Upweke unasababisha natumia pesa kwa kiwango kikubwa sana

iamriq_arthur

JF-Expert Member
May 1, 2021
377
884
Natumai ni wazima wa afya nyote.

Mimi nahisi nina tatzo langu binafsi la kutumia pesa nyingi pindi ninapokua mpweke, najikuta nafanya vitu vingi vinavyonigharimu pesa nyingi ili moyo wangu uwe na furaha na amani,

Naombeni ushauri na ufafanuzi kuhusu hili jambo, huwa ni kwangu tu ama hata kwenu nyinyi kwa upande wenu pindi muwapo na stress/ upweke huwa mnajikuta mnafanya vitu vingi vyenye kutumia gharama kubwa ili ku-kutuliza upweke na stress.?
 
Hiyo inawatokea nyie wenye pesa nyingi. Sisi wengine tukiwa na stress tunalala tu, na usingizi ukigoma kuja, tunaishia kufumba macho kwa lazima.
 
Ila pamoja na yote ,mi nimemuelewa
Unaweza ukawa na Kila kitu,au ukawa na uwezo wa kupata Kila kitu unachokihitaji, lakini upweke ukakufanya uone hata ulivyo navyo havina maana!

Pesa sio Kila kitu,unapokua huna , unadhani una stress sbb huna
Na ukipata ndo utaelewa ....

Loneliness kills!

Mungu akusaidie sana!
 
Back
Top Bottom