Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
23,057
Reaction score
52,754
Unafurahi kuzaliwa na kuishi Tanzania?

Umewahi kusikia watu wakisema hawapendi nchi walizozaliwa?

Leo katika kipindi cha Amka na BBC kuna taarifa nimesikia kuhusu wahamiaji kutoka nchi za Nicaragua na Honduras

Wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wanafunga safari wakipitia nchi ya Mexico na kujaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kwa madai ya kutafuta maisha bora

Hata kwetu kuna watu wamekuwa wakiondoka na kwenda nchi nyingine
Watanzania wengi wapo Afrika Kusini mpaka tumeona miezi ya nyuma walivyofurushwa na kurudi nyumbani tena kwa msaada wa serikali wengine wakiwa na muonekano wa kutia shaka

Watanzania wengi pia wapo Ulaya kujitafutia kipato
Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini wenyewe wanadai nyumbani Tanzania pamekuwa pachungu sana na hawavutiwi tena licha ya kua wana pakumbuka

Nina rafiki yangu yupo USA anasema anatamani kurudi bongo hasa mitaa aliyokulia ila havutiwi tena

Nimegundua
Nchi nyingi ambazo wananchi wake wanazikimbia zina mazingira magumu ya kuishi

Nitaongelea hapa Tanzania kwetu

Tunaweza kukubaliana kwamba nchi hii ni ngumu na haivutii kuishi, labda uwe na kiwango fulani cha maisha la sivyo ni shida sana

Umewahi kwenda kwenye hospitali za umma? Msongamano mazingira yasiyo rafikiI mean uchafu umeshuhudia?

Usafiri wa umma daladala alooo!

Watu wanajazwa kuliko hata uwezo wa daladala
Humo ndani ni kukanyagana

Mtu anaenda kazini alfajiri kuwahi foleni anarudi anadandia gari kama vile nyani wanavyodandia miti unapanda daladala unaogopa kugusa hata lile bomba mana lina majasho ya kila namna

Msongamano harufu za kila aina zisizovutia unaweza kupata depression

Masoko jamani! Masokoni ukienda huko kipindi cha mvua uvae gumboots, la sivyo unarudi kama umetoka kulima mpunga
Umewahi kwenda Soko la Mabibo kipindi cha mvua?

Machinga wamezagaa ma barabarani watembea kwa miguu unapishana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa

Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi

Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?

Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?

ShesRise_1 ✋️
 
Machinga wamezagaa mabarabarani member kwa miguu anaposhana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa

Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi

Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?

Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?

ShesRise_1 ✋️
Mimi binafsi nikiwa na pesa Tanzania itakuwa sehemu mzuri sana ya kuishi,,lakini hivi kapuku ni hovyo sana. Tanzania mtu mwenye pesa naamini anaenjoy sana maisha kuliko mwenye pesa wa kiwango sawa wa ulaya,,huku huduma za jamii duni sana,kama ulivosema,, wanao enjoy maisha ya Tanzania ni waliojipata tu,, mafisadi na watoto wao, wafanyabiashara wakubwa,na watu wa tabaka la kati wenye kipato cha uhakika daily..NB ukiwa na pesa Tanzania utaishi kama mfalme.
 
Back
Top Bottom