Wee sema siku hizi hakuna siasa, ni mwendo wa kijeshi jeshi nitakuelewa. Sasa huku unazuia wanasiasa yaani wapinzani wasikutane wakatueleza ajenda na Sera zao, si mikutano ya hadhara wala bunge live, leo hii unasema hawana hoja. Wazisemee wapi? Utaisikilizia wapi? Ni mkuu tu ndio yuko live kila kukicha. Hapa tunashindanisha mabondia wawili, mmoja amefungwa kamba mikono tena kwa nyuma, halafu mwingine anajichezea anavyotaka halafu na wewe kwa akili ya upeo wako unamsifia anayemtwanga yule aliyefungwa mikono, hii ni akili ya kiwango cha changarawe. Fungulia Uhuru wa kujieleza hata kwa wiki moja tu, chops zianze kukata anga ndio utajua kuwa hoja zipo au hakuna.