Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 33,203
- 74,770
Ni takribani wiki nzima sasa nasikiliza wimbo mmoja tu,Upepo cover aliyoifanya Ray C.
Baada ya kusikiliza version hii ya Ray C nikajaribu kusikiliza original version aliyofanya Rachel! Sikutumia hata sekunde 10 niliachana nayo na kurudi kusikiliza aliyoimba Legendary Ray C.
Kwa ujio huu umenifumbua masikio kusubiria ngoma kali kutoka kwako,naamini hutoniangusha...
Sijawahi kuwa shabiki wa msanii yeyote wa kike Tanzania hii zaidi ya Ray C,kwa jide nilijishikiza tu lakini sasa nimerudi nyumbani.
Niliposikiliza wimbo huu nililia sana.
Hiki kipaji kilishapotea!
Nafurahi umerudi tena,nakupenda sana Ray C,sana.
Tafadhali usiyarudie madawa...Kama sivyo leo hii huyo Yemi Alade angekuwa si lolote Afrika hii.
Nimeweka link hapo juu,team muziki mzuri mtajua namaanisha nini baada ya kusikiliza.
Hauhitajiki kurudia mara 2 kuuona uzuri wa huu wimbo.
Rachel kapotezwa vibaya sana humo.
Naam,Ray C is baaaaaaaaack
P.S Ray C pls fanya cover ya Nashukuru ya Recho,kwa ajili yetu mashabiki wako.
Asante
Nifah