UPWEKE: Ni lini nitapata rafiki mwingine wa kweli?

Pole sana mkuu ila hii ndio dunia ichukulie kama ilivyo ili maisha yaendelee

Nyuzi kama hzi unaweza kuishia kwenye typing hua zinaumiza sana hisia.
Dah, mkuu niliahirisha kutype mara kadhaa kufuta machozi kwanza. Nimetype nikilia asee.
 
Tafuta mke uoe kama utabahatika kupata mke mwema utakuwa umepata suluhisho la upweke ulionao kama hatakuwa mwema sana ila akakuzalia watoto hao wananao watakuwa faraja kwako.
 
Itabidi mkuu. Ahsante sana kwa ushauri
 
Ninakuja kwenu Wakuu kwa unyenyekevu, kwa namna ambavyo nimeona watu wanasaidika kimawazo kupitia jukwaa hili la JF. Ninawasalimu nyote. Naomba nilete kwenu changamoto ambayo nimekuwa nayo muda mrefu sasa.

Mimi ni kijana mwenye umri chini ya miaka 30. Mama yangu alifariki nikiwa na miezi mitatu. Baba alikimbia majukumu baada ya kumzika mama. Bibi na babu wakanilea, na kunianzisha shule, hadi walipofariki nikiwa bado shule ya msingi. Nimepitia changamoto nyingi za kimaisha tangu walipofariki walezi wangu hawa, ikiwemo kuishi kwa ndugu tofautitofauti (kutokuwa na makazi maalumu), huku nikiendelea na masomo.

Ninamshukuru sana Mungu kwa ajili ya wote waliojitoa kwa namna yeyote ile kunisupport kimaisha na kielimu. Pia, ninaishukuru sana serikali yetu (Awamu ya Nne) kwa sera nzuri zilizosaidia na mimi kupata mkopo wa elimu ya juu. Mungu wa mbinguni awabariki.

Mungu alinisaidia, nikamaliza degree yangu salama, na sasa niko kazini. Katika kipindi chote hicho nimekutana na watu wa aina zote. Nilipata marafiki, wakike na wakiume. Wengine niko nao bado, wengine walikuwa ni wa muda mfupi. Kuhusu mahusiano sijawahi kuwa kwenye relationship, japo nishawahi kupenda.

Kama kichwa cha thread kilivyo, niko mpweke. Siyo kwamba sijichanganyi, ninajichanganya, lakini deep inside Ni mpweke. Dhoruba nyingi nimepitia. Mtu pekee (Rafiki) aliyekuwa karibu nami tukapendana genuinely na nikafurahia maisha ni bibi yangu aliyenilea (Mungu am'bariki huko aliko). Bibi yangu alinipenda sana. Mnooo. Mpaka sasa ninahisi pendo lake kwangu, japo inaelekea miaka ishirini sasa tangu alipofariki.

Wengi niliokutana nao baada yake ni watu wanaoumiza kuliko kuponya (siwasemi vibaya). Hii imenifanya niwe na watu wachache sana katika circle yangu. Katika hao wachache, niliojaribu kuwaweka karibu zaidi nao waliishia kunidisappoint kwa namna 1 au nyingine au hawakuwa permanent (walikuwa ni wa kupita tu). Yaani kwa kifupi sina mtu ninayemwamini kumshirikisha mambo yangu personal asiyatoe kwa wengine, au asisaliti mpango husika. Hali hii imeniweka katika ulimwengu wangu peke yangu, japo ukiniona na hata kuzungumza nami ni vigumu kugundua hilo. Changamoto ni kwamba, sitamani haya maisha, lakini ndiyo ninyoishi sasa. Shida ni kuwa nishachoka. Ninatamani kuwa na marafiki wakweli, hata mmoja tu, lakini hadi sasa hata huyo mmoja sina. Wakati mwingine ninajiuliza au tatizo ni mimi? But mbona mie ni mtu mwema tu? (Sijisifii)

Kuhusu mzee yupo, na huwa simlaumu kwa lolote, instead ninawasiliana naye, na ninamuheshimu kama baba yangu mzazi. Japo sijui kama anaelewaga, kuwa alichofanya sicho alichopaswa kufanya kama mzazi.
Tumelelewa na wazazi lakini ikiwa wamekufa mzazi anayefuata huwa ni mke au mme for ke.
Oa muombe MUNGU mwambie nahitaji mke awe ni mama yangu kweli yaani mama yangu ajifunue kupitia yeye. Usihuzunike kuwa karibu kanisani pitia mafundisho kadhaa ya ki roho katu utabadilika.

Usijione ni nothing wala usiwe mtu wa hasira. Tatizo ni kwamba ulishaathirika kisaikolojia unahitaji cancelling.
 
pole sana chief,
ila hapa mimi naona tatizo ni wewe.

kwa miaka yote hiyo tangu unaanza shule hadi umefika kazini sitaki kuamini haujaona watu hata 5 tu ambao unahisi mnaweza kuvumiliana kwa baadhi ya tabia,

kitu ambacho nimekiona kwako ni uoga wa kuumia au kuwa disappointed....

wanasema hauwezi kujua raha/thamani/utamu wa mkate mzuri bila kuonja mkate mbaya.

jiachie, jichanganye na watu, kuwa open, kuwa na vigezo vyako vichache then let things flow naturaly....haya maisha hawezi kupata kile unachokitaka kwa 100%, tunatakiwa kujifunza kiCop kulingana na mazingira wakati mwingine.

kama wewe unajiona ni rafiki mzuri na mwema basi amini pia wapo wengine wazuri na wema...waruhusu tu.
 
Ushauri kuntu!
 
Hapana weka wazi hapa..hao wachache ni Mademu???? Inamaana hata marafiki wakiume bado walikua wakupita, vipi jamaa wako yule wachuon??au kazin inamaana hauna marafiki km hao?? .

Hapa naona umeshindwa Sema "Natafuta mwanamke mkweli wakunipenda nimpende"....

Umeamua kutumia indirect way ya kutafuta mwanamke kwanjia ya huruma ..ila sina mashaka hata hao wachache walokuwepo wamekupa Hints za kujua nani ni mwanamke sahihi .

Akili yangu imekataaa katakata kuamin kua hauna Rafiki hata mmoja yaaan hata mshikaji wako???
 
Aisee kweli binadamu tuko tofauti, for me ni rahisi sana kupata marafiki wema (good friends). ila ni vigumu sana kupata mke wa kuoa, yani imekuwa ngumu sana kupata demu ambae naweza sema huyu atakuwa mke wangu, though nshawahi kuwa kwenye romantic relationships huko miaka iliopita julyhero
 
Mkuu nitafute inbox. Ila kukushauri kwa ujumla ni kuwa ndawa ya kuishi maisha ya furaha unayo wewe mwenyewe. Our injuries inside us heal believe that.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa upande mmoja huo upweke ni mzuri kwa maana ukitaka ku fill hiyo emptiness kwa kutaka kuonyeshwa upendo utaishia kuwa disappointed (kama mwenyews ulivyokiri kuwa disappointed).

Nashauri utafute kitu cha kufanya unachokipenda kitakacho kuondolea upweke. Katika maisha haya usitegemee kuipata furaha ya kweli kutoka kwa mwanadamu mwenzio.. Furaha yako unayo mwenyewe. Itafute
Chalii umenena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumelelewa na wazazi lakini ikiwa wamekufa mzazi anayefuata huwa ni mke au mme for ke.
Oa muombe MUNGU mwambie nahitaji mke awe ni mama yangu kweli yaani mama yangu ajifunue kupitia yeye. Usihuzunike kuwa karibu kanisani pitia mafundisho kadhaa ya ki roho katu utabadilika.

Usijione ni nothing wala usiwe mtu wa hasira. Tatizo ni kwamba ulishaathirika kisaikolojia unahitaji cancelling.
Ahsante sana kwa ushauri. Nitaufanyia kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana chief,
ila hapa mimi naona tatizo ni wewe.

kwa miaka yote hiyo tangu unaanza shule hadi umefika kazini sitaki kuamini haujaona watu hata 5 tu ambao unahisi mnaweza kuvumiliana kwa baadhi ya tabia,

kitu ambacho nimekiona kwako ni uoga wa kuumia au kuwa disappointed....

wanasema hauwezi kujua raha/thamani/utamu wa mkate mzuri bila kuonja mkate mbaya.

jiachie, jichanganye na watu, kuwa open, kuwa na vigezo vyako vichache then let things flow naturaly....haya maisha hawezi kupata kile unachokitaka kwa 100%, tunatakiwa kujifunza kiCop kulingana na mazingira wakati mwingine.

kama wewe unajiona ni rafiki mzuri na mwema basi amini pia wapo wengine wazuri na wema...waruhusu tu.
Nashukuru sana mkuu kwa mawazo yako. Ninazidi kujifunza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana weka wazi hapa..hao wachache ni Mademu???? Inamaana hata marafiki wakiume bado walikua wakupita, vipi jamaa wako yule wachuon??au kazin inamaana hauna marafiki km hao?? .

Hapa naona umeshindwa Sema "Natafuta mwanamke mkweli wakunipenda nimpende"....

Umeamua kutumia indirect way ya kutafuta mwanamke kwanjia ya huruma ..ila sina mashaka hata hao wachache walokuwepo wamekupa Hints za kujua nani ni mwanamke sahihi .

Akili yangu imekataaa katakata kuamin kua hauna Rafiki hata mmoja yaaan hata mshikaji wako???
Mkuu nimekuelewa, ninayemzungumzia ni mtu wa karibu, awe wa kiume au wa kike sijali, ili mradi awe ni rafiki wa kweli.

Kuhusu konewa huruma mkuu, ninajua hakutonipa mwenzi sahihi, je huruma zikiisha? Sina nia ya kuonewa huruma. Michango ya mawazo tu itanitosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom