Heshima kwenu wakuu.
Upendo ni nguvu kubwa kuliko zote zilizoko katika huu ulimwengu. Nguvu zingine ni za uvutano, upepo, radi n.k. Tofauti na hizo nguvu zingine, UPENDO upo ndani ya mtu, ndani ya moyo na nafsi yake.
Unapomwambia mtu 'nakupenda' naye akakujibu 'nakupenda pia' --kimsingi alichokifanya ni kukurudishia upendo uliompa. Jitazame mbele ya kioo chako, utaona sura yako nzuri. Kama kioo kimekreki, sura yako itaonekana kana kama ina ufa. Endapo ina lensi mbinuko, basi na sura yako itaonekaka kana kwamba imebonyea. Ili uone sura yako vizuri, tumia kioo kizuri.
UPENDO ni maisha ni uhai wa mwanadamu. Ukimpenda m2 lakini yeye hakupendi - achana naye tafuta akupendaye.
Unapohangaika na m2 asiyethamini UPENDO unaompa ni sawa na kujichukia kwa sababu ya kuona sura yako ni mbaya mbele ya kioo chenye lensi mbinuko. Hahaaa. Usithubutu kujiua kwa sababu mwanamke/mwanaume fulani amekukataa... hapana, hapana. Upendo wako umo ndani mwako, sio kwa huyo aliyekukataa.
Ukijiua kwa kukataliwa, sisi tunafahamu kwmb umekufa sio kwa sababu ya huyo jamaa/binti, ila kwa sababu ulishindwa kutumia nguvu za upendo zilizoko ndani mwako. Ukajijengea hisia za hasira na chuki--umejichukia mwenyewe.
UPENDO una nguvu kuliko MAUTI.