Urafiki wa Joseph Mbilinyi (Sugu) na Rais Samia unampa shida Dkt. Tulia

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,608
8,749
Sugu na Mama ni marafiki bila kujali siasa. Hakuna kitu wala mtu yeyote anaweza kubadilisha hilo maana ndiyo ubinadamu kuna wakati watu wanakuwa marafiki bila kujali siasa.

Uhusiano wa Dkt. Tulia na Rais ni wa kisiasa tu na ni vigumu kuona hata Mama akicheka akiwa na Tulia.

Hii inamuogopesha sana Dkt. Tulia lakini ukweli ni kwamba hakuna kitu ambacho anaweza kufanya.

Tulia ni mtu ambaye amebebwa kuanzia wakati wa Magufuli na Mama anajua hilo na kibaya Mama hamuamini kabisa anajua anafanya kila kitu kisiasa.

Kuna mawili apendekeze jimbo waligawe mara mbili au wamuahidi viti maalumu lakini kihalali ukiangalia mikutano hatoweza kumshinda Sugu ambaye anazidi kuwa maarufu kila siku.

Kitu ambacho hajui Mama na Wazanzibari wanataka Katiba mpya wakati huu ambao mwenzao ni Rais hivyo hilo ni muhimu kuliko Dkt. Tulia kushinda kwa Rais.
 
Dkt. Samia na Sugu hakuna urafiki wowote, Sugu katika maongezi yake anamuhusisha Rais wetu katika kuwa - brainwash Wanambeya, (kwamba hata Rais wenu yupo pamoja nami) that what he did, Rais akiwa pamoja na wewe na kama wewe ni mtendaji bora hukupa nafasi bila choyo, wana Mbeya lazima waelewe na wajinasue katika mtego huo fake!

ANGALIZO:
Wana Mbeya mlishakosea sana huko nyuma, pimeni, mjitafakari, msikosee tena, msitumiwe kama ngazi ya maendeleo ya mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom