Upepo umegeuka, sasa ni Makongoro Nyerere!

Upepo umegeuka, sasa ni Makongoro Nyerere!

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
6,067
Reaction score
2,229
Mkuu Pasco najua wajua naongelea nini!

Hatimaye ndugu charles Makongoro aka MAKO ameshatangaza nia kama ilivyotarajiwa sasa kilichobaki ni kumtembeza tu...

kashfa hana zaidi ya majungu tu!

Twende kazi 2015.
Cc: Mzee Mwanakijiji

 
Last edited by a moderator:
Makongoro ni nani ?
Ni vema mkamuelezea kwa kuweka historia yake, cv nk wengine hatumjui.
 
Makongoro amekuja kivingine kwani ujumbe wa nje wa nchi umehudhuria na kumkubali!
 
Mkuu Pasco najua wajua naongelea nini!
Hatimaye ndugu charles Makongoro aka MAKO ameshatangaza nia kama ilivyotarajiwa sasa kilichobaki ni kumtembeza tu...


kashfa hana zaidi ya majungu tu!

Twende kazi 2015.
Cc: Mzee Mwanakijiji

Mtafute yuko kwenye kundi gani!.

Nikikusoma katikati ya mstari Mzee Mwanakijiji inamaana CCM huwa hakuna demokrasia? Ile ya kukaa kamati kuu kuchuja majina mara NEC yao nayo inachuja na Mkutano mkuu kupiga kura ni kiini macho? Yani Makongoro 'apewe'? Apewe na nani? Kwa utaratibu upi? Na 'jamaa yake' Pasco watamfanyaje? Eti kaka Pasco kumbe uongozi mnapeana? Process yote ni kiini macho?
Mkuu Mzito Kabwela, kwenye watangaza nia wa CCM, kuna watangaza nia tuu ili nao waonekane tuu kuwa wanauweza urais kufuatia JK kuifanya taasisi ya urais kuwa very cheap, kama JK amekuwa rais na ameweza, then every Tom, Dick and Harry think he/she can be a president!.


Hivyo kwenye watia nia hao, yapo wakundi matano,

kundi la kwanza ni ni wale nawaita ma show off tuu kuwa na wao wanaweza!, hawa wanajijua hawawezi kuchaguliwa, ila wanajitia kimbembele tuu ili na wao wajionyeshe kuwa ni presidential materiale!. Hili ndilo kundi kubwa.

Kundi la pili ni kundi la watu serious ambao wana uwezo wa kuwa rais na wanautaka urais kwa dhati, wengine kwaudi na uvumba and by all means!. Kundi hili lina watu wachache kama Lowassa, Membe na Wasira.

Kundi la Tatu la watia nia, ni kundi la Wasindikizaji tuu, hawa nawaita 'pace makers' wameletwa ili kuonyesha urais una unashindani, ni wale ambao wanajijia kuchaguliwa hawawezi, lakini watagombea ili tuu kuwasindikiza baadhi ya wagombea wao makini just in case anything can happen, mgombea wao asipopitishwa kwa sababu zozote zile, then watumike kama fall back positions, mfano ni watu kama Magufuli, Nchimbi, Lukuvi, Ngeleja etc.

Kundi la Nne, ni ni la wagombea zuga tuu ili kuzipooza hasira za watu, kundi hili mostly litahusisha wagombea kutoka Zanzibar, kufuatia urais wa muungano ni suala la muungano na ulipaswa kupokezana kati ya Bara na Zanzibar, na pia kuna mpekezano wa Dini kati ya Mkristu na Muislamu, then, alipomaliza Mkapa ambaye ni Mkristu kutoka Bara, alipaswa afuatiwe na Muslamu kutoka Zanzibar, lakini kwa vile kitu kinachoitwa "Mtandao" kiliishabuniwa na kuwepo in place, kikaangalia aliyepaswa kumpokea Mkapa ni Muislamu kutoka Zanzibar, ili kubadili mchezo, Huyo Muislamu kutoka Zanzibar ilimbidi ashughulikiwe na kupotezewa kabla!, ili game liweze kurudi bara kwa excuse kuwa Zanzibar hakuna mtu!, kilichomkuta wengi mnakijua!, na "jamaa wa sehemu walihakikisha no post-mortem' ili kuthibitisha ni kazi ya Mungu!. Sasa kufuatia 1995 rais alitoka bara, 2005 rais akatoka tena bara, this time 2015 ki haki, kimuungano na kihalali ni zamu ya Zanzibar, lakini kwa vile mgombea wa CCM aliyemaliza ni Muislamu, na mgombea wa CCM wa 2015 tayari yupo, huu mchakato ni zuga tuu, then CCM wakituletea Muislamu mwingine, 'Kanisa' linaweza lisikubali, waliangalia uwezekano wa kumshawishi Jaji Ramadhani, ili kumtumia tuu kama zuga kuwazuga Wazanzibari, akaishtukia hii dili, akawagomea kata kata na hakuna Mkristo mwingine Presidential materia kutoka Zanzibar, hivyo CCM itahakikisha inawachagiza baadhi ya wagombea kutoka Zanzibar kugombea ili kuzugia tuu!.

Kundi la tano ni la watia nia mimi ninaowaita madekio au madodoki ya kusafishia watu!. Kufuatia mmoja wa wagombea kusemekena alikataliwa na Baba wa Taifa, masikini Makongoro, bila ya yeye kujijua, huku anafahamika wazi sio presidential material, ameshawishiwa na 'wenyewe' agombee kwa kuahidiwa ati rais atakayepitishwa ni yeye ili tuu kumuenzi baba wa Taifa, atapitishwa kwenye tatu bora, yeye, Mzanzibari wa zuga, na mgombea rasmi, kwenye Mkutano Mkuu, Makongoro atajitoa na kusema kura zake wampe 'fulani', sambamba na huyo Mzanzibari nae pia atajitoa na kusema kura zake wampe fulani, hivyo mgombea wa CCM atapitishwa unanimously na CCM itaibuka as one, stronger than ever. Hivyo huyu Makongoro amewekwa pale kama dekio tuu!, la kusafishia watu njia ya ikulu!.

Kundi la sita ni Vichinjio, hili ni kundi ambalo wenyewe hawautaki urais, ila ni heavy guards, hawa watashawishiwa kutangaza nia ili CCM iwatumie kama chinjio la kuchijia waloe heavy guards wasiotakiwa. Mfano mzuri ni Mizengo Pinda na Fredrick Sumaye, siamini kama hawa ni kweli wanautaka urais, bali wamechagizwa kugombea ili kuwatumia kama chinjio!. Kwa vile Lowassa ni kipenzi cha watu na ameupania sana urais, calibre yake ni Waziri Mkuu, ili kuhalalisha kumchinjia baharini, CCM imemshawishi Waziri Mkuu mwingine mstaafu nae agombee, na Waziri Mkuu incumbent pia agombee ili kwenye kikao cha maamuzi, ijengwe hoja hatuwezi kupitisha mawaziri wakuu wastaafu watatu, tutapitisha mmoja, huyu ni yupi, hatuwezi kumkata incumbent tukampitisha wazamani, hivyo wa kwanza kuchinjwa atakuwa ni Sumaye, akifuatiwa na Lowassa, hivyo kujikuta kafungwa mdomo!.

Kundi la saba, la mwisho ni la Akiba Uzeeni, hawa wanatumia mtindo unaitwa the JK style. Hili ni kundi la vijana ambao umri bado sana, hivyo wanatangaza nia ili tuu kujenga profile ya 2025, kama alivyofanya JK 1995 na kuja kuchukua 2005.

Pasco
 
Last edited:
Urais ni zaidi ya kutokuwa na kashfa, uwezo wa kufikiri, kuamua, kutekeleza na kusimamia unachokiamini ni muhimu kuzingatiwa... Ifike wakati na sisi tuone fahari kuwa na rais mwenye IQ kubwa!! (siku tukiwa na rais kichwa kama Muhongo- Prof (sina maana awe Muhongo) kama taifa tutasonga mbele.
 
BONGE BONGE Katika watangaza nia wote ndani ya CCM, ni Makongoro na Mwandosya tu ndio wanaoweza kunifanya nifikiri iwapo kura yangu iende CCM au iende UKAWA; wengine wote wananirahishia kupeleka kura UKAWA.
 
Last edited by a moderator:
Pasco ndugu yangu huachi unafiki!

Makongoro kaja kama suprise tena suprise ya mwaka huu.najua kuwa unajua alternative ya Makongoro ni UKAWA ....this is according to the 'system'...acha ubishi bana!
 
ninavyoona atakae tia nia wa mwisho ndiye atakua gumzo kwa kuwa watia nia wanavizia mwenzao aliyetangulia kasema nini ili apate pa kumkosoa mfano ni wa huyu makongoro. wao hawajui kuwa wananchi wanawasoma tu na wanawajua kuliko hata wanavyojijua mi nashauri ccm iwaambie watia nia waseme kuwa wamejitokeza kuwania kiti bila kutaja majina ya watu na kukosoa walicho sema kwa sababu kila mtia nia ana staili yake.

alafu makongoro kutuambia kuwa atarudisha nidhamu ya chama akimkosoa mwigulu lazima ajue hiyo staili kwa wasio na chama haiwausu na lazima ajue ccm haiwezi shinda uchaguzi kwa kutegemea wanachama wake pekee.

hivyo swala la nidhamu eti kisa mwigulu kakosoa utendaji wa serikali kwa ambao awana chama haiwausu yeye alitakiwa kuwaambia wananchi atawafanyia nini ili kuirudisha nchi kwenye msitari ambao ata yeye anakiri imezungukwa na watawala mafisadi.
 
Back
Top Bottom