CCM ni hatari kama "Dihdydrogen Monoxide", dihydrogen monoxide ni kemikali hatari ambayo pia hujulikana kama hydric acid, hydrogen oxide, hydroxilic acid.
Kemikali hiyo hutumika kwenye viwanda vya nuclear, huweza kusababisha madhara ya kukuunguza vibaya sana, pia inasaidia kutengeneza kutu kwa haraka sana, lakini kemikali hiyo pia hupatikana majumbani mwetu, hutumika kwa kuzuwia moto, hutumika kwa kutayarisha vyakula na pia kwenye baadhi ya dawa tunazotumia.
Ili kuhakikisha Watanzania hatujiongezei madhara kwa kemikali hii hatari inabidi tuhakikishe na tuwe makini kutoitumia, majumbani mwetu, viwandani mwetu, mashuleni na hata mitaani.
Upinzani Tanzania kila kukicha unakuja na hatari mpya ya CCM kubaki kuwepo madarakani. CCM kuendelea kuwepo madarakani ni kama kukubali kuiwacha dihdrogen monoxide iendelee kuwepo majumbani mwetu na huku madhara yake tunayajuwa.
Ni wakati muafaka sasa tuhakikishe kuwa hatukubali kutumia dihdrogen monoxide (CCM) kuwepo Tanzania hii. Madhara ya kuiwacha ni makubwa sana.
Kabla hatuja chukuwa hatua ya kuwacha kuitumia dihdrogen monoxide aka CCM, kwanza tuielewe vizuri hii kemikali;
Dihdrogen monoxide pia kitaalam hujulikana kama H2O. H2O kwa walioenda shule japo kiduchu si kingine bali ni Maji.
Jee, tupo tayari kuacha kuitumia kemikali hii hatari kama upinzani unavyotaka kutuaminisha?
Ukitaka kujuwa zaidi kuhusu dihdrogen monoxide, pitia hapa: http://geekiez.com/have-you-been-exposed-to-deadly-dihydrogen-monoxide/