu ya uongozi kwenye chama. Tazama pia formative years na namna nilivyoandaliwa na mfumo kuwa kiongozi. Ukiona sitoshi, ninyime kura yako. Ukiona natosha nipigie debe wakati ukifika.
 
Kivipi? Hii hoja nimeandika kwenye #Kigwanomics miaka minne iliyopita, nenda kasome.

Bila shaka Mhe. Lowassa ama washauri wake waliisoma mle na kumuandikia, siyo mbaya akinukuu, maana kitabu ni public document, siyo siri. Na siwezi kulalamika hata kidogo, maana niliandika ili watu wasome na watumie.

Hata hivyo mimi elimu si kipaumbele cha kwanza, cha kwanza ni kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha ajira nyingi kupitia kilimo, viwanda na biashara - vyote vikiwa linked na kilimo (#AjiraKwanza), cha pili ni kuboresha huduma za jamii na cha tatu ni Kudumisha utawala bora. Tuna tofauti kidogo. Pole.
twambie ccm tatizo no mfumo mbovu wa uongozi, mahakam na bunge utafanya mini kuondo mfumo mbovu huu! Maana hat kama were no msafi kwa mfumo huh utachafuka tu na utaonekana umeshindwa kazi, utafanya mini sasa kwa hili!
 
CCM nahisi wameanza kuchanganyikiwa!!! mpaka huyu naye anataka uraisi? hivi mnafikiri uraisi ni pipi? naona hata Ridhiwani atatangaza nia
poleni sana kwa kudandia treni bwana wadoo
 
ndiyo kwanza mchakato unaanza, tusivuke mto kabla ya kuufikia.
Sijui umekula matobolwa ya wapi we kijana. Chonde chonde na UKAKA MKUU wako wa shule ya msingi, usitake kutuletea ktk taasisi kubwa kama unayojishaua nayo.
 
Tafunaneni kama senene kwenye chupa kwanza mkichoka sisi tunamalizia kazi,UKAWAAAA
 
Ndg. Zigizaga,

Uchaguzi wa Urais si jambo la uzoefu tu, kwa zaidi ni jambo la dhamira ya kuleta mapinduzi ya hali ya maisha ya kesho (elections are about the future, not the past). Hivyo naelezea future ya Tanzania itakuwaje kama nikiwa Rais, nipime kwa hilo.

Hata hivyo, ukitaka rekodi yangu, tazama miaka mitano ya ubunge wangu, tazama pia miaka mitano ya kufanya kazi kwenye kampuni (biashara), miaka mitano ya kuwa mwanaharakati, mwanazuoni na mtafiti. Tazama pia rekodi yangu ya uongozi kwenye chama. Tazama pia formative years na namna nilivyoandaliwa na mfumo kuwa kiongozi. Ukiona sitoshi, ninyime kura yako. Ukiona natosha nipigie debe wakati ukifika.
Nimekuuliza suala la umaskini nzega umelipunguza kwa asilimia ngapi una bwabwaja tu. Hivi hiyo PHD yako uli-specialize kusomea ujinga? Swali dogo kama hili unashindwa, je kwa masswala magumu utaweza wewe bwana mdogo?
 
URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

Kwenye awamu ya nne tumeshuhudia Serikali ya CCM ikijenga shule nyingi na kuzalisha na kuajiri walimu wengi kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi yetu. Tumeshuhudia vyuo vingi vya elimu ya kati vikipanda hadhi na kuwa vya elimu ya juu, na tumeshuhudia idadi ya wahitimu wenye elimu ya chuo kikuu wakiongezeka mwaka hadi mwaka. Sambamba na jitihada hizi, tumeshuhudia wahitimu wakifanya usaili wa mchujo wa awali kwa ajili ya nafasi za kazi kwenye uwanja wa Taifa. Tumeshuhudia baadhi ya taasisi zikilalamikiwa kwa kutoa ajira kwa undugunaizesheni. Hii inatanabaisha kuwa tuna tatizo si tu la kukosa elimu yenye kutoa ujuzi wa kujiajiri bali pia tuna wasomi wengi wenye elimu ya juu kushinda mahitaji ya soko la ajira. Tumeshuhudia shule za kata zikitoa wahitimu wenye ubora ambao wamekuwa wakisonga mbele zaidi kwenye masomo yao, huku wengine wengi wakifeli . Ni lazima tufanye paradigm shift.

Ni wazi kwamba hatupaswi kuendelea kuwekeza kwenye kusomesha watu wetu kwenye elimu ya juu kwa kipindi hiki, pengine tujikite zaidi kuwekeza kwenye kuongeza ubora na kwenye utafiti na teknolojia.

Nini tunahitaji kwenye elimu sasa?

Tunahitaji:

(1.) Kuongeza ubora wa shule zetu kwa kujenga maabara, maktaba, mabweni, viwanja vya michezo, karakana (zinapohitajika) na nyumba za walimu. Pia kuhakikisha shule zote nchini zinakuwa na umeme, maji na mtandao mzuri wa mawasiliano ili kuongeza ari ya walimu kuishi kwenye maeneo yote bila kuchagua (retention scheme).

Hapo namba moja umesahau kitu muhimu kuliko vyote, VYOO, tunahitaji mashuleni vyoo vingi na bora.
 
Back
Top Bottom