Upimaji duni wa malaria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upimaji duni wa malaria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Mar 2, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Maabara ya Kituo cha Afya Kigamboni inatumia vifaa vya kupimia Malaria visivyoaminika.Vifaa hivyo vinadaiwa kutolewa kwa msaada na Marekani.Watu na Watoto wanaopimwa Malaria kwa kutumia vifaa hivyo huonekana hawana malaria,lakini wakienda sehemu nyingine huonekana na malaria.Wakati mwengine mgonjwa huzidiwa kwa kupimwa na vifaa hivyo na kuonekana hawana malaria.Vifaa hivyo vinaonekana vinaweza kutumiwa na zaidi ya mgonjwa mmoja,je ni salama kwa afya?na vifaa vyenyewe vimethibitishwa ubora?Ni vizuri Wizara ya Afya ikafutilia na kuhakiki ubora wa vifaa hivyo.Wana JF mwenye zaidi kuhusu hili aturushie.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu kuamni kama teknolojia ya Marekani inashindwa kugundua vijidudu vya malaria. Inawezekana kuwa watumiaji wa vifaa hivyo wana matatizo katika kuvitumia. Upimaji wa malaria ni kitu rahisi sana, hata teknolojia za miaka ya 1930 ambazo bado tunatumia hapa Tanzania zinaweza kutambua, hili sio tatizo kubwa kwa Tanzania.
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ukishapimwa katika hicho kituo unaenda wapi kwingine?, zahanati za kulipia?. Manake Zahanati na Hospitali nyingi binafsi Tanzania kuna tatizo la mtu kuambiwa ana Malaria wakati hana ili anunue dawa wanazomwandikia. Suala linakuwa ni biashara zaidi kuliko kuwa na Malaria ama ugonjwa mwingine kama Typhoid. Muhimu ni kujaribu katika Maabara zinazopima tu bila kutoa dawa, hawa huwa ni wa kweli. Manake kazi yao wanapima na kukuandikia una Malaria ama la, then majibu unaenda nayo hospitali ili uandikiwe dawa.

  Lingine laweza kuwa ni tatizo letu wagonjwa, kwakuwa tunajua dalili za Malaria, ukijiona hizi ni dalili za Malaria, na ukapimwa ukaambiwa hauna. Basi unaona kuwa wamekosea.

  Mwisho, kwakuwa umeleta hili suala hapa lijadiliwe. Kwanini usiwaandikie Wizara ya Afya. Huenda kweli kuna tatizo la hivyo vifaaa ili kujiridhisha watakapochunguza kweli lipo ama la.
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama vifaa vya Marekani ni bora katika upimaji malaria basi vifaa hivyo vichunguzwe kama havijaisha muda wake na pia ihakikiwe matumizi yake kama vinatumika ipasavyo.
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sehemu niliyoenda na kuonekana na malaria ni Kituo cha Afya Navy Kigamboni.
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi siyo mtaalam wa vifaa hivyo na pia sitazungumzia upimaji wa malaria kny kituo cha afya cha Kigamboni kwa sababu sijawahi kutibiwa hapo na wala sijawahi kufika hapo!

  Nataka tu kuzungumzia uzoefu wangu wa jinsi sehemu (Hospital) nyingi hapa Tz nimekuwa nikienda huko kutibiwa mimi mwenyewe au rafiki zangu na ukiwa una kila dalili ya kuumwa malaria lakini ukipimwa unaambiwa huna wadudu wa malaria lakini ukienda pahala pengine waambiwa unaowadudu wa malaria na ukitumia dawa unapona!

  Hili linaweza kuwa si geni kwa wengi wanaoishi Dar na kutumia hospitali za Aghakhan au Regency ambapo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watu wengi juu ya issue hii (vipimo vyao kutoona malaria). Mimi sielewi inakuwaje hawaoni malaria ila mimi binafsi nilishakutana na issue hii na baadaye nikawa situmii hospitali hizo kwa vipimo vya malaria.

  Wataalam wanaweza kutuambia ni sababu zipi zinaweza kusababisha blood sample yenye malaria ikipimwa isionwe na malaria na baadhi ya vipimo!
   
 7. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Ni kipimo gani hicho?, tafadhali kitaje!, ukweli wa kisayansi ni kuwa:-
  1. GOLD STANDARD test ya malaria ni kwa kutumia darubini kuangalia wadudu ktk damu (Blood slide for malaria parasites- Bs for Mps) na si vinginevyo.
  2. A negative Blood SLIDE (Bs) does not necessarly exclude malaria infection.
  Hivyo mganga anayejua ukweli huu, Bs si kitu pekee cha kumfanya atoe maamuzi ya kutibu malaria.
   
 8. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni ukweli kuwa malaria jijini dar inakuwa over-diagnosed; kila homa malaria! dispensary ndogo ndogo wanapatia biashara hapo kwani wagonjwa wengi wenye homa hawataki kingine zaidi ya kupata confimation kuwa wana malaria.
  na sio malaria tu, hata typhoid; dar hakuna typhoid kihivyo lakini kila mahala ukipita- mtu amekutwa na typhoid na malaria.
  we unadhani kama una malaria kweli kwa nini regency na aga khan wasikuambie hivyo? ao hawataki biashara au?!
  kuna vijidudu kibao vyasababisha homa; eg. for example waweza kupata aina fulani ya virusi ambavyo ni self-limiting (yaani vinapona bila dawa- saana sana labda panadol kutuliza maumivu ama homa), sasa hiyo ukipima malaria utaonekana huna, lakini mtu anaamua kunywa dawa za malaria, akipona sio kwamba zile dawa za malaria ndio zimemponyesha bali ugonjwa wenywe ndivyo ulivyo ni wa siku 3-4 unapona; moja kwa moja hapo siwaamini tena kigamboni!
  na wewe uliyekuja na stori ya kigamboni utakuwa umeongezea ushabiki; ukisema vifaa vinatumiwa na zaidi ya mmoja wamaanisha nini? kila mtu apimwe kwa darubini yake! hheee! itakuwaje?
   
 9. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nilisahau la negative bllod slide; ni kwamba vijidudu vya malaria ama magonjwa mengine haviko "evenly distributed" kwenye damu; ndio kusema tone moja la kutoka mkono huu linaweza kuwa na vijidudu vingi kutoka tone lingine kutoka mahala pengine, au hata usione kabisa vijidudu kutoka tone lingine; hivyo daktari wa kweli akimtibu mtu ha-rely kwenye hiyo bs moja tu; aweza kukuambia urudie hata 3 times kila baada ya muda fulani au atatumia feature zingine kwani zaidi ya vipimo vya maabara madokta wanagundua magonjwa kutokana na historia ya mgonjwa, ama kumpima kwa kumshika ili kuona dalili/signs fulani fulani; lakini ukijitibu mwenyewe au na madokta feki una-rely solely on bs!
  ni hayo tu.
   
 10. M

  Mama JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Hii kali, kwa hiyo malaria parasites wana-form colony patches kwenye damu?!
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Mar 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Labda hiyo mitambo imegharimu $10.00
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Mar 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Siyo kweli hata kidogo. Kwanza Marekani hakuna gonjwa la Malaria kihivyo. Pili, siamini Wamarekani waliopeleka binadamu mwezini eti wasiweze kuwa na teknolojia ya kugundua vijidudu vya Malaria. Nimetembelea maabara za CDC na Emory hapa Atlanta na wana state of the art equipment including hivyo vya kupimia Malaria. Tatu, kwa vile Miafrika Ndivyo Tulivyo, hatuna hata akili ya kutengeneza vifaa hivyo sisi wenyewe na hivyo kutegemea misaada ya kukabiliana na gonjwa hilo kutoka nchi zisizoathirika nalo kama Marekani. Kwetu sisi usemi wa "necessity is the mother of all inventions" hauna maana. Shame on us.
   
 13. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nadhani hili suala lipo, na haya ni masuala ya teknolojia kadiri siku zinavyoenda wanadamu tunazidi kutafuta njia za kurahisha mambo zaidi na pengine bila kuangalia ubora au manufaa ya kitu, haswa inapokuja katika masuala ya afya, na hapo ndio tunapotakiwa kuzingatia uzuri na ubaya wa teknolojia.
  hili suala limenigusa kweli pana upimaji wa malaria siku hizi nadhani hawatumii darubini wataalam wa fani hii tunaomba mtusaidie, pana kitu wanaita rapi test (nadhani huwa wanakifupi chake) RT kitu kama hiki,

  hii imemtokea ndugu yangu, mtoto alikuwa ana homa joto lipo juu sana, kawaida yeye huenda hospital za private, ila siku hiyo akaamua aende ngoja mwananyamala (hospitali ya serikali) kwa kuhisi kuwa pengine angeweza pata huduma nzuri maana siku hizi wanadai pamebadilika,

  alienda mwananyama akaandikiwa hicho kipimo RT mara tu akaletewa majibu, akarudi kwa daktari, akaandikiwa sindano ya "kristapen" ikabidi mama aulize kwani ana tatizo gani daktari akamwambia kuwa tumempima malaria hana! hee!! ikabidi mama ahoji sasa hana malaria hii sindano ya nini?? akaaambiwa wewe mpeleke akachome kwa kweli ilibidi abebe mtoto aondoke na ndipo alipoamua kwenda hospitali ya private mtoto akaonekana ana malaria na akaaanza dawa na anakapona, kwahiyo jamani nadhani ni kweli pana vipimo vingie vya malaria mbadala na darubini, tunaomba wenye utaalam watuelimishe!!
   
 14. s

  saidmbuluma New Member

  #14
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Mmaroroi vifaa ivo vinaonesha negative.Ila inabidi ujiulize we si dokta wala mtu wa maabara kwanini hukatae ukiambiwa huna malaria?Vifaa unavyozungumzia vinaitwa Malaria Rapid diagnotic test(MRDT)au paracheck.Vifaa ni salama ondoa hofu na vimekusudiwa kutumika maeneo ya zahanati ndogo.Muhimu ni ni kufanya uhakiki wa negative slide ya malaria kwa kutumia microscope hapo ndipo utagundua ukweli kuhusu una malaria au la sababu microscope mara nyingi hutoa majibu yasiyo na utata.Ushauri naiomba serikali iwe na utaratibu wa kukusanya hiz negative slide zilizopatikana kwa kutumia paracheck na kuzihakiki kwa kutumia microscope ili kugungua ubora wa vifaa hivi kuliko kuamua kuacha kuvitumia bila kufanya utafiti yakinifu.
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kuongea na mtaalamu mmoja wa malaria kuhusu vijidudu vya malaria kutoonekana katika maabara. Yeye alifananisha vijidudu hivi na samaki walio baharini. Wavuvi wote wanajua baharini kuna samaki lakini hili halina maana kwamba kila akienda kuvua baharini basi ni lazima apate samaki. Kwa kiasi kikubwa itategemea ameenda saa ngapi, maeneo gani la bahari, anatumia kifaa gani kuvua, na umahiri wa mvuvi mwenyewe. Hivyo, pengine haishangazi sana kuona wapimaji wawili au zaidi wanatofautiana katika majibu yao especially kama wanatumia sample tofauti - i.e zilizochukuliwa sehemu tofauti kidoleni? mkononi? etc au nyakati tofauti.

  Baada ya kupima, kitaalamu mpimaji hawezi kusema 'hakuna wadudu wa malaria' anatakiwa asemwe 'hajaona wadudu wa malaria' (i.e. No malaria parasites seen!). Hili linatoa uhuru kwa Daktari ama kuomba vipimo vifanywe upya na mtu mwengine/maabara nyingine au kuzingatia dalili nyingine za mgonjwa na kuamua kutoa 'dawa' ya malaria ama la.

  Ni kweli vifaa vya kupimia malaria vinaweza kuwa sababu ya kuto-detect malaria parasites (hata kama wamo) kwa baadhi ya maabara. Lakini kwa maoni yangu chance ni ndogo sana. Tatizo lipo kwenye watumiaji wa hivyo vifaa (lab technicians). Wengine hawana ujuzi/elimu ya kutosha kutumia vifaa, wengine wana matatizo ya macho na wengine ni uzembe tu (kukosa umakini, haraka kama sample ni nyingi nk!).

  Kama walivyochangia wachangiaji wengine, biashara kuingizwa kwenye huduma za afya kwa kiasi fulani kimemomonyoa maadili ya baadhi ya watendaji katika sector hii.

  Zingatia:

  - Malaria ikichelewa kutibiwa inaweza kuuwa hasa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Unapoona dalili za malaria nenda kwenye hospitali zinazoaminika (sio zile za 'vichochoroni') hata kama ni kwa gharama ya juu kidogo. Afterall unaghramia afya na maisha yako au ya mpendwa wako!

  - Homa sio ugonjwa bali ni 'dalili' tu ya ugonjwa. Si lazima ugonjwa huo uwe malaria, inaweza kuwa ni tatizo jingine. Jieleze vizuri kwa Daktari ili aweze kuelewa tatizo lako. Mara nyingi wagonjwa tumekuwa na tendency ya kuwa pre-empty madaktari kwa kuwaambia tunajisikia 'malaria'. Mwambie unavojisikia naye atakudodosa na kufanya vipimo - kama ni malaria yeye ndio anatakiwa aseme na si wewe mgonjwa.

  - Sio lazima vijidudu vya malaria vionekane hata kama vipo kwenye damu yako. Fuata ushauri wa Daktari. Hata hivyo 'maumivu' yakizidi/yakiendelea muone Daktari.

  - Tumia dawa kwa maelekezo ya Daktari. Usimeze dawa kwa uzoefu wako tu.

  Prevention is better than cure.

  Ni hayo tu kwa sasa.
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Vifaa vinavyotumiwa na Kituo cha Afya Kigamboni ni tofauti kidogo na zingine.Ukishatobolewa damu ikitoka kuna kifaa kama mrija inatumika kutoa damu halafu inawekwa kwenye kifaa kingine.Hii ni kabla ya kupeleka kwenye slide,hivyo kuna uwezekano wa vifaa hivi kutumika kwa mtu zaidi ya mmoja.Na hiyo si ajabu kwani kuna Hospitali moja Nesi alinaswa akimdunga mgojwa aliyelazwa sindano kwa kutumia bomba lililotumika kwa mwingine kutokana na uvivu tu.Nesi huyo aliambulia kibao kutoka kwa Daktari aliyemuona akifanya ukatili huo.Hivyo cha maana kwa wahusika kuchunguza na kufuatilia habari hizi.
   
 17. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Malaria ni ugonjwa unaosumbua sana hivyo vipimo vyake ni vema visimamiwe kwa uhakika.Hata hivyo ugonjwa wa malaria ni bora ingeunganishwa na magonjwa yanayotibiwa bure kama TB,UKIMWI nk.Ili kujaribu kupunguza vifo vinavyosababishwa na malaria kutokana na uwezo duni wa jamii hivyo kupunguza nguvu kazi ya TZ.
   
Loading...