SoC02 Upimaji wa taaluma vyuo vikuu vya serikali na ufanisi wake

Stories of Change - 2022 Competition

Lameck Ezekiel

New Member
Sep 14, 2022
4
3
Suala la upimaji wa taaluma vyuo vikuu hasa vile vya serikali,limefikia hatua ambayo linahitaji
serikali kuingilia kati ili kuifanya elimu ya juu kuleta matunda tarajiwa kwa taifa. Niukwel usiopingika kuwa elimu ya Tanzania hususani ile ya vyuo vikuu imekuwa ikionekana kupungua ubora wake kila kukicha.

Hii ni kutokana na kukosekana kwa uhalisia wa ubora wa wahitimu kutoka vyuo vikuu unaosababishwa na utofauti wa upimaji wa taaluma kwenye taasisi hizo. Hii inatokana na ukweli usiopingika kuwa elimu ya Tanzania hususani ile ya vyuo vikuu imekuwa ikionekana kupungua ubora kutokana na utofauti wa upimaji wa taaluma kwenye taasisi hizo.

Tatizo la nchi nyingi kama Tanzanaia ni kwamba, kuna tabia ya kutofanyia mapitio mambo yanayoonekana kuwa mazuri leo bila kuzingatia kama yatakuwa bora vivyo hivyo hata kesho.

Mfumo wa elimu ya vyuo vikuu haujawafanyiwa mabadiliko kwa muda sasa kitu ambacho kimsingi kimeufanya ufikie hatua ya kumilikiwa na wakufunzi na watawala katika vyuo hivyo,hasa vile vya serikali,kiasi cha kuwa na uwezo wa kushikilia hatima ya taaluma za wanafunzi. Suala hili kwa upande mwingine limepelekea matatizo mengine yanayohusisana nalo kama vile kukithiri kwa rushwa hasa ile ya ngono vyuoni.

Swali la msingi ni je, sasa si muda mwafaka wa serikali kupitia tume ya vyuo vikuu (TCU), kuanzisha baraza la mitihani la vyuo vikuu litakolokuwa na muundo sawa naule wa NECTA ili kupima ufaulu wa wanavuo, tofauti na kuacha jukumu hilo kwa wakufunzi binafsi wanaotumia mara nyingi utashi wao wakati wakiwapima wanafunzi? Wazo hili linasukumwa na ukweli kuwa, sasa nchi yetu ina wasomi na watalaamu rukuki waliobobea juu ya mambo mengi yanayofundishwa vyuo vikuu.

Kama hiyo haitoshi, utaratibu wa waangalizi wa njewa mitihani ya vyuo vikuu(external examiners) uboreshwe na kukaziwa, ili kuitimiza ile adhima na madhumuni ya nafasi zao.

Kumekuwa na utetezi kutoka kwa wakufunzi kwamba upimaji wa taaluma wanoufanya kwa wanavyuo ni wa haki kwa sababu na wao wanachunguzwa pia na wakufunzi wenzao nje na chuo husika. Lakini kwa upande mwingine jambo hili halifanyiki katika ufanisi unaosemwa.

Hili linadhihirishwa na ukweli kuwa kumekuwa na baadhi ya wakufunzi ambao bila uoga wanawaambia wanafunzi waziwazi kwamba hawatafaulu,na kweli matokeo yanatoka wamefeli isivyo kawaida. Swali ni je, kwa nini hao waangalizi wamitihani wa nje wasizuie hali hii? na kama wanafanya hivyo, mbona hazionekani hasa hatua wanazochukua juu ya hali hii?

Lakini, sote tutakubaliana kuwa, tabia ya ubinafsi na umimi ni ya asili na imo ndani ya kila mtu. Kwa maana kwamba kila mtu huwa anataka kuonekana bora kuliko wengine. Suala hili huwa linanisukuma kutafakari kuwa, je walimu wa vyuo vikuu ambao wanahusika kupima ufaulu wa wanafunzi kwa masomo wanayowafundisha wanawezaje kutoa ufaulu ambao wao hawakuupata kipindi wao wanasoma hayo masomo?

Hii kidogo ni tofauti na NECTA ambapo unakutahata mwalimu akiwa anatawaliwa na hiyo roho inakuwa ni ngumu kuidhihirisha maana uwanja wake wa kusahihisha unakuwa unaminywa na uwepo wa wasahihishaji wenzake kwenye mtihani huo mmoja.

Ni wakati pia mwafaka wa serikali kufanya mapitio na ukaguzi wa taratibu za rufaa za wanavyuo wasioridhika na matokeo yao. Hii ni kwa sababu utekelezwaji wa taratibu hizo maranyingi umekuwa ni mgumu na unakuta umewekwa kwa namna ambayo mwanafunzi husika (anayekata rufaa)atajikuta akikata tamaa mwenyewe. Kuna msemo wanasheria wanapenda kuusema kwamba ‘’ Mtu hawezi akawa mwamuzi wa kesi yake mwenyewe’’, ambayo pia kwenye suala la rufaa hizi inahusiana. Kwenye rufaa unakuta uamuzi umetoka pengine mtihani wa mkata rufaa usahihishwe upya na wakati anayepewa jukumu hilo unakuta ni mkufunzi anayehusiana tu na yule anayelalamikiwa.

Sambamba na hilo, kuna wakati unakuta mkufunzi amesahihisha mitihani vizuri kabisa lakini tatizo linakuja wakati akituma matokeo hayo mtandaoni ambapo wakati mwingine kunakosekana ufanisitarajiwa kutokana labda na idadi ya wanafunzi ambapo wakufunzi wanakuwa ni wachache au mmoja tu. Kuna makosa amabayo yamekuwa yakibainika wakati wa kutumwa mtandaoni kwa tamuriri(courseworks), ambapo unakuta wanafunzi walio na chanagamoto ya kubadilishiwa matokeo yao wanaitwa na walimu husika ili yarekebishwe.

Swali langu huwa,ni kwa namna gani changamoto hizi za ukusanyaji na upangaji wa matokeo huwa zinatatulika kwenye mitihani ya mwisho wakati ambapo wanafunzi hawana uwezo wa kuiona? Suala hili limepelekea kukosekana kwa uhalisia wa uwezo wa kitaaluma wa wanafunzi kwa maana kwamba kuna wale wanaostahili wanajikuta wamefeli na wale wasiostahili wanajikuta wamefaulu.

Kuna wakati kwa mfano mwanfunzi mwenye tamuririya 37 anajikuta kashindwa kupata alama3 kati ya 60 ili kufikia alama40 kwenye mtihani wa mwisho, na hivyo kujikuta anarudishwa kufanya mitihani ya ziada (supplementary examinations).

Serikali pia iongeze usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara kwa vyuo vikuu. Hii ni kutokana kwamba usimamizi wa serikali kwenye vyuo hivyokwa sasa kupitia tume ya vyuo vikuu Tanzania, bado hautoshi kupelekea upimaji sahihi na wa haki wa maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi vyuoni. Kwa mfano mtu anaweza akajiuliza juu ya gharama amabazo serikali inaingia kugharamia mitihani ya taifa ya darasa la nne wakati mitihani ya vyuo vikuu inayomwandaa mwanafunzi moja kwa moja kutumika kwenye jamii inaachwa chini ya usimamizi wa vyuo ambao unategemea utashi wa wakufunzi wenyewe.

Mwisho,ushrikishwaji wa wanafunzi kwenye masuala yanayowahusu hususani yale ya kitaaluma uboreshwe. Sheria zilizopo zinatoa nafasi hii lakini uhalisia wake ni mdogo sana. Nguvu ya serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu inazidi kufifia kila kukicha kutokana na vitisho vinavyotolewa na viongozi wa vyuo vinavyoungwa mkono na serikali.
 
Back
Top Bottom