Ulikua unakomaa hapa jamvini kwa kila post inayohusu escrow a/c. Tena si wewe tu, kuna team iliibuka hapa ilikua haichangii uzi wowote tofauti na escrow a/c. Sikiliza Faiza, linapokuja suala la kitaifa linalogusa umma hebu tuwe tunajitahidi kuweka kwanza pembeni mahaba ya hivi vyama vyetu. Kwenye hili tulipaswa kuwa wamoja likisha malizika kila mtu atawanyikie upande wake. Tuwe kama national team ambayo ina mkusanyiko wa wachezaji toka vilabu mbalimbali wakipigania taifa lao. Hivi kwa mfano wewe leo hii report ya escrow iwekwe mezani na ionekane ni kweli kulikua na wizi na kabla ulikua unatetea kua sio wizi utajisikiaje?