Upepo wa Tundu Lissu 2020, Utakuwa mkali sana!

MsemajiUkweli,

..kwa mara ya kwanza CCM itakuwa na mgombea anayezungumza pumba katika majukwaa kulinganisha na mgombea wa upinzani.

..TL anaweza kulitawala jukwaa hata kwa masaa 3 na wananchi wasichoke kumsikiliza. Jpm ni lazima asaidiwe na wasanii, viongozi wa dini, na utitiri wa wazungumzaji.

..Hali ya maisha ya Watanzania ya umasikini na ukosefu wa ajira ni mambo ambayo hayarekebishiki kwa muda mfupi uliobaki. Sidhani kama Jpm ataweza kujitetea pale TL atakapojenga hoja za kuishitaki ccm kwa matatizo yanayoikabili Tanzania.
 
tindo,
Umeandika maelezo marefu lakini hayana mantiki(contradictory premises)

Kama umeelewa ulichokiandika basi utakuwa na tatizo la logical fallacy in reasoning!
 
Una mzungumzia Tundu Lisu uyu aliye chukua vipande vya fedha akiwa na DJ ili kumpitisha maMvi agombee urais kupitia Chadema ikiwa pamoja na kumsafisha kwa tuhuma za ufisadi. Yaani unawachukulia pooa Watanzania!!!, Yaani unatuona Watanzania wote Nyumbu!!
 
Nakumbuka kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita Lowasa akiwa juu kisiasi wote tuliamini atashinda, katika mkutano mmoja wapo alisema kama chadema hawatashinda uchaguzi Mkuu ule kupitia yeye basi itabidi wasubiri kwa miaka mingine hamsini! Ngoja tuone itakuwaje
Na ule utabiri ndio wa ukweli kabisa. Inaweza kufika miaka 100.
 
Hata kama hutapenda lkn jilazimishe kumpenda Rais aliyeko madarakani sasa hivi - kwa kazi nzuri aliyofanya tutamuongezea miaka mingine mitano 2020 - 2025
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kama Magufuli anayo hadhi ya kuwa rais, mtu asiyemjua hata Gaddafi alikuwa rais wa wapi, Lissu atakosa hadhi kweli??
Mashabiki wa CHADEMA ni kama huwa hamna akili! Nyie mnadhani URAIS ni kama UENYEKITI wa CHADEMA!
Tundu Lissu hana bado hadhi ya URAIS na hana upepo wowote kwenye nafasi hiyo!
Huo ndo ukweli mchungu ambao hamwezi kuukubali!
 
Kwa type ya watu waliowahi kuitawala nchi hii na hata waliopo madarakani sasa ni kielelezo tosha kuwa anaweza.
Hao leadership failures ni "The Pale Shadow of Himself".
 
JokaKuu,
Neno ''pumba'' kwenye siasa ni relative term! Uchokidhani ni ''pumba'' kuna wengine wanadhani sio ''pumba''.

''Pumba'' kwa nani na anayeongea ''pumba'' anaongea katika mazingira gani?

Marekani inaongozwa kwa sasa na Rais ambaye wakati wa kampeni baadhi ya watu na manazi wa chama cha democrat walikuwa wanasema anaongea ''pumba''.

Uingereza ambayo kwa sasa iko kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu inaenda kuongozwa na Waziri Mkuu ambaye baadhi ya watu na manazi wa chama cha Labour wanadai ni ''muongo'' na anaongea ''pumba''

Nimekupa mifano hai ya Marekani na Uingereza kukuonyesha kuwa neno ''pumba'' kwenye siasa ni relative term.

Kikubwa zaidi, historia inaonyesha katika nchi za Afrika huwezi kumshinda ''incumbent president'' katika Uchaguzi Mkuu kama Rais huyo yuko katika uongozi kwa miaka 5. Tumeona ya juzi yaliyotokea huko Botswana na Namibia. Aliyekuwa Rais wa Botswana Ian Khama alijiunga na wapinzani ili kupambana na Rais aliyeko madarakani lakini juhudi zake zimegonga mwamba.

Nilitegemea unajua hali halisi lakini maelezo yako yanaonyesha hujui au unajenga hoja kwa kutumia matamanio yako.

Nimalize kwa kukuambia,Mikutano ya siasa na kampeni sio intellectual gathering.
 
Mashabiki wa CHADEMA ni kama huwa hamna akili! Nyie mnadhani URAIS ni kama UENYEKITI wa CHADEMA!
Tundu Lissu hana bado hadhi ya URAIS na hana upepo wowote kwenye nafasi hiyo!
Huo ndo ukweli mchungu ambao hamwezi kuukubali!
Mtajamba cheche, kama wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji wamewasababisha ccm waweke mpira kwapani, basi Lissu atawajambisha cheche ccm na dikteta wao jiwe.
 
Magufuli siyo populist sema anaonekana hivyo kwa sababu ameziba mianya yote ya kukosolewa.

Kama Magufuli angeweka Mizania sawa ya kisiasa kama alivyojaribu mzee Kikwete angekuwa na wakati mgumu sana kuliko wakati wowote ule.

Kwanza kwa sasa ccm haina hoja yoyote ya maana kupambana na vyama vingine vya siasa ccm bila vyombo vya dola hawawezi kusimama hata round moja, wamechoka kisera, kisiasa, kimikakati na kila kukicha wanakosa political strategists.

ccm wameweza kusurvive awamu hii kwa sababu ya vyombo vya dola tu huyo Bashiru na Polepole hawana hata robo ya uwezo aliokuwa nao Kinana na Nape, hawana uwezo wa kupambana kwa hoja hata na Ole Sosopi tu au Ado Shaibu.

Ni kweli Magufuli atakuwa na uchaguzi mwepesi kwa sababu ametumia vibaya mamlaka yake dhidi ya wapinzani wake
Jeshi la polisi, tume ya uchaguzi, na msajili wa vyama vya siasa ndiyo ngao zake na siyo kwa sababu ya uongozi wake bora, he is just a jackal of all trades but a master of non. MsemajiUkweli,
 
Umeandika maelezo marefu lakini hayana mantiki(contradictory premises)

Kama umeelewa ulichokiandika basi utakuwa na tatizo la logical fallacy in reasoning!

Hutakiwi uelewe chochote maana inawezekana kusiwe na maelezo yanayokufurahisha kabisa. Lakini uelewe Magufuli hana uwezo wowote wa kushawishi wapiga kura zaidi ya kutumia mabavu na vitisho kupitia madaraka yake. Anaweza kushinda ila sio kwakuwa katatua au atatatua matatizo ya hao masikini, bali mfumo mbovu wa uchaguzi unaoweza kumpatia ushindi, ndio hasa nguzo yake halisi.
 
PTER,
Niliposoma hii sentesi yako nikajua hujui populist leaders ni viongozi wa aina gani!
''Magufuli siyo populist sema anaonekana hivyo kwa sababu ameziba mianya yote ya kukosolewa''

Halafu kwa kukusaidia tu, CCM sio Dkt, Bashiru na Polepole. Kwenye Uchaguzi Mkuu unapofika, ndio maana utaona viongozi wote wastaafu wa CCM na wasio wastaafu hufikia mpaka kupanda majukwaani kupiga kampeni. Hii inaonyesha ni jinsi gani wanakuwa wameshiriki katika kutengeneza strategy za chama kushinda katika uchaguzi. Kwa hiyo kudhani Strategist wa CCM ni Bashiru na Polepole pekee ni kujidanganya na kutoijua vizuri CCM.
 
Tunamuhitaji Lissu aje kuiandaa Tanzania kisheria zaidi. Huku tunapokwenda vijana wasipoandaliwa vizuri ukatili na chuki zinaweza kuathiri nchi yetu.

Tuungane kumuunga mkono agombee ili asaidie kuiweka Tanzania katika mstari wa kisheria na katiba ifanyekazi yake. Hatuwezi kuwafundisha watoto wetu siasa za uwongo uwongo. Na tutapata serikali inayoweza kujiendesha bila kuingiliana.

Naunga mkono Lissu agombee na atapata kura za watanzania wote.
 
ccm katika jukwaa huru haina ushawishi tena kwa wananchi hata kama wamwite yesu aje awasaidie kufanya kampeni.

Kinachoifanya ccm iendelee kuishi katika siasa ni vyombo vya dola tu na ccm wanalijua hill ndiyo haitatokea ccm ikaruhusu mazingira sawa ya kisiasa kwa sababu ndiyo utakuwa mwisho wake.
Niliposoma hii sentesi yako nikajua hujui populist leaders ni viongozi wa aina gani!
''Magufuli siyo populist sema anaonekana hivyo kwa sababu ameziba mianya yote ya kukosolewa''

Halafu kwa kukusaidia tu, CCM sio Dkt, Bashiru na Polepole. Kwenye Uchaguzi Mkuu unapofika, ndio maana utaona viongozi wote wastaafu wa CCM na wasio wastaafu hufikia mpaka kupanda majukwaani kupiga kampeni. Hii inaonyesha ni jinsi gani wanakuwa wameshiriki katika kutengeneza strategy za chama kushinda katika uchaguzi. Kwa hiyo kudhani Strategist wa CCM ni Bashiru na Polepole pekee ni kujidanganya na kutoijua vizuri CCM.
 
MsemajiUkweli,

Ni hivi anaongea pumba ila madaraka yake ndio yanambeba, inshort anabore. Hao wapinzani njia yako kubwa ya kukutana na wananchi ni kupitia mikutano, na huko ndio wanajenga ushawishi. Magufuli amezuia hilo kwani ana wivu wa kisiasa pindi anapoona chama kingine kinapata watu, hivyo namna pekee ni kutumia madaraka yake vibaya kugomea wananchi kusikia vyama vingine.

Lakini hata hivyo hiyo haijamsaidia yeye wala chama chake kukubalika kulinganisha na nguvu anayotumia ili akubalike. Mfano wa dhahiri kuwa yeye na chama chake hawakubaliki, ni idadi ndogo sana iliyojitokeza kujiandikisha kupiga kura uchaguzi wa SM, mpaka ikabidi ipikwe idadi kuficha aibu. Jiwe hana mvuto na Lissu ana mvuto wa hatari.
 
Niliposoma hii sentesi yako nikajua hujui populist leaders ni viongozi wa aina gani!
''Magufuli siyo populist sema anaonekana hivyo kwa sababu ameziba mianya yote ya kukosolewa''

Halafu kwa kukusaidia tu, CCM sio Dkt, Bashiru na Polepole. Kwenye Uchaguzi Mkuu unapofika, ndio maana utaona viongozi wote wastaafu wa CCM na wasio wastaafu hufikia mpaka kupanda majukwaani kupiga kampeni. Hii inaonyesha ni jinsi gani wanakuwa wameshiriki katika kutengeneza strategy za chama kushinda katika uchaguzi. Kwa hiyo kudhani Strategist wa CCM ni Bashiru na Polepole pekee ni kujidanganya na kutoijua vizuri CCM.

Kwani hao viongozi wastaafu kupanda jukwaani ndio inamaanisha wanamvuto au kukubalika? Wanapata jukwaa la kuongea sio kwa sababu wanamvuto, bali ccm inaamini hao wanakubalika hivyo wanawapa nafasi. Kitu pekee kinachoibeba ccm ni tume ya uchaguzi na vyombo vya dola fullstop.
 
ccm katika jukwaa huru haina ushawishi tena kwa wananchi hata kama wamwite yesu aje awasaidie kufanya kampeni.

Kinachoifanya ccm iendelee kuishi katika siasa ni vyombo vya dola tu na ccm wanalijua hill ndiyo haitatokea ccm ikaruhusu mazingira sawa ya kisiasa kwa sababu ndiyo utakuwa mwisho wake.
Unajenga hoja kwa kutumia dhana ya kufikirika katika msingi wa matamanio yako badala ya utafiti wa kisayansi.

Halafu unaposema, ''CCM hata kama wamwite Yesu aje awasaidie kufanya kampeni'' ni kuonyesha dharau kwa waumini wa dini fulani na kutojua umuhimu wa Yesu katika maisha ya baadhi ya waumini.

Kwa akili yako una maana kuwa, Mungu Mwana hawezi kuwashawishi wananchi kwa lolote kuhusu CCM hata kama atataka kufanya hivyo! Huu ni ujinga au kutojua nguvu za Yesu!

Yaani hujawahi kupata hilo jukwaa huru halafu unasema CCM haina tena Ushawishi!

Ni lini ulipata jukwaa huru la kisiasa halafu ukapima kwa kutumia utafiti wa kisayansi kama CCM ina ushawishi au la?
 
Back
Top Bottom