Uraia pacha/dual nationality, tunakwama wapi kama taifa?

Roho mbaya tu za ma CCM!

Nilikuwa natizama.michezo ya olympics mashindano ya kuogelea na michezo ambayo ni white dominated. Unakuta wenzetu kama Eq Guinea, Mauritania nk wanawakilishwa na watoto ambao wazee wao wana uraia pacha. Mimi personally, kwa roho mbaya hizo za viongozi wetu siwezi kumshauri mtoto wangu aiwakilishe hii nchi.

Eti watafanya uhalifu halafu wakimbilie nchi zao za pili! Kwani hakuna extradition treaty? Jee hakuna raia wa nchi nyengine katika jela zetu? Ni roho mbaya tu hakuna jengine. Kuna watu wasiopungua milioni moja ambao wako elligible kwa uraia pacha wa Kitanzania. Talking about kukusanya kodi, hawa wote wangweza kuchangia pato la taifa tumebakia kuwanyonya wanyonge tu sasa hivi. Bei ya mafuta ya aina yoyote unayijuwa wewe, ikiwa ya fuel, body oil au cooking oil ni kubwa Tanzania kuliko Ulaya! Bei za mboga zinashuka wakati pembejeo zinapanda bei. Hakuna hela kitaa!
 
Amueni moja tuu,Kama majuu kunalipa kaeni huko,Kama vipi TZ mnakupenda rudini tujenge Tanzania ya viwanda.

Maana hamchelewagi kuanza vurugu kwa kisingizio Cha demekrasi maana mnapakukimbilia Kama bwa na yuleee wa Ubelgiji.
 
Nafikiri uje mkeka comprehensive wa faida na hasara...kwa individuala na Serikali

Kama mnataka kuishauri Serikali
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwa miaka kadhaa sasa, kumekuwa na mijadala kadhaa Tanzania kuhusu uwezekano wa Watanzania kuwa na uraia pacha.

Serikali imekuwa na woga wa kutoa uraia pacha kwa hoja kwamba itaongeza hofu ya usalama (security issuesTu), kwamba mtu anafaya kosa Tanzania kwa uraia wa Tanzania then anakimbilia nje kwenye uraia wa pili.

Hoja hii mie naipinga sana kwa sababu kuna utaratibu wa kimataifa wa kukabiliana na uhalifu (cross border crime controls) kuna ushirikiano wa kipolisi kimataifa (Interpol).

Tunapoteza vingi sana kwa kutokua na uraia pacha, hasa kimapato. Tulijadili sana hili suala kwenye katiba pendekezwa miaka ile, ila likapingwa na wajumbe wa bunge la katiba.

Ningeomba serikali ilione hili kwa macho marefu, iruhusu uraia pacha.
Tunakwamishwa na ubinafsi wa wale walioishi ughaibuni na kurudi wakapewa vyeo wakajisahau.
bun
Wapo watoto wa vigogo wenye uraia pacha nje ya nchi na kuna wake wa vigogo ambao wakikaribia kujifungua wanafungasafari kwenda US, Canada na ulaya ili watoto wao wapate uraia pacha. Hao hao ndo wakiingia bungeni ndo wa kwanza kuhakikisha hakuna hicho kitu.

Most of the time ni wale waliokuwa maofisa balozini hivyo they are not politicians and the can not make any law.
 
Faida ni nyingi sana sijui hasara kusema kweli. Membe wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alitembelea nchi nyingi za Africa na kule Carribean ambazo zinaruhusu uDC ule kujifunza umuhimu/hasara za uraia pacha ambazo Serikali hizo na hitimisho la Membe kutoka Serikali hizo ni kwamba faida ni kubwa sana hakukuwa na hasara. Nakumbuka Afrika alienda pia Ghana na Nigeria.
Nafikiri uje mkeka comprehensive wa faida na hasara...kwa individuala na Serikali

Kama mnataka kuishauri Serikali
 
Amueni moja tuu,Kama majuu kunalipa kaeni huko,Kama vipi TZ mnakupenda rudini tujenge Tanzania ya viwanda.

Maana hamchelewagi kuanza vurugu kwa kisingizio Cha demekrasi maana mnapakukimbilia Kama bwa na yuleee wa Ubelgiji.
Hapo umbegugi ndugu yangu. Diaspora anachangia pato la nchi kikubwa tu. Ulizia mabenki na miamara uone wanavyoongeza pato kwa kutuma pesa nchini.
 
Kwa miaka kadhaa sasa, kumekuwa na mijadala kadhaa Tanzania kuhusu uwezekano wa Watanzania kuwa na uraia pacha.

Serikali imekuwa na woga wa kutoa uraia pacha kwa hoja kwamba itaongeza hofu ya usalama (security issues), kwamba mtu anafaya kosa Tanzania kwa uraia wa Tanzania then anakimbilia nje kwenye uraia wa pili.

Hoja hii mie naipinga sana kwa sababu kuna utaratibu wa kimataifa wa kukabiliana na uhalifu (cross border crime controls) kuna ushirikiano wa kipolisi kimataifa (Interpol).

Tunapoteza vingi sana kwa kutokua na uraia pacha, hasa kimapato. Tulijadili sana hili suala kwenye katiba pendekezwa miaka ile, ila likapingwa na wajumbe wa bunge la katiba.

Ningeomba serikali ilione hili kwa macho marefu, iruhusu uraia pacha.
Ni viongozi tunaowachaguwa au wanaoiba kura kujifanya wanajuwa kuliko sisi! Kujifanya wanajuwa lipi bora kwetu. Uoga wao ndio mateso yetu.
Wanatupa hasira sana kwa kweli…
 
kukiwa na uraia pacha utawanyima watawala ccm kushindwa kukubana maana haki zako za msingi zita simamiwa na nchi nyingine
 
Back
Top Bottom