Urafiki, mipaka na mahaba

Roca fella

JF-Expert Member
May 13, 2023
1,247
2,338
Hii ni stori ya ukweli iliyo tokea nchini Tanzania, jijini Arusha mnamo mwaka 2021, mwezi wa septemba ( 9 ) tarehe Kama ya leo 09.

usiku wa saa 7, mwanadada mrembo aliye amua kujiua mwenyewe, kuilazimisha roho itoke pasipo idhini ya Mola Mlezi. Watoto , ndugu , Jamaa na marafiki mpaka majirani walihuzunishwa na kifo hiki Cha ghafla Cha mpendwa wao Irene ( jina bandia )

kisa kilikuwa hivi......

irene ni mwana mama aliye olewa na mjasiria mali, mwenye familia ya watoto watatu, 3 kwa upande wa uchumi aliridhika nao, uchumi wa wastani. Huyu Irene alikuwa na rafiki yake wa karibu mno tokea utotoni, mpaka wanakuwa watu wazima.

huyu rafiki yake julieth ( jina bandia ) alizoea kupewa kiasi kadhaa Cha fedha kutoka kwa Irene, pindi anapo kwama ama kutunukiwa na rafiki yake kipenzi,

julieth alikuwa anafahamu mbivu na mbichi za Irene, Siri nyingi alifahamu, wakati ule Irene akienda kwa mchepuko wake mwenye kujaliwa uchumi imara, akihongwa mpaka milioni 3 keshi, rafiki yake julieth aliambulia chochote.

hapa shetani alimpitia julieth, kwa maana julieth alipata ujasiri wa kwenda nyumbani kwa rafiki yake kipenzi Irene, kumkuta mama mkwe na kufitinisha rafiki yake, kuthibitisha maovu ya Irene, akapiga simu na kuweka loud speaker, wakazungumza kana kwamba wapo wawili, mwana mama Irene akajiachia akaeleza yupo kwa mchepuko wake Kama kawaida, huku akimtolea mbovu mama mkwe wake bila kujua simu iko loud kila kitu kipo wazi, maongezi yote yanasikika.

irene kurudi nyumbani baada ya kutoa kumpa raha na burudani mchepuko wake ikiwa pia alirudi na kibunda, nyumbani watu walikuwa mbogo, si mama mkwe si mumewe, hakuna wa kumwelewa Irene ingawaje ushahidi upo kwa mama mkwe kupitia simu ya rafiki yake julieth katika maongezi ya awali, mume akamsikiliza mama yake kuwa Irene ni mtovu wa nidhamu, ametia ndoa aibu, ndoa imeingia doa. Hivyo afukuzwe.

kwa hasira ya mama mkwe na mwanaye walilazimika kumtoa usiku ule ule aende kwao, Irene hakuwa na namna Kama kulia imetosha, msamaha aliomba zaidi ya mara 20, ilibidi akubali matokeo, aliondoka kurudi kwao na kupokelewa na wazazi wake wote wawili. Akaeleza shida na taabu zilizo mleta usiku ule, maana nyumbani kwao na kwa mumewe si mbali ni kilometa kadhaa kufikia.

irene aliingia chumbani mwenye mawazo, hasira, maamuzi magumu, na kulia mpaka kwi kwi. Irene aliamua kunywa sumu na kupoteza uhai wake.

1. Kwanini Irene alijiua, kwa sababu alishindwa kuvumilia aibu, fedheha, dharau za rafiki yake kumweka uchi hadharani kwa kusema maovu yake, huku pesa anasaidiwa, rafiki yake amemsaliti.

2. Mama mkwe ana kosa la kukaa nyumbani kwa mwanae kwa muda mrefu hii pia kuchangia ndoa nyingi kuvunjika.

3. Mumewe, hakuwa makini kufanya maamuzi sahihi, kumtukuza mke kwa nyakati za usiku si vyema, Mambo ya mahusiano malizeni utofauti zenu kwa utaratibu sio hasira baadae ni hasara.

4. Julieth, ndiyo chanzo Cha yote haya, wivu wa mapenzi, kwanini yeye hana mchepuko wa kumhonga hela nyingi, kwanini akamwanike mwenzake maovu yake kwq familia yake, kwanini awe msaliti.

maisha yana Mambo mengi mno changamoto lukuki,
Kuwa makini na marafiki zako.

rafiki yako, ndugu na Jamaa wawe na mipika yake katika mahusiano yenu.

wazazi wetu tunao ishi nao wawe na hekima , busara, na maarifa kutatua migogoro ya ndoa wawe imara na vinara kutuliza ndoa na si kuiwekea sumu.

wewe binafsi usiwe mwepesi kufanya maamuzi magumu, usikate tamaa na changamoto unazo pitia, huu ndiyo mfumo wa maisha wa kiumbe hai katika hii sayari,
kujiua sio suhulisho wa tatizo lako, utulivu wa akili, mshirikishe Mola wako Mlezi, akuepushie majaribu, usikate tamaa Kuna maisha mengine baada ya hayo.

Kuchepuka sio lazima ila unaweza kupunguza Kama hautojali, usianike Mambo yako hadharani kila mmoja au rafiki yako ajue, hao hao ndio maadui baadaye.

MAREHEMU ALALE ANAPO STAHILI.
 
Lenye mwanzo halikosi mwisho, mwisho wa usaliti wa Irene ndio huo.

Julieth ndio chanzo kivipi? Irene ndio chanzo cha kifo chake mwenyewe(msaliti)

NB: Unapofanya kitu kwa makusudi uwe tayari kuyabeba matokeo yake +-.
 
Lenye mwanzo halikosi mwisho, mwisho wa usaliti wa Irene ndio huo.

Julieth ndio chanzo kivipi? Irene ndio chanzo cha kifo chake mwenyewe(msaliti)

NB: Unapofanya kitu kwa makusudi uwe tayari kuyabeba matokeo yake +-.
ikiwa rafiki, au ndugu yako wa karibu kukueleza jambo fulani la Siri, Basi mtunzie Siri usitoe Siri yake.

Julieth amemsaliti mwenzake kwa kutoa Siri. Wakati ilikuwa ni makubaliano ya wote kutunza Siri.
 
Siri inatakiwa ibaki kuwa ya mtu mmoja, Irene aliyakanyaga mwenyewe kwa kuvujisha Siri kwa rafiki Yake Julieth
 
Back
Top Bottom