Upinzani pamoja na figisu zote wanazofanyiwa unatakiwa kubadilika na kubadili mitazamo na aina ya siasa wanazozifanya kutoka kwenye siasa za kiharakati kua siasa za ukombozi zenye hoja mubadala kwa mustakabali wa nchi na zifike kwa wananchi.
Kuendelea kung'ang'ania kudai vitu ambavyo pengine wananchi walio wengi hawajui maana yake na faida zake ni kupoteza muda.
Hapa upinzani unatakiwa uje na hoja mbadala namna gani watayabadilisha maisha ya watanzania ikiwa ni pamoja na kueleza Sera zenye nguvu na mashiko kwa wananchi:
- Waeleze namna gani wataboresha huduma ya elimu ili ilete tija kwa watanzania wote tofauti na saizi ambapo mtu unasoma huna mbele Wala nyuma pengine hata fani unayosomea haujui faida zake na matumizi yake. Mbona watu waliosoma ulaya ni simple kutoboa kimaisha tofauti na huku kwetu tatizo liko wapi hapa waje na majibu na hoja za kueleweka.
- Waeleze namna gani wataongeza au kuboreaha mazingira ya ajira nchini ili kila mtanzania hata yule ambae hana degree 4 aweze kuajilika kutokana na elimu yake hatimae ajikwamue kimaisha.
- Waeleze namna gani wataboresha huduma za afya na upatikanaji wa vifaa tiba, dawa nk. ili ikiwezekana kila Mtanzania atibiwe kama sio bure basi kwa gharama ya chini sana ambayo ni affordable
- Waeleze namna gani wataboresha shule za kata zilizojengwa na serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na kuzipatia vifaa vya maabara vya kutosha au kuzifanya zifanane na shule kongwe nchini ambazo kipindi cha nyuma ziliaminika ni shule za vipaji maalumu.
- Waeleze namna gani wataboresha sector ya michezo ili iwe mkombozi kwa watu wenye vipaji vya michezo lakini pia namna gani watavutia wawekezaji hata kama ni wazawa ili waweze kuwekeza katika michezo hatimaye kuanzisha accademy za michezo nchini. Ambapo michezo kwa wenzetu imetumika kama njia mbadala wa ajira.
- Waeleze namna gani watawasaidia vijana ambao wako katika harakati za kujenga nyumba namna gani serikal watakayokua wameiunda itawasaidia mabati, au sehemu yote ya upauaji.
Na mengine mengi hata kama yatakuwa sio ya kutekelezeka kwa muda mfupi bali hapa lengo ni kufikisha sera kwa wananchi ili imani iliyopotea irejee sasa .Kwa sababu siasa ni kuuza sera pamoja na purukushani kutoka chama tawala lakini ukiwa mjanja unafanya siasa katika mazingira hayo hayo.
Lakini pia pamoja na kuuza sera huko wasisahau kudai demokrasia na tume huru kwa pamoja mana kufanya hivyo bila demokrasia ni sawa na kulia chakula kwenye mzinga wa nyuki.
Kwa kuongezea wapinzanu kutokana na mazingira ya siasa nchini pia inatakiwa wajifunze kula na kipofu,wanatakiwa waache kuwachukia polisi Tena kabisa inatakiwa wawapende watoe ushirikiano mzuri tu,ikiwezekana kabisa wawape ushirikiano wa kinafiki hata hao ccm.Yote hiyo ni kujitengenezea mazingira mazuri ya kutokubughudhiwa kisiasa.
Inatakiwa pale wanapokua na labuda na mikutano ya kuuza Sera Kama wakipata nafasi hiyo wafanye siasa za kistarabu tu ikiwezekana watoe barua ya mwaliko kwa mkuu wa polisi nchini kuja kusikiliza Sera za kistarabu na kutoa ulinzi.Ili kujitengenezea mazingira ya kutokubughudhiwa tu.
Wawape ushirikiano viongozi wa kiserikali na polisi pia hata Kama niwakinafki hapa lengo ni kutengeneza mazingira mazuri ya kutokubugudhiwa.Kwani Kama watu mnagonga wote bia,kukuchukua,mbuzi na kwenye mahafla flani mko wote watakusumbuaje Tena si mnakua marafiki tu automatically Tena huyo huyo anaweza akakutonya pale atakapokua ameagizwa na watu wasio kutakia mema.
Tena kabisa ikiwezekana waandae hafla ya kuwachangia ujenzi wa nyumba za askari,hata Kama itapatikana ya kutosha nyumba moja sawa tu lengo ni kutake control.
Tumieni fursa vizuri kuelekea uchaguzi mkuu mwakani na 2025 kwani hamjifunzi hata kwa mawazili Hawa wakipewa mic mbele ya mkulu ni full kusifia tu sio kwamba wote wanamkubali lahasha Bali ni katika kula na kipofu.
Pale viongozi wenu wa serikali za mitaa watakapokua wamechaguliwa wapeni ushirikiano wa kutosha waweze kufanya Mambo yanayo konga nyoyo za wananchi katika mitaa bila kuonesha viburi na kupoteza imani.
Tofauti na hapo kwa mazingira ya kisiasa nchini upande wa upinzani saizi ni ngumu kufanya siasa kwa Uhuru na ndivyo hivyo mnazidi kupoteza Imani kwa wananchi.