Kusini pride
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,762
- 4,071
Upinzani wa Ndani CCM, Kinachomponza Samia Ujanajike Wake
Katika siku za hivi karibuni, tumeona kuibuka kwa baadhi ya wanasiasa waliowahi kuwa ndani ya mfumo wa utawala wa awamu ya tano—wakijaribu kuvaa joho la uanaharakati na kuunyooshea kidole utawala wa sasa. Alianza Job Ndugai kwa kauli zenye miguno ya malalamiko. Akafuata Askofu Josephat Gwajima kwa maneno ya kejeli yenye ladha ya chuki ya kisiasa. Sasa ni Humphrey Polepole, akijaribu kuandika upya historia kana kwamba yeye hakuwa sehemu ya kinacholalamikiwa leo.
Lakini historia haijisahau.
Watu hawa si wapya katika siasa za Tanzania. Si wageni wa mfumo wanaoupinga sasa. Wamekuwa sehemu ya mfumo ambao leo wanaunyooshea kidole. Tofauti ni kwamba, wakati mfumo ulipowapa nafasi kubwakubwa, walinyamaza. Walitumia mamlaka yao kufunika maovu, kuhalalisha unyanyasaji, na kuwakemea wale waliothubutu kuhoji.
Serikali ya Magufuli: Hali Halisi Waliyonyamazia
Wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli, Tanzania ilishuhudia ongezeko la matukio ya kukamatwa kwa wanaharakati, wanasiasa wa upinzani, na hata watu wa kawaida waliokuwa na maoni tofauti. Matukio ya kutekwa, kubambikiziwa kesi, kufungwa kiholela, na kuporwa kwa ushindi wa chaguzi yaligeuka kuwa kawaida.
Na bado, Ndugai akiwa Spika wa Bunge, Gwajima akiwa mbunge, na Polepole akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM—hawakusema chochote. Walikuwa mstari wa mbele kuhalalisha, kutetea na hata kushambulia wale waliokemea.
Leo wanarudi kama watetezi wa haki? Kama mashujaa waliochelewa? Hapana. Historia itawahukumu kwa ukimya wao wa wakati ule na unafiki wao wa sasa.
Tatizo ni Mfumo Dume, si Samia
Msingi wa malalamiko yao hauko katika uovu wa serikali, bali katika kuvunjika kwa ndoto ya mfumo dume wanaouhusudu. Hawa walikuwa na mgombea wao, walichokuwa wanasubiri Magufuli amalize hatamu yake. Magufuli alipofariki ghafla, walihamaki. Inasemekana, kulikuwepo na mpango wa kumfanya Samia Suluhu Hassan awe Rais wa mpito tu, kisha taifa liende kwenye uchaguzi mpya ili kurudisha mtu wao.
Hawakuwahi kumkubali Samia. Si kwa sababu ya sera, bali kwa sababu ya jinsia na asili ya uongozi wake. Alipovunja mnyororo wa utegemezi na kuanzisha mwelekeo wake—wakati mwingine kwa makosa yake—ndipo wakageuka na kuanza kupiga kelele kama vile walikuwa wapinzani wa kudumu.
Tuwe Makini: Historia si ya Kuandika Upya
Watanzania hawawezi kusahaulishwa yaliyotendeka. Sauti za sasa za malalamiko haziwezi kufuta ushiriki wa watu hawa katika misingi ile ile wanayoikemea leo. Siasa za Tanzania hazihitaji mashujaa wanafiki—wanaotokea tu pale wanapopoteza fursa au madaraka.
Tunapaswa kupima hoja zao si kwa ukubwa wa sauti, bali kwa ukweli wa historia zao. Je, walikuwa wapi wakati watu wakipotea? Wakati chaguzi zikiibwa na kunajisiwa? Wakati upinzani ukizimwa kwa nguvu za dola? Wakati mikutano ya hadhara imepigwa marufuku, Polepole si alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM?
Wasitufanye wajinga. Ukimya wao wa jana ni ushahidi wa unafiki wao wa leo.
Hitimisho: Tusiingie Mtegoni
Mabadiliko ya kweli huanzia kwenye ukweli na uwazi wa dhamira. Tanzania haitajengwa kwa kurudi nyuma kwenye mitandao ya zamani ya kifisadi na kikatili, bali kwa kuangalia mbele na kujifunza kutoka makosa ya wote—wa jana na wa leo.
Polepole, Gwajima, na Ndugai hawapaswi kuwa sauti ya haki katika taifa walilolinyamazisha kwa muda mrefu. Sauti za kweli ni zile ambazo hazikuwahi kunyamaza hata pale maumivu yalipokuwa makali. Na hizo ndizo sauti tunazopaswa kuzisikiliza sasa.
Wao wakitaka kusikilizwa, waanze kwanza kukiri ushiriki wao na kumkalia kimya Magufuli. Waombe msamaha kwa hilo, kisha ndio waungane na sisi katika mapambano. Kinyume na hivyo ni unafiki na mapambano hayataki unafiki.