Upinzani wakishinda urais, CCM watapisha Ikulu?

Hatutaki vita. ikulu siyo lazima, tukipata zaidi ya nusu ya wabunge na kuchukua halmashauri zote ccm hata wakiwa na rais watalazimika kutekeleza ilani na sera za ukawa. kwanza katiba ya Mzee Warioba ni lazima ipitishwe kama ilivyo ndani ya siku 100. huyo rais wa ccm akikaidi mi rahisi kupiga kura ya kutokua na imani naye.

Kwa vyovyote chini ya katiba ya 1977 ukawa hawawezi kuingia ikulu kwa kuwa kura za rais hazihesabiwi bali zinatangazwa na aliyeshindwa hawezi kukata rufaa popote. Kwa hiyo vijana eleweni hivyo na msituletee vita isiyo ya lazima, Ingizeni wabunge na madiwani wengi inatosha kwa mabadiliko.
 
Niliuliza swali kitambo kidogo, lakini kwa hali inavyoendelea sasa, ushindi kwa UKAWA NI DHAHIRI!

Swali linabadi, je CCM kweli wataipisha UKAWA waingie na kuikaili Ikulu ya Magogoni, pamoja na sauti nyingi za hila na matumizi mabaya ya vyombo vya dola?

Jinsi CCM Ilivyo Zaliwa Ndivyo Inaenda Kufa Mwaka Huu.
 
Ilikuwa miaka, miezi na sasa zimebaki siku chache watanzania wafanye maamuzi 'magumu' ambayo "WALA UHURU" hawajawahi kuyafikiria wala kuyaona...!
Pamoja na dalili zote njema kwa UKAWA kuingia IKULU safari hii, wasiwasi wangu bado uko palepale, kwamba hawa jamaa wavaa nguo za kijani, watatupisha kweli?
Nina mashaka mengi.....
 
Ndugu wana jamvi, naomba tuweke hapa mawazo yetu kwani hali niionavyo siyo nzuri kabisa kwani kunaanza kuonyesha vihatarishi vya amani. Naomba tuwe balanced katika kujenga.

Hoja iliyopo ni pale CHADEMA na washirika wake wanaojenga UKAWA wakishinda.. Je, wenzao wa CCM watakuwa tayari kuiachia magogoni? Je, ni hatua gani zifuatwe kuleta amani??A u CCM wakishindwa na kwakuwa walishasema hawawezi kuachia Ikulu kwa upinzani Je, nini tufanye kuleta amani??

Au CCM wameshinda ila kwakuwa wamekuwa wakisema watashinda tu na ikishindikana kwa Bao la Mkono je tufanye nini kuleta amani? Kwa leo hayo ndiyo maswali yangu..

Naamini kalamu zenu ndiyo silaha ya kwanza kuzuia machafuko au kuleta machafuko.

Leteni mnayoyawaza.
 
Ukweli unabaki, Nguvu ya Umma itatumika kama tukijua tumeshinda na hawaondoki
 
Hawana namna wasiondoke mkuu! , kwa kuwa ni mpango wa Aliye juu - Muumba wa Mbingu na nchi
 
Ilikuwa miaka, miezi, wiki na sasa zimebaki siku 2 tu!

LAZIMA CCM MTATUPISHA TU IKULU.....
 
Back
Top Bottom