Upendo wa mama

Upendo wa mama

Sasa nimeelewa
Na wanaume wengi (sio wote lakini ) waliolelewa na mama zao kwa upendo huwa wazuri kwenye jamii, kinyume sana na wale waliojeruhiwa nafsi zao na mama zao , huwa wakatili waharibifu wa amani na jamii ke kwa ujimla, most of the times ni users.
 
Huwezi jua nafasi ya baba mpaka utakapo kuwa baba.
Kwangu mimi namzungumzia mama sana kwa sababu ndie mtu alietaka niwe hivi.

Japo tukiwa wadogo baba alilaza mshale akatuacha na mama lakin mama ameendelea kutusimulia mema ya baba, nakiri hajawahi msema vibaya mzee kwetu, ila sina cha kusema kuhusu yeye maana sijawahi kuwa nae katika makuzi yangu.
Asante mkuu, umekua unbiased.

Kwa experience yangu, mara nuingi mtoto anapolelewa na mzazi mmoja lazima ataegemea upande huo huo na kuna uwezekano wa kutoona umuhimu hata kwake baadae kuwa na muungano ktk family. Mfano mtoto wa kike amelelewa na mama ktk makuzi yake hataona umuhimu wa baba then kuna possibility ya yeye kwendelea na trend hiyo hiyo (siyo wote, miongoni)
 
Leo asubuhi katika pitapita zangu, nimekutana na watoto wadogo wakiwa wamebeba mizigo ya kuni kichwani, nikajikuta nimekumbuka tukio muhimu maishani mwangu ambalo nimeona tushirikiane tu kulitafakari, pengine linaweza kuongeza kitu fulani katika malezi ya watoto wetu.

Miaka 17 imepita sasa, jumapili moja tulienda kuchanja kuni, baada ya kuridhika na viwango vya mizigo yetu, mimi dada yetu na mdogo wangu tukajitwika mizigo ya kuni zetu kichwani tukaanza safari, njia tuliyokuwa tunapita kuelekea nyumbani, ilipita kwa bibi (mdogo wa bibi alotuzalia mama)

Baada ya kufika kwa bibi tukashauriana tuiache ile mizigo pale maana tulikua tumechoka na mizigo ya kuni ni mizito. Kweli tukapita kwa bibi tukatua mizigo yetu tukamwambia tutaifata kesho baada ya kutoka shule, bibi akatugea msosi tukapiga tukaenda zetu home, mambo megine yakaendelea.

Siku iliyofuata jioni mimi na mdogo wangu tukaenda kuichukua mizigo yetu ya kuni, hapo ndo nikagundua ile mizigo ilikua mizito, maana kwa umbali wa kama 2.5km na mzigo kichwani tulipumzika mara kadhaa, mpaka tulipofika nyumbani.

Baada tu ya kufika nyumbani na kutua ule mzigo kichwani mama akaanza kutugombeza kwanini tumechelewa akasema maneno mengi, kilicho niumiza ni kubeba mzigo mzito kichwani na nilipoufikisha nikatukanwa. Niliumia mno.

Tukaenda kuoga mie na mdogo wangu kisha tukatoka kuelekea barabarani tukivuta muda bi mkubwa amalizie kupika tuufinye, coz nyumba yetu ilikua katikati ya mji. Tukiwa hapo, bi mkubwa akaja kutuita, sie tukajua msosi tayari.

Ile tumemfikia akatukumbatia kisha akatuomba msamaha, ndo kusema "nilijua mlikua mnacheza njiani ndo maana niliwatukana na nilipanga kuwapiga, kumbe kweli kuni ni nzito" yaani nilihisi kukabwa kooni nikajikuta nalia kwa uchungu na furaha ikiwa imechanganyika, mama akanibembeleza hapo nikanyamaza akatuomba msamaha. "NAOMBA MNISAMEHE WANANGU" Kauli hii imegoma kufutika kichwani.
She is a legend.
 
Kuna ile hali ni mama mzazi ila anamchukia mwanae najua ni wachache wamepitia hii. Unakuta mama yako mzazi anakuambia ww hukua kwenye mpango wangu kuzaliwa bila kutarajiwa, mara na kuchukia sana, kwa kuchukua sura ya baba liangalie hili. Ukifanya biashara yeye ni kukuvunja moyo utaona kama utafanikiwa, kukusemea vibaya kwa mzazi mwenzako dah mm sielewi naona ajabu mnavyosema upendo wa mama, mm kwangu ni upendo wa baba umepitiliza. Ingawa mzee ni kauzu flani ila hivyo hivyo ili mradi
 
Leo asubuhi katika pitapita zangu, nimekutana na watoto wadogo wakiwa wamebeba mizigo ya kuni kichwani, nikajikuta nimekumbuka tukio muhimu maishani mwangu ambalo nimeona tushirikiane tu kulitafakari, pengine linaweza kuongeza kitu fulani katika malezi ya watoto wetu.

Miaka 17 imepita sasa, jumapili moja tulienda kuchanja kuni, baada ya kuridhika na viwango vya mizigo yetu, mimi dada yetu na mdogo wangu tukajitwika mizigo ya kuni zetu kichwani tukaanza safari, njia tuliyokuwa tunapita kuelekea nyumbani, ilipita kwa bibi (mdogo wa bibi alotuzalia mama)

Baada ya kufika kwa bibi tukashauriana tuiache ile mizigo pale maana tulikua tumechoka na mizigo ya kuni ni mizito. Kweli tukapita kwa bibi tukatua mizigo yetu tukamwambia tutaifata kesho baada ya kutoka shule, bibi akatugea msosi tukapiga tukaenda zetu home, mambo megine yakaendelea.

Siku iliyofuata jioni mimi na mdogo wangu tukaenda kuichukua mizigo yetu ya kuni, hapo ndo nikagundua ile mizigo ilikua mizito, maana kwa umbali wa kama 2.5km na mzigo kichwani tulipumzika mara kadhaa, mpaka tulipofika nyumbani.

Baada tu ya kufika nyumbani na kutua ule mzigo kichwani mama akaanza kutugombeza kwanini tumechelewa akasema maneno mengi, kilicho niumiza ni kubeba mzigo mzito kichwani na nilipoufikisha nikatukanwa. Niliumia mno.

Tukaenda kuoga mie na mdogo wangu kisha tukatoka kuelekea barabarani tukivuta muda bi mkubwa amalizie kupika tuufinye, coz nyumba yetu ilikua katikati ya mji. Tukiwa hapo, bi mkubwa akaja kutuita, sie tukajua msosi tayari.

Ile tumemfikia akatukumbatia kisha akatuomba msamaha, ndo kusema "nilijua mlikua mnacheza njiani ndo maana niliwatukana na nilipanga kuwapiga, kumbe kweli kuni ni nzito" yaani nilihisi kukabwa kooni nikajikuta nalia kwa uchungu na furaha ikiwa imechanganyika, mama akanibembeleza hapo nikanyamaza akatuomba msamaha. "NAOMBA MNISAMEHE WANANGU" Kauli hii imegoma kufutika kichwani.
Mama's honesty
 
Wazazi wote ni sawa Mimi mama alikuwa ananipiga lkn ucku baba akija akiniona nimekaa kinyonge ananiuliza nikimwambia nimechapwa anamwambia mama samweli usimpige Sana mtoto atakuchukia naye mama hivohivo nikimkosea baba bc yeye ananiombea msamaha kwa baba hivyo bc wote wanaumuhimu Sana sana
 
Back
Top Bottom