Upinzani wamejipatia sifa ya utoto bungeni

Upinzani wamejipatia sifa ya utoto bungeni

kama hz ndio akili za wana ccm,basi tuna safari ndefu kuifikia tanzania ya maendeleo

Labda kama maendeleo yapo kwa maalim seifu, lakini kama maendeleo yanapatikana kwa kufanya kazi, basi kilichofanywa na wapinzani pale bungeni jana, ule ni utoto uliopitiliza
 
Kwa wale wakristo kuna usemi ulisemwa na Yesu Kristo; Waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wao.
Jiulize alikuwa na maana gani? Kwa wepesi tuu ni kuwa watoto hawana dhambi na hata fikra zao hazijaingiliwa na mawazo ya uovu hivyo ni wasafi kustahili kuuona ufalme wa Mungu.
Kwa jinsi Utawala wa nchi hii ulivyo elemewa na Ufisadi, wizi,rushwa,chuki,mauaji,uongo na mazagazaga mengi machafu ni wazi kuwa Wapinzani ni Watoto wanaostahili kuuona ufalme (utawala) wa nchi hii kwani hayo yote yaliyoelemea mioyo ya viongozi wa ccm wao hawana.
 
Wasirudi bungeni, waende wakakae na wananchi waliowachagua majimboni kwao.
 
Nilifurahi sana jana.....hakika UKAWA mliifanyia haki kura yangu niliyowapa

Hiyo kura yako uliiharibu usijisifie. Wangekuwa wanasimamia wakisemacho wangegoma kabisa kuingia bungeni na kukataa posho. Madamu wanapokea posho hawana jipya ni sawa na watoto kulia lia tu. Hapa kazi tu. Ccm mbele kwa mbele na mzee tingatinga. Watanyooka tu
 
Kwa wale wakristo kuna usemi ulisemwa na Yesu Kristo; Waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wao.
Jiulize alikuwa na maana gani? Kwa wepesi tuu ni kuwa watoto hawana dhambi na hata fikra zao hazijaingiliwa na mawazo ya uovu hivyo ni wasafi kustahili kuuona ufalme wa Mungu.
Kwa jinsi Utawala wa nchi hii ulivyo elemewa na Ufisadi, wizi,rushwa,chuki,mauaji,uongo na mazagazaga mengi machafu ni wazi kuwa Wapinzani ni Watoto wanaostahili kuuona ufalme (utawala) wa nchi hii kwani hayo yote yaliyoelemea mioyo ya viongozi wa ccm wao hawana.
Nina uhakika wewe ni mmoja wa watoto waliotolewa nje.
Kwa hiyo wala hujui maudhui ya utoto wako.

Kwani hukumsikia mzee wa Hapa Kazi Tu alivyosema atawashughulikia?
Ngoma ya kitoto haikeshi.
 
ukawa ni wanawake wanajiiita makamnda kumbe makamanda wa kuzomea kama wanwake wa uswazi dawa ya tatizo ni kutatua tatizo na sio kukimbia tatizo....
 
Ndo wale wale neno lolote litakalomtoka kiongozi wa ccm kwao ni IBADA..... Hopeless kabisaa
 
Labda kama maendeleo yapo kwa maalim seifu, lakini kama maendeleo yanapatikana kwa kufanya kazi, basi kilichofanywa na wapinzani pale bungeni jana, ule ni utoto uliopitiliza

Bora utoto wa kupinga uvunjifu wa katiba na dhuruma.
 
AISE NIMEFURAH SNA JANA UKAWA WAMEITENDEA HAKI KURA ANGU NAAMINI NEXT TIME CCM WATAJIFUNZA HAWATABAKA TNA KATIBA...Nakijaribu nibora ukawa wagome kutoka mbungeni wavuruge kabisa km ni mbwai mbwai tu mpaka dunia ishangae.shezy type ala
 
-Kule kenya wabunge hupigana ngumi bungeni.
-Na kuna mabunge mengine wawakilishi hutoleana Bastola na kutishiana Amani.
NB:Mi naona UKAWA ni wa pole na wastaarabu sana....Na Zitto K ni mwanaharakati Vuguvugu.....Magufuli alikosea sana kuwaita ni UKAWA ni watoto,labda kama Serikali yake itakuwa si ya Demokrasia inayojali Katiba.
 
Mlishauriwa kutumia njia za kistaarabu, njia za kisheria. hata Tundu Lissu kwa vurugu za jana ni mtoto.
Mnaoujua ni utoto, na njia za kitoto, makorokocho!!!


 
Last edited by a moderator:
Gamba mwenyewe Ukawa hawana hoja mbele ya watanzania na Jumuiya za kimataifa kwa 7bu Rais aliyekuwa anazindua bunge hakuwa Rais wa Zanzibar hivo Rais Magufuli hakuwa na kosa Hilo ni Bunge litakalo fanya Kazi kuisimamia serikali atakayounda Magufuli siyo Rais wa Zanzibar. So walichofanya ni UTOTO wachapwe tuuu
 
UKAWA ni kikundi cha wachumia tumbo kilichokusanya raia wajinga wasiojitambua
 
Mtoto ni kiumbe adimu ambacho inabidi kilelewe ili kikue.

Mtoto akiwa na njaa yeye hulia
Mtoto akiwa na usingizi yeye hulia
Mtoto akiumwa yeye hulia tu
Hata akipenda kitu fulani , mtoto hulia.

Mtu mzima inabidi kumwelewa, kumwekea kawalawa ili atulie.
Mtoto vile vile anaweza kwenda haja mbele za watu bila kuwa na aibu au soni.
Na mtoto anaweza kudeka na kulia lia akililia kitu anachokipenda.

Wapinzani wetu wa kisiasa, UKAWA, sasa wamejipatia sifa mahsusi ya utoto bungeni jana.
Na hili ni kwa vile kwenye chama/vyama vyao hawana kiongozi mwenye wadhifa wa ustatesman wa utu uzima.

Makekele na aibu ya kutolewa nje ya bunge kama watoto ni sifa waliyojipatia katika ufunguzi wa bunge la 11.

Mbele ya watanzania na wageni wengi wa kimataifa, na hata marais wetu wastaafu, wamejinyea.
Wamejinyea kisiasa wenyewe wanafikiri wamefanya vema, na harufu bado ingalipo hadi sasa.

Mtoto akiendelea kudeka, suala ni moja tu, kiboko.

Bahati nzuri, hao bado ni watoto na viboko inabidi vitumike kuwarudi, amasivyo wataendelea kujinyea wakifikiri ni utaratibu wa kawaida.

Watu wenye akili, watu wazima waliishawaambia UKAWA, pelekeni suala la ZEC mahakamani, lakini watoto hawajui wala hawaelewi.

Huwez kuona uzuri wa jambo hilo ukiwa CCM bt we are proud of it na ujumbe umefika kote Duniani tumewaaibisha vizuri tu na mahakamani hatwendi
 
UKAWA ni kikundi cha wachumia tumbo kilichokusanya raia wajinga wasiojitambua

mchumia tumbo ni yule anaye lazimisha ushindi ilhali hajashinda,ni yule ambaye anatumia jeshi wengine wasile chakula cha familia ale mwenyewe ni yule ambaye anatumia mgongo wa porojo za amani huku ni mvunja sheria na haki za binadamu
 
Bora utoto wa kupinga uvunjifu wa katiba na dhuruma.

Tatizo lenu katiba mpaka awasomee tundu lissu, kana kwamba nyie hamjui kusoma. Kasome katiba ya zanzibar kuhusu ukomo wa rais, ukisha soma njoo hapa utuambie katiba ya zanzibar inasemaje kuhusu ukomo wa rais.
 
Back
Top Bottom