Upinzani, Aluta Continua! Ni lazima kupigania kupata haki, uhuru na maendeleo japo haitakuwa rahisi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,951
2,000
Mabibi na mabwana na hasa wale wazalendo mapambano kudai haki, uhuru na maendeleo bado yanaendelea.

Alisema J. J. Rawlings (rip):

"Ni lazima ifikie pale ambapo hata kama shweitani atakuwa ndiye mtawala (rais), itakuwa ni lazima afanye kile ambacho Waghana (wananchi) wanataka na wala siyo kile ambacho yeye shweitani na genge lake wanataka."

Ni lazima kupigania kufika huko japo kwa hakika haitakuwa rahisi. Anasema Mandela, "no easy walk to freedom."

CDM mnayo nafasi kubwa zaidi ya kuongoza harakati za kufika huko (ambako ni wazi kila mmoja wetu angekufurahia) kwa:

1. Kuunganisha harakati thabiti za upinzani.
2. Kuendeleza harakati za siasa kwa mujibu wa katiba.
3. Kusimamia maamuzi sahihi ya CHADEMA yenyewe kuwa yanazingatiwa na wanachama wake (nidhamu).
4. Kuwepo mawasiliano ya karibu na mh. Tundu Lissu (makamu mwenyekiti) katika kuratibu na kuongoza chama na harakati hizo.
5. Kujipanga kuhakikisha wizi wa chaguzi hautokei wala kuwa ndiyo njia rasmi ya kupata uongozi nchini katika wakati wowote.
6. Kuhakikisha wasaliti na watuhumiwa wote wa usaliti wanaweka misimamo yao wazi, hadharani na bila kuchelewa.
7. Kuhakikisha wasaliti wote wanaenguliwa na wanaacha kupeperusha bendera na agenda za chama mara moja kuepusha sintofahamu.
8. Kuweka utaratibu wa chama kuendeshwa kifedha na wanachama. Ikihakikishwa gharama za uendeshaji zinadhibitiwa vilivyo na kupunguzwa kwa kadri iwezekanavyo.
9. Kuhakikisha wapenzi wa haki, uhuru na maendeleo wanahamasishwa vilivyo kuhakikisha malengo hayo yanatimia.
10. Kutoshiriki haramu yoyote ya uchaguzi na kweli na iwe hivyo. Walioko kwenye uwakilishi haramu na watoke kule au waache kujitanabaisha kukiwakilisha chama kwa namna yoyote.

Haya ni baadhi ya maoni lakini itoshe kusema kusanyeni mawazo zaidi ya wadau. Palipo na nia pana njia.

Uchaguzi bado, uchaguzi bado narudia tena uchaguzi bado!
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,951
2,000
. Upinzani wa bongo bwana, mipango miiingi halafu utekelezaji zero yetu ngoja tuone

Mkuu kwani wewe nani ambaye wewe au nyie utekelezaji wenu ni kama wote?

Tumeendesha kampeni wenyewe, tumewatia jamba jamba wenyewe hadi mmekwenda kukwiba uchaguzi.

Waulize kina Jiwe, chiro, mamboleo na magenge yao wakwambie kama hawalali usingizi wa mang'amung'amu na ndoto mbaya mbaya zenye kuambatana na ukelele wa kuitiwa wezi.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,951
2,000
Jambo la msingi ni kupigania kupata katiba mpya !!!.Vinginevyo vilio vya tangu 1995 vitaendelea.

Utaratibu (katiba) unaoweza kutaka kuhalalisha haramu kama hii tunayoiona haufai na haupaswi kupewa nafasi.

Pamoja na yote hatimaye misimamo wa Prof. Lipumba ni kutoshiriki uchaguzi mwingine kama haipo katiba mpya.
 

Rutorial k

JF-Expert Member
Jun 8, 2014
934
1,000
Huu ndio wakati wa kuwa na kadi ya chama cha upinzani (CHADEMA). kwa kile kidogo nikipatacho nitachangia harakati za kuinusulu nchi yangu kutoka katika mikonono iliyojaa damu ,mikono ya kuingamiza demokrasia iliyoanza kushamili.shime viongozi wekeni utaratibu wa kutoa kadi za chama na gharama zake
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,951
2,000
Huu ndio wakati wa kuwa na kadi ya chama cha upinzani (CHADEMA). kwa kile kidogo nikipatacho nitachangia harakati za kuinusulu nchi yangu kutoka katika mikonono iliyojaa damu ,mikono ya kuingamiza demokrasia iliyoanza kushamili.shime viongozi wekeni utaratibu wa kutoa kadi za chama na gharama zake

Uzalendo uliotukuka kama huu ni msiba mkubwa kwa lile genge la watekaji, waporaji na wauaji waliokirimiwa mioyo isiyokuwa na chembe ya ubinadamu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom