Upepo wa Tundu Lissu 2020, Utakuwa mkali sana!

Unajenga hoja kwa kutumia dhana ya kufikirika katika msingi wa matamanio yako badala ya utafiti wa kisayansi.

Yaani hujawahi kupata hilo jukwaa huru halafu unasema CCM haina tena Ushawishi!

Ni lini ulipata jukwaa huru la kisiasa halafu ukapima kwa kutumia utafiti wa kisayansi kama CCM ina ushawishi au la?

Kuna sayansi gani kwenye siasa? Acha maneno ya kitapeli, kuna sayansi yoyote mahali watu wanaenda kwenye mikutano kufuata vikundi vya burudani na kusikia lugha za kejeli? Mahali ambapo vyombo vya dola vinaagizwa vikawapige wapinzani mabomu, kuna sayansi hapo au mabavu na siasa za kishenzi?
 
Lissu ni mwepesi km karatasi

Watanzania huwa tunamchukulia km mtu aliyechanganyikiwa
 
uran,

Jiulizehuyo tundu alifanya kampeni kwenye uchaguzi wa marudio zanziba, aliambulia nni kama unakumbuka?
 
Mashabiki wa CHADEMA ni kama huwa hamna akili! Nyie mnadhani URAIS ni kama UENYEKITI wa CHADEMA!
Tundu Lissu hana bado hadhi ya URAIS na hana upepo wowote kwenye nafasi hiyo!
Huo ndo ukweli mchungu ambao hamwezi kuukubali!
Kwani nani alijua jiwe angekuwa rais,huwa mnajitoa fahamu wakati mwingine au buku saba imewalevya
 
Kuna sayansi gani kwenye siasa? Acha maneno ya kitapeli, kuna sayansi yoyote mahali watu wanaenda kwenye mikutano kufuata vikundi vya burudani na kusikia lugha za kejeli? Mahali ambapo vyombo vya dola vinaagizwa vikawapige wapinzani mabomu, kuna sayansi hapo au mabavu na siasa za kishenzi?
Ni kweli hakuna sayansi kwenye siasa kwa sababu hata programme za political science ambazo wahusika hupata mpaka PhD in political science ni kupoteza muda tu!

Kama nilivyokueleza huko nyuma, tatizo lako sio ubishi bali ni ubishi usio na mantiki! Unajenga hoja ambazo mtu mwenye fikra pana na uelewa mpana atakata tamaa hata kukujibu kwa sababu unaonyesha hujui lakini unadhani unajua!

Kumuelimisha mtu ambaye hajui lakini anadhani anajua sio kazi rahisi!

Samahani kama nitakukwaza kwa ushauri huu!
 
uran,
Kwanza kabisa Tundu Lissu hawezi rudi Tanzania hivi karibuni. Itamchukua muda mrefu zaidi ya Kambona kurudi. Kumbuka Lissu hasemagi ukweli wowote ni mwongo na tapeli - tukianzia maneno yake ya MIGA, kuzunguka dunia kuisema Tanzania, kuhutubia Senate ya Marekani, kurudi akimaliza matibabu, kuwataja waliompiga risasi, na sasa kugombea urais! Yote ni matendo ya kitapeli kusudi abaki kuwa maarufu, lakini hamna kitu. Moto wa mabua! Hamtishi yeyote.
 
MsemajiUkweli,

Acha nikachekee mbali, hilo political science ni somo la kukariri, hata walioko mbele kwenye siasa sio wenye hiyo elimu. Wengi wa wanaofanya siasa na kutoa maamuzi ya kisiasa, ni watu wenye elimu tofauti na hiyo fani na wasio na elimu kabisa. Kwenye nchi za wenzetu wangalau hiyo elimu ndio inaonekana umuhimu wake. Hapa kwetu figisu kwenye siasa ndio zenye nguvu kuliko hiyo nguvu ya political science.

Hao wenye elimu ya political science wamebaki kuratibu baadhi ya mambo kwenye siasa, lakini maamuzi hasa ya kisiasa yanafanyika kwa upepo tu, tena wanaofanya maamuzi ni vilaza wa ajabu na wenye elimu za fani nyingine kabisa. Mfano mrahisi ulisema baada ya cdm kuuwawa kitaanzishwa chama mbadala, waliotoa mkakati huo ni hao wenye elimu ya political science, cha ajabu wananchi wala hawahitaji hiyo porojo ya wasomi uchwara. Hiki ulichosema kuhusu PhD za hiyo political science, ni kama ule uhanithi aliosema Mwakyembe eti ana degree 4, hivyo mtu asiye na elimu hawezi kumchallange!

Yaani mimi wala sijali na wala usitegemee eti utaniambia jambo linikwazwe, nina ufahamu wa kutosha, na hizo lugha za kuprovoke nazijua na ninazitumia sana kuwatoa watu kwenye mstari, ww ukiwa mmojawapo wa lugha hizo. Yaani nazimudu na hazinipi shida kabisa, maana kwangu inakuwa kama samaki ndani ya maji. Huku jukwaani tuko wengi, hakuna namna tunaweza kufanana michango wala kukubaliana kwa kila kitu. Habari ndio hiyo.
 
MsemajiUkweli

..1995 Mrema alikuwa muongea pumba na vyama vya upinzani vilikuwa vipya ktk jamii ya waTz.

..Dr.Slaa, Prof.Lipumba, DJ Mbowe, waligombea wakati vyama vyao ni dhaifu na hawakuwa wanajulikana kwa waTz.

..Mzee Lowassa alikuwa mgonjwa. Hali yake ktk majukwaa ilikuwa inakatisha tamaa.
MsemajiUkweli,

..uko sahihi 100% kuwa "pumba" ktk siasa ni relative kulingana na mazingira.

..na ninapomlinganisha Jpm na TL sizungumzii mazingira ya Chatham House au Harvard Kennedy school of government.

..nazungumzia mazingira ya Tz ambapo Jpm na TL watauza sera na ilani zao kwa wananchi wa kawaida.

..Ni yupi kati ya wawili hao ana uwezo wa kujenga hoja zenye mashiko na ushawishi?

..Yupi ataweza " ku-connect " na wapiga kura?

..na hoja yangu ya mwisho ni kuwa Tz tuna matatizo makubwa ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, na kiutawala, na ccm ndiyo chama kilichokuwa madarakani. Mzigo wa lawama unaangukia kwa ccm na siyo wapinzani.

..binafsi sidhani kama ccm iko salama kwa 100% ukizingatia matatizo na changamoto sugu na za muda mrefu zinazoikabili nchi yetu.
 
Walishindwa kuandamana kwa kupokonywa ubunge kiwazi wazi jimboni kwake
Walishindwa kuandamana kwa Mwenyekiti wao wa Taifa kuwekwa ndani.zaidi ya miezi kadhaa,,,na huenda krismass hii akailia ndani ya gereza kutokana na mwenendo wa kesi yao
Halafu leo mnasema ati Pepo inavuma kwa kasi kwa Lisu 2020
Labda itavuma mapepo
 
Mashabiki wa CHADEMA ni kama huwa hamna akili! Nyie mnadhani URAIS ni kama UENYEKITI wa CHADEMA!
Tundu Lissu hana bado hadhi ya URAIS na hana upepo wowote kwenye nafasi hiyo!
Huo ndo ukweli mchungu ambao hamwezi kuukubali!
Hadhi ya Urais ipoje mkuu?? Mimi naona ukishapewa ndo unapewa hiyo hadhi, mtu hawi na hadhi hiyo kabla ya kuwa Rais.
 
Walishindwa kuandamana kwa kupokonywa ubunge kiwazi wazi jimboni kwake
Walishindwa kuandamana kwa Mwenyekiti wao wa Taifa kuwekwa ndani.zaidi ya miezi kadhaa,,,na huenda krismass hii akailia ndani ya gereza kutokana na mwenendo wa kesi yao
Halafu leo mnasema ati Pepo inavuma kwa kasi kwa Lisu 2020
Labda itavuma mapepo
FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Kwanza kabisa Tundu Lissu hawezi rudi Tanzania hivi karibuni. Itamchukua muda mrefu zaidi ya Kambona kurudi. Kumbuka Lissu hasemagi ukweli wowote ni mwongo na tapeli - tukianzia maneno yake ya MIGA, kuzunguka dunia kuisema Tanzania, kuhutubia Senate ya Marekani, kurudi akimaliza matibabu, kuwataja waliompiga risasi, na sasa kugombea urais! Yote ni matendo ya kitapeli kusudi abaki kuwa maarufu, lakini hamna kitu. Moto wa mabua! Hamtishi yeyote.
Wewe ni m'bishi tu.
Inamaanisha hujui kama Lissu alishambuliwa?
Watanzania wengi machozi yakawatoka?
Wakamwombea Mungu amnusuru, wakashangilia walivyomuona akiwa Hai tena?
Lissu ni Moto
 
Jiulizehuyo tundu alifanya kampeni kwenye uchaguzi wa marudio zanziba, aliambulia nni kama unakumbuka?
Amekuwa mtu mwingine sasa.
Waliompiga wamempa credit ya juu kabisa
 
Wafanye wafanyalo watanzania waleo hawatishiwi hawangombani na wadhulumati ni wajanja ni wazalendo bali watakususia kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Hata wale uliowapa ulaji wanakula tu kwa kuwa njaa inawauma lakini hawapo na wewe. Siku moja wakiamua kukugeuka wanakugeuka.

Katika enzi hizi za digit vikao zaidi ya milioni moja zinfanyika kwa Massa 12. Kwa utaratibu huu ni bora ukawaruhusu kusema hadharani kuliko kuzibwa midomo angalau utanaweza kupata mawazo yao.

Karne hii ya 21 na watu wake ni hatari kuliko Bomu la Nuclear wasibezwe unaweza ukajikuta uko uchi muda wote bila wewe kujua. Nawaogopa sana watu wa kizazi hichi kwa kuwa wana uelewa mkubwa na hawadanganyiki
uran,
 
Ujinga ujinga tu maana tunaambiwa ushindi wa ccm ni wa wizi wa kura miaka yote sasa wamuogope Lisdu kwa vp kama wao wanategemea kuiba kura? Kja Lowassa watu wakaongea ya kuongea ila baada ya matokeo ya uchaguzi yakarudi maneno yaleyale ya wizi wa kura na sasa Lissu,pia baada ya matokeo ya uchaguzi yatarudiwa yaleyale ya wizi wa kura yani watanzania sijui wana matatizo ya kisaikolojia ama vp?
 
Back
Top Bottom