Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

Unafurahi kuzaliwa na kuishi Tanzania?

Umewahi kusikia watu wakisema hawapendi nchi walizozaliwa?

Leo katika kipindi cha Amka na BBC kuna taarifa nimesikia kuhusu wahamiaji kutoka nchi za Nicaragua na Honduras

Wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wanafunga safari wakipitia nchi ya Mexico na kujaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kwa madai ya kutafuta maisha bora

Hata kwetu kuna watu wamekuwa wakiondoka na kwenda nchi nyingine
Watanzania wengi wapo Afrika Kusini mpaka tumeona miezi ya nyuma walivyofurushwa na kurudi nyumbani tena kwa msaada wa serikali wengine wakiwa na muonekano wa kutia shaka

Watanzania wengi pia wapo Ulaya kujitafutia kipato
Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini wenyewe wanadai nyumbani Tanzania pamekuwa pachungu sana na hawavutiwi tena licha ya kua wana pakumbuka

Nina rafiki yangu yupo USA anasema anatamani kurudi bongo hasa mitaa aliyokulia ila havutiwi tena

Nimegundua
Nchi nyingi ambazo wananchi wake wanazikimbia zina mazingira magumu ya kuishi

Nitaongelea hapa Tanzania kwetu

Tunaweza kukubaliana kwamba nchi hii ni ngumu na haivutii kuishi, labda uwe na kiwango fulani cha maisha la sivyo ni shida sana

Umewahi kwenda kwenye hospitali za umma? Msongamano mazingira yasiyo rafikiI mean uchafu umeshuhudia?

Usafiri wa umma daladala alooo!

Watu wanajazwa kuliko hata uwezo wa daladala
Humo ndani ni kukanyagana

Mtu anaenda kazini alfajiri kuwahi foleni anarudi anadandia gari kama vile nyani wanavyodandia miti unapanda daladala unaogopa kugusa hata lile bomba mana lina majasho ya kila namna

Msongamano harufu za kila aina zisizovutia unaweza kupata depression

Masoko jamani! Masokoni ukienda huko kipindi cha mvua uvae gumboots, la sivyo unarudi kama umetoka kulima mpunga
Umewahi kwenda Soko la Mabibo kipindi cha mvua?

Machinga wamezagaa ma barabarani watembea kwa miguu unapishana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa

Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi

Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?

Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?

ShesRise_1 ✋️
Hakuna nchi nzuri kama Tanzania kwa fursa, amani na utulivu, ni issue ya kuwa na right mindset.

Nenda Ulaya/ Marekani/ SA kama una elimu au fani inayohitajika na kafanye kazi kwa makaratasi sahihi. Lakini unakwenda ughaibuni kwa kuzamia na huna elimu, wewe maisha yako yataishia kuzoa mavi na makohozi ya wazee kwenye nursing houses.
 
Hakuna nchi nzuri kama Tanzania kwa fursa, amani na utulivu, ni issue ya kuwa na right mindset.
Au sio huihui
Nenda Ulaya/ Marekani/ SA kama una elimu au fani inayohitajika na kafanye kazi kwa makaratasi sahihi. Lakini unakwenda ughaibuni kwa kuzamia na huna elimu, wewe maisha yako yataishia kuzoa mavi na makohozi ta wazee kwenye nursing houses.

Kwani kwa hapa Tanzania kama huna elimu unaweza kufanya kazi kwa makaratasi?
Labda uwe CCM 🤣🤣
Siku hizi kuna bodaboda wenye degree we huoni tatizo hapo?
 
ZirlovimovicZirkov masuala unayoandika na uhalisia ni vitu viwili tofauti na hata wewe unajua kuhusu hilo

Mimi kusema Bongo bahati mbaya haina maana kwamba siipendi Tanzania

Naipenda chi yangu hapa ndipo kitovu changu kilipozikwa
Lakini wakati mwingine nahisi ardhi yenyewe ya Tanzania hainipendi
Au labda mazingira ndiyo hayanipendi 😄
Majibu Yako hayajaniridhisha Bado.

Niambie ni mambo mangapi nyumbani kwenu hayapo sawa??? Je! Uliona solution ni kukimbia kwenu??? Kuhama ukoo??? Au kujiita jina la kitajiri???

Ukinijibu hapa angalau nitakuelewa.

Kuhusu suala la usafi haimaanishi kwamba mimi niliyeandika ni mchafu au mafurahia uchafu
Lakini tusipindishe hoja suala la ustaarabu kwenye masoko bado ni changamoto
Kuna uhitaji wa usimamizi kutoka kwa mamlaka zinazohusika kwa sababu watu binafsi wanaonekana kulichukulia suala la usafi kama jambo lisilo na umuhimu

Hili la kusema tugomee kwenda kwenye masoko machafu we uliona wapiiii 🤣utagoma wewe peke yako trust me
Watu wameyazoea mazingira hayo na wengine hawajali kabisa
Mamlaka zinazohusika ndizo zinazopaswa kusimamia lakini hazijihusishi ipasavyo
Labda hata wao wenyewe wamezoea hali hiyo

Kipindi cha Rais Magufuli kulikuwa na nafuu kwenye suala la usafi
Na hapo ndipo unapaswa kuelewa kwamba ili usafi uwepo, hasa kwenye masoko wakati mwingine watu wanahitaji kushurutishwa na kusimamiwa
Mimi Huwa siendi kwenye masoko machafu, alafu pia Huwa nawashawishi na watu wengine wasiende hiyo sehemu. Nakushauri tumia kalamu kufanya hivyo.

Naamini ujumbe wako utafika.
 
Wanapenda wepesi, wanataka amani na maisha Bora aliyotengeneza nani???
Kila mtu anapenda wepesi unadhani maviongozi yenu yasingependa wepesi mbona nchi ingekua mbali sana hii, jidanganye tu utakufa waje watoto wako, vitukuu hata vilembwe bado watalikuta hili li nchi lako liko hivyo hivyo sioni likiendelea kutoka hapo. Acha watu waondoke wakapambanie familia zao hio nchi bila kua kwenye circlr ya ma ccm, jijue utakufa maskini na watoto watarithi kuendesha boda boda.
 
Back
Top Bottom