Upinzani waonesha wizi wa Tsh Trilioni 2.4 toka ripoti ya CAG na ulaghai wa kamati ya PAC iliyopangwa na Ndugai kuficha ukweli

Mimi sijaelewa lolote zaidi ya overdraft!!!

Nawaonea huruma watanzania ambao hawajui kwamba idadi ya majambazi ni kubwa kuliko wale tunawajua.

Hawa majambazi wengine wanaua majambazi wenzao wabaki peke yao na sisi watatuua kwa ugumu wa maisha.


Deal done.

Mkuu hata hii summary huelwi ?

Mchanganuo wake ni kama ifuatavyo:
• TZS 290.67 bilioni ambayo ni Overdraft yenye utata.
• TZS 976.96 bilioni iliyotumika Ikulu (Reallocation) bila kupitishwa na Bunge, bila idhini ya CAG na haikukaguliwa matumizi yake.
• TZS 656.6 bilioni ambayo ilikuwatofauti (Mis-match) kati ya Fedha zilizoidhnishwa kutoka akaunti ya mapato (exchequer issue warrants) na ripoti ya fedha iliyotolewa ( exchequer release report )
• TZS 3.45 bilioni ambayo ilikuwa exchequer issues warrant ambayo ilifutwa bila sababu za msingi
• TZS 3.3 bilioni ambayo exchequer issue warrant ambayo haikuwa na vielelezo
• TZS 234.12 bilioni ni fedha ambazo hazikuingizwa kwenye exchequer account na hakukuwa na vielelezo
• TZS 189.99 bilioni hizi zilitumiwa na Katibu Mkuu Hazina bila kupata kibali cha CAG na kinyume na sharia ya Fedha


Jumla ya hoja zote hizo ni Shilingi 2.4 trilioni
 
Hii kitu tungeitengenezea movie tungeuza sana! steling awe prof Asad na adui ni jiwe 😂😂
 
Huyu Binti ndio maana KAFIWA Na MUMEWE LEO. Hizi findings zote anazoongelea ni kabla ya UHAKIKI kukamilika. Kwa anayejua AUDIT PROCESS , hizo Hoja za Ukaguzi zilizotolewa na baadaye Serikali imetoa MAJIBU ambayo ndio yaliingia kwenye PAC na kisha kuletwa Bungeni. Kamama kana mdomo mrefu na kapotoshaji kakubwa.
 
Hili si sishaisha jaman CAG mwenyew na report imesomwa mmeambiwa hamna upotevu wa pesa yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninadhani hukulewa swali aliloulizwa CAG "Kuna pesa yoyote imeibiwa?" akajibu "Hapana". Kama mbunge alivosema kwenye uzi, CAG hakusema pesa zimeibiwa. Katika ripoti yake ameonesha kiasi cha pesa ambazo matumizi yake hayajathibitishwa. Ni bahati mbaya sana swala limehamia kwenye "wizi". Wanaojitetea wanasema "hawajaiba" badala tu ya kuonesha fedha hizo zilivotumika na tukatoka katika mkwamo huu. Mkuu, elewa hapa swala sio wizi/kupotea fedha - ni kuthibitisha matumizi yake. Period.
 
2..Bilioni 976.96 Zimetumika Ikulu Bila kupitishwa na Bunge na Kuidhinishwa na CAG Baada ya Serikali kushindwa kuonyesha zilivyotumika Shilingi 1.5 Trilioni iliamua kujilinda kwa kuitumia Ikulu kwa kuwa inajua CAG hatakagua Ikulu. Hivyo CAG alielezwa kuwa shilingi 976.96 bilioni zilihamishwa kutoka kwenye mafungu mbalimbali ya Kibajeti ya Serikali (Reallocation) na kupelekwa Fungu namba 20 (Ikulu). Bunge halikupitisha shilingi 976.96 zitumike na Ikulu, na hata hiyo huo uhamishaji (Reallocation) haukuidhinishwa na CAG kama Sheria inavyotaka, na hata baada ya kutumia bado Serikali haikumpa CAG vielelezo wala uthibitisho wowote wa matumizi hayo. Serikali imeshindwa kuthibitisha imetumiaje Shilingi 1.5 Trilioni, Maelezo kuwa zimetumika na Ofisi ya Rais Ikulu yametolewa kwa makusudi kwa sababu Serikali inajua kuwa CAG hakagui Ofisi ya Rais Ikulu, hivyo ni kichaka cha matumizi mabaya ya fedha za Umma. Jambo baya zaidi ni kuwa Kamati ya Bunge ya PAC ililikalia kimya jambo hili kwenye ripoti yake iliyoletwa bungeni.

Endeleeni kumuamini Raisi Mzalendo na Raisi wa Wanyonge

Mkuu, umetendea haki dhamira yako!! Swala ni kuthibitisha matumizi. CAG ana wajibu wa kufuatilia hizo reallocations. Sasa zikipelekwa au kiukweli au kinadharia sehemu ambayo hataweza kuzifuatilia - maana yake zitabaki katika "querries"!!
 
Huyu Binti ndio maana KAFIWA Na MUMEWE LEO. Hizi findings zote anazoongelea ni kabla ya UHAKIKI kukamilika. Kwa anayejua AUDIT PROCESS , hizo Hoja za Ukaguzi zilizotolewa na baadaye Serikali imetoa MAJIBU ambayo ndio yaliingia kwenye PAC na kisha kuletwa Bungeni. Kamama kana mdomo mrefu na kapotoshaji kakubwa.
Duuu!!! Mambo ya kufiwa yanatoka wapi sasa hapa jamani. Huwezi kumjibu mtutu bila kutukana? Dada katowa Data hapa njoo na Data utueleweshe sisi wananchi wa kawaida ambao hatuwezi kupata hizo documentsd. Kwakweli silazima utokwe povu kiasi hiki unless otherwise. Anyway ushauri wangu tu
 
Duuu!!! Mambo ya kufiwa yanatoka wapi sasa hapa jamani. Huwezi kumjibu mtutu bila kutukana? Dada katowa Data hapa njoo na Data utueleweshe sisi wananchi wa kawaida ambao hatuwezi kupata hizo documentsd. Kwakweli silazima utokwe povu kiasi hiki unless otherwise. Anyway ushauri wangu tu
Anashangilia mtu kufiwa badala ya kuchambua hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Binti ndio maana KAFIWA Na MUMEWE LEO. Hizi findings zote anazoongelea ni kabla ya UHAKIKI kukamilika. Kwa anayejua AUDIT PROCESS , hizo Hoja za Ukaguzi zilizotolewa na baadaye Serikali imetoa MAJIBU ambayo ndio yaliingia kwenye PAC na kisha kuletwa Bungeni. Kamama kana mdomo mrefu na kapotoshaji kakubwa.

Kufurahia kifo kwa binadamu mwenzio ni ugonjwa wa Akili.
Tumezaliwa, kifo hakikwepeki,
suala la muda kufika,
Akili Timamu haiwezi kushabikia Kifo.

Hoja zimetolewa, jibu pasipo kushabikia kifo cha Marehemu mume wa Hon MP.

Hon amesema wp, alipata hizo facts, ni kutoka CAG.
Kamati ya PAC, iliamua kuficha hizo facts Mjengoni, facts kutoka kwa CAG.
Hon amelizungumzia hilo pia.
Hon aliwahi kuwa Member wa PAC kabla mabadiliko yaliofanywa karibuni.
Anajua kila kitu..
Alizungumza Mjengoni.



Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]
 
Hakuna pesa iliyoibwa. Ruge anataka sifa kwa kutoweka majibu ya Serikali kwa kila hoja. Ugomvi wake na Mwenyekiti wa PAC Tunaujua. Alitaka yeye ndo awe Mwenyekiti akapigwa chini. Mngoreme Huyu mnafiki kweli.
 
Kwa hoja hizi mama umeitendea haki Taaluma yako. Hoja za msingi zinahitaji majibu ya msingi. Tuache ushabiki na matusi Dada apewe majibu kwa Data kama alivyo Dadavua. Hoja ishawekwa mezani mbele ya hazara na ni issue serious ipatiwe majibu sahihi na wahusika.
Hawa watu Ni hatari kwa ustawi was Tanzania.Wanakula bill kunawa,hadi makombo na vilivyodondoka wanakula bill kusaza Wala kufikiri.
Watanzania tudai Katiba ya Wananchi kabla hatujachelewa zaidi.
 
Kazi ipo!!! Hata haijulikani "watanzania" kipaumbele chetu ni nini!? Tunapiga vita ufisadi ndani ya ufisadi!! Tunasema elimu bure huku tukiwahimiza wazazi kuchanga kwa lazima huku wasanii wakipewa 2b za matembezi yasiyojulikana tija yake!!! Mungu Ibariki Tanzania
 
mnadhani ule ununuzi wa kununua wabunge wa upinzani wakidai wanaunga mkono juhudi na mambo mengine pesa zilitoka wapi
 
Back
Top Bottom