Upinzani fanyeni mageuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upinzani fanyeni mageuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Sep 6, 2009.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Sep 6, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mojawapo ya matatizo ya kisiasa nchini kwetu ni kufanya vyama vya saisa kama sehemeu ya kupatia ajira ya kudumu au mradi wa ukoo fulani. Kwa mfano, tangu nimeisikia CUF katika nyanja za siasa, mgombea wa urais huko Zanzibar amekuwa ni Maalimu Seif Shariff Hamad ambaye pia ndiye amekuwa Katibu Mikuu wa CUF miaka yote, na mgombea wa urais wa Muungano amekuwa ni Profesa Lipumba miaka yote ambaye pia ni mwenyekiti wa CUP muda wote huo. Kwa upande wa TLP tunamjua Mrema na mbwebwe zake wakati kwenye CHADEMA tunamfahamu sana Freeman Mbowe na Helicopter yake: sina uhakika sawasawa, ila nadahani kuwa Mbowe aligombea Urais mara mbili wakati ambapo pia amekuwa ni mwenyekiti wa CHADEMA muda wote huo.


  Vyama vya upinzani mnatakiwa muondoke usingizini. Siku zote simamisheni mtu ambaye mna uhakika kuwa ataweza kuwaletea ushindi badala ya kuangaliana wenyewe kwa wenyewe. Kama mnafahamu historia sawasawa, mtakumbuka kuwa McKinnon aliachia ngazi kwenye chama cha Labor hapo Uingereza mara tu baada ya kubwagwa na John Major; hiyo ilisababisha Tony Blair kuingia ulingoni akiwa kijana mdogo na kupata ushindi ambao umeiweka Labor madarakani kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Kwa marekani pia mtakumbuka kuwa wakati Al Gore aliposhindwa kwa mbinde mwaka 2000 aliacha mambo ya siasa za uchaguzi ili kuwapisha wengine, na mambo yaliendelea hivyo hadi Obama alipoibuka na kutwaa ushindi kwa tiketi ya Demokrati. Somo kubwa hapo ni kwamba ukisimama kwenye uchaguzi na ukashindwa hata kwa kuonewa kama alivyofanyiwa Al Gore, basi pisha njia waje watu wengine na mawazo yao mapya kwa sababu yale ya kwako yatakuwa yameshapitwa na wakati.

  baada ya somo hilo, sasa nasema hivi: Upinzani Tanzania achaneni na utaratibu wa ukiritimba wa kuwabeba watu waliojaribu miaka yote bila kuwaletea mafanikio kisiasa. Kama mtu aligombea akashindwa basi asipewe nafasi ya kugombea tena ati. Radi haipigi mara mbili.

  Ninafahamu kuwa Rais Nixon alibwagwa na Kenndey mwaka 1960 na baada ya miaka kama minane hivi akaibuka tena na kushinda kiti hicho; lakini sote tunafahamu fika alikoishia. Watu wasifanye siasa za vyama kama profession yao; hiyo ni huduma kwa jamii tu, na kama jamii ikishakutosa basi usitafute mianya ya kung'ang'ania.

  Baada ya Longolongo hizo hapo juu, napneda kusisitiza kuwa mwelekeo wa Tanzania kipindi kijacho kwa sasa hivi unategema zaidi sera na nguvu za upinzani kuliko CCM. Kama Upinzani wakifanya Vizuri, nchi itakwenda pazuri ila kama upinzani utakufa, basi nduipo nchi yetu itakpozidi kudidimia kama mabavyo tumekuwa tunadidimia miaka yote.
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Kichuguu,

  Mwaka 1995 CHADEMA ilimuunga mkono Mrema kwenye urais na mwaka 2000 wakamuunga mkono Lipumba. 2005 ilimsimamisha Mbowe kugombea urais, hivyo si kweli kuwa Mbowe amegombea urais vipindi viwili. Mbowe alichaguliwa mwenyekiti wa chama 2004 baada ya Bob Makani kupumzika, huo muda wote unaoongelea ni upi?
   
 3. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  wapinzani tanzania bado,jamani mmesahau ya Mwalim [baba wa taifa] 'UPINZANI WA KWELI UTATOKA NDANI YA CCM'
   
 4. C

  Choveki JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2009
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Semanya hapo umeseme ukweli upinzani wa Tz ni blah blah tu wote ni Sisiemu hao, ndo maana kila wakipanda chati wanagombana mpaka wanasambaratika!
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Unajua mkuu unanifanya nianzew kufikiria Upya maanake inaonyehsha kama hapa tunacheza Sinema tu na hizi CUF Chadema TLP nasiju madudu gani mengine! haiwezekanai kila tunapokaribuia kufika mahala wanatokea wachawi, haiwezekani! sidhani kama tuna vyama vya Upinzani!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Sep 6, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Asante kwa kunifahamisha hilo. Ndiyo maana nimesema wazi kabisa kuwa sina uhakika sawasawa na hilo la Mbowe, hata hivyo jambo kubwa linalonikera kwa hawa ndugu zetu wa upinzani ni kwamba kwao mtu kuwa mwenyekiti wa chama ndiyo tiketi ya moja kwa moja kwake kugombea uraisi. Ningetegemea mwenyekiti awe na jukumu moja tu la kuimarisha chama na kuhamsisha wanachama ambao wana mvuto kwa wanachi ili wagombee.
   
 7. C

  Choveki JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2009
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mkuu fuatilia kwa makini waanzilishi wa vyama vingi vya upinzani (na cv zao) na hasa hivyo vinavyokuwa na wafuasi wengi. Kwanza utaona kuwa waanzilishi wake karibu wote ukiwakata watavuja damu ya kijani. Pili, wakishaona chama chao kimeanza kuwa na wafuasi wengi na kinaweza itoa ccm kamasi basi wanaanza ugomvi wa kijinga na wanagomaba kwelikweli! halafu wanasambaratika! Tatizo ni kuwa sisi watanzania na uzito wetu wa kufikiri tunashinda kugundua kuwa wote ni wamoja, hakuna cha upinzani wala nini. Nina uhakika wengi walio rank za juu upinzani wapo payroll ya hao watawala.
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kichuguu,

  Watafanyaje Mageuzi huku wanavimiliki vyama na si kuwa ni ushirika wa waumini wa Itikadi?

  Ikiwa Mtei, Hamad na Mrema hawakubali kukachia hatamu za Chama ili vyama vyao viundwe katika mfumo bora na wa kisasa na si wa kijima kama CCM, unategemea ni lini vitafanya mageuzi?
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu, sasa hivi nadhani tunaelekea pazuri, mahala ambapo tunaweza pata solution ya matatizo haya yote..
  Nimefikiria sana swala hili na kusema kweli nashindwa kabisa kuamini kinachotokea kila siku.. Kuna wakati vyama vya Upinzani vilishikamana vikawa pamoja karibu kabisa kufikia Muafaka...wakatokea wachawi wakasambaratika ktk chaguzi ndogo zilizofuata...
  Haya tunakaribia uchaguzi mkuu, vyama vyote vya Upinzani umejenga upinzani mkubwa sana kiasi kwamba siamini ati J.J. Mnyika na Zitto leo ni wapinzani ndani ya chama. Sababu hata siielewi zaidi ya ku wonder if kweli hawa ni viongozi wazuri au wana agenda zao binafsi.

  Kisha mawazo ya mkuu wangu Kichuguu kuhusiana na kiti cha mwenyekiti wa chama kuwa ndiye mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama ni mfumo mbaya sana..ndio maana tumeona uchaguzi TLP, CUF na sasa hivi Chadema umezua utata mkubwa sana ndani ya chama. Kama kweli vyama vya upinzani vinapenda mageuzi basi bila shaka sauti ya Umma iwe mbele ya maamuzi yao. wananchi tutapenda kuona muungano wa vyama hivyo wakimsimamisha mtu mwingine kabisa nje ya kundi la wazee au wababe walioshindwa na JK mwaka 2005. Ushindi kwao hauwezekani, watrudi kugombea Ubunge na mtu mwingine kabisa mwenye sifa na uwezo wa kupambana na JK achaguliwe kuwakilisha vyama vyote.. Mtu huyo awe Dr. Slaa!.

  Mbowe mshikaji, napenda sana kumwona Ikulu (maanake nitauchinja) kwi kwi kwi!... lakini ni lazima niukubali ukweli kwamba anahitajiwa mtu mwingine kabisa kupambana na JK mwaka 2005. Mbowe, Zitto, Lipumba, Mrema na wengine wote wataweza kujitokeza tu ikiwa Upinzani utachukua utawala na hapo ndipo wananchi tunaweza kuwapima hawa viongoizi wakiwa ktk nafasi za utawala. na kama Muungano au mshikamano wao utavunjika basi sii haba kumwona Mbowe, Lipumba, na Mrema wakirudi mwaka 2015 wakati Upinzani wameshachukua nchi mwaka 2010.. Mbowe bado kijana, Zitto bado hata kufika Umri wa kugombea kiti hicho, Lipumba, Mrema na Cheyo hawa hawawezi kushinda hata kwa miaka 20 ijayo ikiwa vyama vyao vitasimama pekee.
  Hivyo kusimama kwao wakitumia neno Demokrasia ktk swala ambalo wanajua kabisa haawezi kujenga ila kubomoa ni upuuzi mtupu..

  Uchaguzi mwaka kesho 2010, Kikwete atapeta vibaya sana kwa sababu tu ya wajinga fulani wanaofikiria wao ndio nguzo ya Upinzani nchini..Mafisadi wamekuwa hatua moja mbele yetu kwa kila siku ya matumaini yetu kiasi kwamba tunapoteza imani...Tunaupoteza muda muhimu sana ktk mapinduzi ya siasa nchini..
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Sep 7, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mkandara na Reverend ,

  Nashukuru kuwa nanyi mmeliona tatizo hilo. Unajua muda mfupi ulioipita nilikuwa kule kijijini kwetu na kukutana na watu waliochoka kabisa utawala wa CCM lakini bado wanajiuliza kuwa wamchague nani kutoka kwenye upinzani kwa sababu wagombea wote wa upinzani walishagombea siku nyingi na kwa sasa hivi wanajulikana kabisa udhaifu wao kuwa hawana tofauti na wale wa CCM kwa kutaka kung'ang'ania madaraka.

  Mzee mmoja aliniambia wazi kwa busara kuwa kama kweli viongozi wa upinzani wangekuwa wanafaa kuchaguliwa, basi kwa muda huu kijijini hapo wangekuwa wamfungua matawi mengi kuonyesha kuwa wakichaguliwa watafanya kazi zao hadi huko vijijini. Badala yake pale kijijini hakuna hata tawi moja la chama cha upinzani ispokuwa lile la CCM ambalo linachukiwa sana na wananchi hao. Hiyo ni dalili ya kutisha kwa watu wa vijijini kuwa wakiwachagua wapinzani basi hawatawaona tena hadi siku wakati wa uchaguzi unaofuata.

  Uenezi wa matawi ya chama huko vijijini ndilo lingekuwa jukumu la kwanza la mwenyekiti wa chama cha upinzani ambaye yuko makini badala ya kufikiria kuwa next time nitasimama tena kugombea uraisi.
   
Loading...