Uraia/ labels | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uraia/ labels

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Injinia, Mar 29, 2010.

 1. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna jambo linanitatiza sana kuhusu uraia wa hii nchi inaitwa Marekani (United States of America).

  Raia wa nchi hii ambao ni weusi huitwa African-Americans, haijalishi kama raia huyo ametokana na kizazi kirefu cha waliokuwa waafrika waliopelekwa huko kama watumwa au kama ni raia aliepata uraia wa Marekani yeye binafsi ambapo kabla alikuwa raia wa ama nchi ya Kiafrika au nchi za Caribbean.

  Wamarekani wa asili ya bara Asia nao vivyo hivyo, huitwa Asian-Americans. Wa Amerika ya Kusini Latin/ Hispanic/Mexican-Americans

  Wale wazawa halisi wa Marekani, yaani Wahindi Wekundu (Red Indians) wao huitwa Native Americans.

  Kabila/ raia pekee wasiokuwa na hiki kitambulishi/ label ni wazungu wenye asili ya bara Ulaya. Kwa nini na wao wasiitwe European-Americans?

  Naomba tujadiliane chanzo na sababu za hivi vitambulishi
   
Loading...