UPO JF kwa MWAKA MZIMA , UMECHANGIA NINI ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,230
2,000
kila unachokipanga bila shaka kuna ulicholenga , malengo yako ya kuwemo jf tena kwenye JUKWAA LA SIASA ( tukumbuke kwamba SIASA NI MAISHA ) UMEYATIMIZA ?najua kuna walioanguka na wengine wamesimama , lakini wewe je ? Jukwaa hili ni dira ya nchi , ndiyo bakora kwa WANASIASA UCHWARA ! NI KAMA SHULE VILE ! UMELITUMIA IPASAVYO ? tujitazame upya , HAPPY NEW YEAR !
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,503
2,000
Naamini nimechangai mengi, ubora au udhaifu wa michango hiyo ni nyie wa kunihukumu!!! Nimejitahidi sana kuchangia na kurudisha mjadala kwenye hoja hasa wale ndugu zangu pale walipojaribu kukwepesha maana nzima ya MADA lengwa. nashauri next year kama thread ikianzishwa tuchangie thread peke yake sio kuleta vitu ambavyo viko nje ya mada
 

Deshmo

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
4,774
2,000
Jf ni kama darasa kwangu,limewafunza wengi pia,wanasiasa uchwara pia wamejifunza na zaidi ya kujifunza wanaiogopa sana hadi kuizungumzia bungeni
 

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,148
2,000
Mkuu Jf imekuwa zaidi ya reference kwa kila kitu...si kwa wanasiasa tu bali kwa kila nyanja na kwa kuwa siasa ni kiungo kati cha maendeleo ya taifa lolote imechukua uwanja mpana zaidi!

Mwaka 2013 ni mwaka uliokumbwa na mambo mengi sana kisiasa huku alert nyingi pia zikiibuliwa na wanawema wa JF waliolitakia mema taifa letu....

Ni imani yangu pia viongozi wa kada mbali mbali walitumia muda wao wa kazi kuperuzi mawili matatu kwenye majukwaa yaliogusa moja kwa moja majukumu yao kikazi na kupitia peruzi hizo wameweza kujua sura yao/nafasi yao kijamii ivivyo hivyo kubadili mienendo yao ambayo ililalamikiwa na kuimarisha pale walipoambiwa wamejitahidi...

Mwaka 2013 ni mwaka uliogubikwa na matukio mengi pia ya wanandoa/wapenzi kutokuwa na uaminifu kwenye mahusiano yao hali iliyopelekea wale waliokosa ustahimilivu kuinuka juu ya wenza wao na kusababisha maafa yalioacha funzo kwa wengine kutopitia njia walizopita wenzao....

Yatosha tu kusema JF ni zaidi ya mtandao wa kijamii,na Mwenyezi Mungu awajaalie uzima na heri bwana Maxcence Melo na ndugu Mike Mushi as founder wa hiki kisima cha mawazo,na chem chem ya fikra ili waendeleze ambayo 2013 hawakuyapa kipaumbele!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom