Upendo wa mama

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,940
3,825
Leo asubuhi katika pitapita zangu, nimekutana na watoto wadogo wakiwa wamebeba mizigo ya kuni kichwani, nikajikuta nimekumbuka tukio muhimu maishani mwangu ambalo nimeona tushirikiane tu kulitafakari, pengine linaweza kuongeza kitu fulani katika malezi ya watoto wetu.

Miaka 17 imepita sasa, jumapili moja tulienda kuchanja kuni, baada ya kuridhika na viwango vya mizigo yetu, mimi dada yetu na mdogo wangu tukajitwika mizigo ya kuni zetu kichwani tukaanza safari, njia tuliyokuwa tunapita kuelekea nyumbani, ilipita kwa bibi (mdogo wa bibi alotuzalia mama)

Baada ya kufika kwa bibi tukashauriana tuiache ile mizigo pale maana tulikua tumechoka na mizigo ya kuni ni mizito. Kweli tukapita kwa bibi tukatua mizigo yetu tukamwambia tutaifata kesho baada ya kutoka shule, bibi akatugea msosi tukapiga tukaenda zetu home, mambo megine yakaendelea.

Siku iliyofuata jioni mimi na mdogo wangu tukaenda kuichukua mizigo yetu ya kuni, hapo ndo nikagundua ile mizigo ilikua mizito, maana kwa umbali wa kama 2.5km na mzigo kichwani tulipumzika mara kadhaa, mpaka tulipofika nyumbani.

Baada tu ya kufika nyumbani na kutua ule mzigo kichwani mama akaanza kutugombeza kwanini tumechelewa akasema maneno mengi, kilicho niumiza ni kubeba mzigo mzito kichwani na nilipoufikisha nikatukanwa. Niliumia mno.

Tukaenda kuoga mie na mdogo wangu kisha tukatoka kuelekea barabarani tukivuta muda bi mkubwa amalizie kupika tuufinye, coz nyumba yetu ilikua katikati ya mji. Tukiwa hapo, bi mkubwa akaja kutuita, sie tukajua msosi tayari.

Ile tumemfikia akatukumbatia kisha akatuomba msamaha, ndo kusema "nilijua mlikua mnacheza njiani ndo maana niliwatukana na nilipanga kuwapiga, kumbe kweli kuni ni nzito" yaani nilihisi kukabwa kooni nikajikuta nalia kwa uchungu na furaha ikiwa imechanganyika, mama akanibembeleza hapo nikanyamaza akatuomba msamaha. "NAOMBA MNISAMEHE WANANGU" Kauli hii imegoma kufutika kichwani.
 
Nmejikuta niamba ule wimbo wa Christian Bella Nani Kama mama
 
Mapenzi ya mama hayafananishwi na chochote, hata yeye ile hali ya kuwatukana haikumtoka haraka alijiona mkosaji kwa wanae kwa muda mrefu sana
 
Angekuwa Mdingi angepiga kimya huku moyoni akijua amekosea.
Tena angejifaragua kwa kusema 'tukuni twenyewe twepesi tu halafu mnachelewa hivi'
Kwenye hii dunia hakuna kama Mama.
Baba yangu ana miaka 71 lakini hadi leo akipata matatizo huwa anasema "kama mama yangu (yake) angekuwepo haya yasingenipata"
Kauli hii unifikirisha sana na nimegundua kuwa licha ya uzee wa Baba yangu lakini upendo wa mama yake aliyekufa miaka mingi iliyopita haujafutika moyoni mwake.
Ndugu zangu wanaume, zawadi kubwa tunayoweza kuwapa watoto wetu ni kuwapenda na kuwaheshimu mama zao.Tafadhali usimtukane wala kuvunjia heshima mkeo mbele ya watoto wenu.
Kwa wale mliowatelekeza Mama zenu vijijini hamtumi hata mia ya sabuni tafadhali badilini fikra zenu hata kama mama yako alikukosea sana.
 
Kila mzazi ana role yake muhimu kukufanya ulivyo,awe wa kike au wa kiume.Nimelelewa na wazazi wote wawili na sasa wametangulia mbele ya haki.Huwa siungi mkono hii tabia ya kumtukuza mama peke yake, huku baba haumpi umuhimu.Kwangu Mimi wazazi wote walikuwa muhimu mno.
 
Kila mzazi ana role yake muhimu kukufanya ulivyo,awe wa kike au wa kiume.Nimelelewa na wazazi wote wawili na sasa wametangulia mbele ya haki.Huwa siungi mkono hii tabia ya kumtukuza mama peke yake, huku baba haumpi umuhimu.Kwangu Mimi wazazi wote walikuwa muhimu mno.
Asante kwa kuliona hilo. Yaani watu wa namna hiyo hawajui baba naye alivumilia mangapi kwa ajili yao. Tena wakati mwingine maudhi ya kutosha tu kutoka kwa hao mama zetu, lakini nao walivumilia kwa ajili ya familia. Hivyo wazazi wote wanahitaji kupongezwa kwa usawa.
 
Mwenye upendo wa dhati ni mama wote watakugaya ila sio mama mzazi,elfu tano unayompa mama ina worth milion dolar utakayompa mpenzi wako shukrani na baraka zake na atakavyojihisi furaha mama
Nilipokuwa mdogo nilikuwa na mawazo kama yako. Lakini baada ya kujitambua na mimi kuwa na majukumu ya kifamilia, nimegundua kuwa wazazi wote wanauzito ulio sawa. Tuache kuwa tunawabagua baba zetu.
 
nani kama mama? jibu hakuna
Wazazi wote wana uzito sawa. Unadhani baba yako naye alivumilia mangapi kutoka kwa mama yako mpaka ukakua? Usikute mama alikuwa na mchepuko lakini mzee akavumilia tu kwa ajili yako. Tusiwabague eti tu kwa kuwa wao si warusha lawama kwa watoto kuhusu wazazi wenzao kama walivyo akina mama.
 
Kweli mkuu.
Mama anakutakia mema kuliko yeyote, kwa kidogo unachompa anahisi kapokea kila kitu katika dunia
Mwenye upendo wa dhati ni mama wote watakugaya ila sio mama mzazi,elfu tano unayompa mama ina worth milion dolar utakayompa mpenzi wako shukrani na baraka zake na atakavyojihisi furaha mama
 
Kabisa mkuu! Hiki kitendo kimenifanya nimuone mama kuwa watofauta sana, hasa inapotokea nimetofautiana na mtu, huwa naikumbuka sana hii scenario
Woooow that’s beautiful thing, I can feel
 
Back
Top Bottom