julyhero
Member
- May 18, 2018
- 45
- 22
Ninakuja kwenu Wakuu kwa unyenyekevu, kwa namna ambavyo nimeona watu wanasaidika kimawazo kupitia jukwaa hili la JF. Ninawasalimu nyote. Naomba nilete kwenu changamoto ambayo nimekuwa nayo muda mrefu sasa.
Mimi ni kijana mwenye umri chini ya miaka 30. Mama yangu alifariki nikiwa na miezi mitatu. Baba alikimbia majukumu baada ya kumzika mama. Bibi na babu wakanilea, na kunianzisha shule, hadi walipofariki nikiwa bado shule ya msingi. Nimepitia changamoto nyingi za kimaisha tangu walipofariki walezi wangu hawa, ikiwemo kuishi kwa ndugu tofautitofauti (kutokuwa na makazi maalumu), huku nikiendelea na masomo.
Ninamshukuru sana Mungu kwa ajili ya wote waliojitoa kwa namna yeyote ile kunisupport kimaisha na kielimu. Pia, ninaishukuru sana serikali yetu (Awamu ya Nne) kwa sera nzuri zilizosaidia na mimi kupata mkopo wa elimu ya juu. Mungu wa mbinguni awabariki.
Mungu alinisaidia, nikamaliza degree yangu salama, na sasa niko kazini. Katika kipindi chote hicho nimekutana na watu wa aina zote. Nilipata marafiki, wakike na wakiume. Wengine niko nao bado, wengine walikuwa ni wa muda mfupi. Kuhusu mahusiano sijawahi kuwa kwenye relationship, japo nishawahi kupenda.
Kama kichwa cha thread kilivyo, niko mpweke. Siyo kwamba sijichanganyi, ninajichanganya, lakini deep inside Ni mpweke. Dhoruba nyingi nimepitia. Mtu pekee (Rafiki) aliyekuwa karibu nami tukapendana genuinely na nikafurahia maisha ni bibi yangu aliyenilea (Mungu am'bariki huko aliko). Bibi yangu alinipenda sana. Mnooo. Mpaka sasa ninahisi pendo lake kwangu, japo inaelekea miaka ishirini sasa tangu alipofariki.
Wengi niliokutana nao baada yake ni watu wanaoumiza kuliko kuponya (siwasemi vibaya). Hii imenifanya niwe na watu wachache sana katika circle yangu. Katika hao wachache, niliojaribu kuwaweka karibu zaidi nao waliishia kunidisappoint kwa namna 1 au nyingine au hawakuwa permanent (walikuwa ni wa kupita tu). Yaani kwa kifupi sina mtu ninayemwamini kumshirikisha mambo yangu personal asiyatoe kwa wengine, au asisaliti mpango husika. Hali hii imeniweka katika ulimwengu wangu peke yangu, japo ukiniona na hata kuzungumza nami ni vigumu kugundua hilo. Changamoto ni kwamba, sitamani haya maisha, lakini ndiyo ninyoishi sasa. Shida ni kuwa nishachoka. Ninatamani kuwa na marafiki wakweli, hata mmoja tu, lakini hadi sasa hata huyo mmoja sina. Wakati mwingine ninajiuliza au tatizo ni mimi? But mbona mie ni mtu mwema tu? (Sijisifii)
Kuhusu mzee yupo, na huwa simlaumu kwa lolote, instead ninawasiliana naye, na ninamuheshimu kama baba yangu mzazi. Japo sijui kama anaelewaga, kuwa alichofanya sicho alichopaswa kufanya kama mzazi.