Mabibi na mabwana na hasa wale wazalendo mapambano kudai haki, uhuru na maendeleo bado yanaendelea.
Alisema J. J. Rawlings (rip):
"Ni lazima ifikie pale ambapo hata kama shweitani atakuwa ndiye mtawala (rais), itakuwa ni lazima afanye kile ambacho Waghana (wananchi) wanataka na wala siyo kile ambacho yeye shweitani na genge lake wanataka."
Ni lazima kupigania kufika huko japo kwa hakika haitakuwa rahisi. Anasema Mandela, "no easy walk to freedom."
CDM mnayo nafasi kubwa zaidi ya kuongoza harakati za kufika huko (ambako ni wazi kila mmoja wetu angekufurahia) kwa:
1. Kuunganisha harakati thabiti za upinzani.
2. Kuendeleza harakati za siasa kwa mujibu wa katiba.
3. Kusimamia maamuzi sahihi ya CHADEMA yenyewe kuwa yanazingatiwa na wanachama wake (nidhamu).
4. Kuwepo mawasiliano ya karibu na mh. Tundu Lissu (makamu mwenyekiti) katika kuratibu na kuongoza chama na harakati hizo.
5. Kujipanga kuhakikisha wizi wa chaguzi hautokei wala kuwa ndiyo njia rasmi ya kupata uongozi nchini katika wakati wowote.
6. Kuhakikisha wasaliti na watuhumiwa wote wa usaliti wanaweka misimamo yao wazi, hadharani na bila kuchelewa.
7. Kuhakikisha wasaliti wote wanaenguliwa na wanaacha kupeperusha bendera na agenda za chama mara moja kuepusha sintofahamu.
8. Kuweka utaratibu wa chama kuendeshwa kifedha na wanachama. Ikihakikishwa gharama za uendeshaji zinadhibitiwa vilivyo na kupunguzwa kwa kadri iwezekanavyo.
9. Kuhakikisha wapenzi wa haki, uhuru na maendeleo wanahamasishwa vilivyo kuhakikisha malengo hayo yanatimia.
10. Kutoshiriki haramu yoyote ya uchaguzi na kweli na iwe hivyo. Walioko kwenye uwakilishi haramu na watoke kule au waache kujitanabaisha kukiwakilisha chama kwa namna yoyote.
Haya ni baadhi ya maoni lakini itoshe kusema kusanyeni mawazo zaidi ya wadau. Palipo na nia pana njia.
Uchaguzi bado, uchaguzi bado narudia tena uchaguzi bado!