Upendo Peneza: Nahitaji kushinda na nitashinda

Status
Not open for further replies.
Aug 7, 2014
8
95
Mimi UPENDO binti wa PENEZA maisha yangu yamejaa mapambano yasiyoisha duniani. Nimekuwa mtu wa kuthubutu kinyume na mategemeo ya rafiki,wazazi na ndugu zangu kwa ujumla. Nimehatarisha heshima yangu kwa jamii kwa sababu ya ndoto zangu,utu wangu umejaribiwa kufifishwa mara nyingi lakini nilisimama kama mtu mzima maana kwa mila za kiafrica mtoto wa kike akiwa mpambanaji hupewa tafsiri nyingi lakini sikujali na sitajali.
Kwa kiasi Fulani nimefanikiwa kuchomoza na kung'ara lakini naamini sijafika ninapotaka kufika,ninachojua moyoni mwangu nitashinda kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Mwaka 2009 nishiriki maisha plus ya kwanza(season 1),nilikotokea wengi hampajui lakini kwa faida ya wengi mimi ni msichana wa kawaida kutoka kwenye familia ya kawaida na pengine msomaji wangu yawezekana unatoka kwenye mazingira kama ya kwangu. Niling'ara(ukubali usikubali) sikunyakua taji lakini kuna mengi niyolijifunza.

February mwaka huo huo wa 2009 nilijiunga na CHADEMA bila kushawishiwa na mtu yeyote nilitafuta Makao makuu ya CHADEMA ambapo nilipata kadi yangu ya uanachama iliyosainiwa na JOHN&[HASHTAG]#8203[/HASHTAG]; MREMA, Mkurugenzi makao makuu ya CHADEMA. Baada ya kupata kadi na kusoma wajibu wa mwanachama,sikurudi nyuma,sikuiweka mfukoni na kuiweka nyumbani bali kwa ujasiri mkubwa na bila kujali uzoefu wangu wa kisiasa,nilijiunga na oparesheni kubwa kuwahi kutokea kwenye historia ya vyama vingi (OPARESHENI SANGARA) iliyozinduliwa kanda ya ziwa .Nilishiriki kikamilifu kwenye mkoa wa Tanga na sehemu ya mkoa wa Kilimanjaro,ikumbukwe kwamba gharama zote za kujikimu zilikuwa juu yangu tofauti na makamanda wengine sababu ikiwa kwamba nilijitolea kwenye oparesheni hiyo.

Namkumbuka sana Marehemu REGIA MTEMA ambaye alinikaribisha na kulala naye chumba kimoja kwa siku kadhaa,kiukweli alinipunguzia sana gharama za maisha na nilipata ushauri mwingi wa namna ya kuishi kwenye siasa. Kwa kifupi nimeshiriki oparesheni nyingi pamoja na chaguzi mbalimbali na zote hizi zimenijenga sana kisiasa,kijamii na kupanua uelewa wangu juu ya uzalendo na moyo wa kuutumikia umma.

Mwaka 2010 niligombea ubunge viti maalum nikiwa na umri wa miaka 22 na nilileta changamoto kubwa na nilikuwa miongoni mwa wagombea wenye ushawishi mkubwa,sikuteuliwa lakini moyo wangu ulipata medani nyingi za ujasiri,upendo,uvumilivu na kutokata tamaa. Zaidi sana iliniongezea kujitambua kuwa mimi ni nani,nina uwezo gani na ninaweza kutimiza nini hapa duniani.

Nimalizie kwa kusema kwamba nina deni kubwa sana kwa chama changu cha CHADEMA kimenijengea ujasiri wa kupambana na maisha haya bila uoga hata kidogo na nimepata msukumo wa kugombea nafasi kubwa ya kisiasa ili kuwasemea wasio na sauti ya kuweza kusikilizwa na watawala.
KWA PAMOJA TUNAWEZA.

NAAMINI kwamba vijana wanaweza kuleta mabadiliko hapa nchini, lakini mabadiliko hayo hayawezi kuonekana kwa sasa kama vijana hawataingizwa kwenye taasisi mbalimbali na kushirikishwa katika vyombo vya kutoa maamuzi."

Hivyo ndivyo anavyoanza kuzungumza na safu hii, mwanasiasa chipukizi, Upendo Furaha Peneza, ambaye mwaka jana alishiriki katika shindano la mchezo wa Maisha Plus akiwakilisha Mkoa wa Mwanza.

Upendo alijizolea umaarufu zaidi katika shindano hilo aliloshika nafasi ya tatu, mrembo huyu ameamua kujiingiza katika medani ya siasa akiwa na imani kuwa vijana wana uwezo mkubwa wa kutawala endapo vyama vya siasa vitawajengea misingi mizuri ya kufikia mafanikio.

anasema kama vyama vya siasa vitaanzisha mifuko ya kukusanya fedha zitakazotumika kuwawezesha vijana watakaohitaji kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi mbalimbali.

Peneza anasema kuwa wapo vijana wengi wenye uwezo wa kuongoza ambao wakipewa nafasi wanaweza kuonyesha vipaji walivyonavyo lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa kukosa usaidizi.

"Vijana wenyewe kwanza wajitambue, waipende nchi yao kwa uzalendo na vyama vya siasa vianzishe mifuko ya kuwasaidia vijana waweze kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa mwaka huu," anasema.

Anabainisha kuwa iwapo vyama vya siasa havitatenga mifuko ya kuwasaidia vijana, kamwe kundi hilo halitaweza kupata uzoefu unaohitajika katika medani ya siasa ya vyama vingi ambayo imejaa mikikimikiki ya hapa na pale.

Upendo anasema vijana wanaweza kuanzisha utaratibu wa kuchangishana fedha zitakazotumika kuwasaidia wenzao wenye ari ya kuingia katika medani ya siasa lakini hawana uwezo wa kiuchumi kufanya kampeni zitakazowawezesha kufikisha ujumbe wao kwa wapiga kura.

Anasema ana uhakika mazingira ya siasa yakiwa mazuri pamoja na vijana kuwezeshwa kundi hili litajitokeza kwa wingi kuwania nafasi za serikali za mitaa, udiwani, ubunge na kiti cha urais.
Anabainisha kuwa nguvu za vijana katika vyama ni chachu kubwa ya mafanikio kwa kwa kuwa kundi hilo kwa muda mrefu limekuwa halishiriki kikamilifu kwenye chaguzi.

"Vijana wakipewa nafasi wanaweza, ile nadharia kwamba vijana hawawezi imepitwa na wakati labda wazee wachukuliwe kwa sababu ya uzoefu tu," anasema.

Chipukizi huyo katika siasa pamoja na kuanika ushiriki wake kwenye medani hiyo amegoma kutaja ni mwanachama wa chama gani, ila anasema siasa ipo kwenye damu yake na anaamini ipo siku atashika nafasi za juu za uongozi nchini.

Upendo anasema moja kati ya mambo yanayomkera ni vigezo vinavyotolewa na baadhi ya taasisi, wizara, kampuni na viwanda za kuwataka vijana wawe na uzoefu wa miaka fulani katika kazi ili waweze kuajiriwa.

Anasma katika maisha ya kawaida vijana wengi hawana uzoefu wa kutosha kwa sababu ya kutoka vyuoni ambako kwa kiasi kikubwa hujifunza kinadharia kuliko vitendo vifanyikavyo ofisini.

"Kijana amemaliza chuo leo anataka kazi halafu unamwambia awe na uzoefu kwanza, sasa atautoa wapi kama si kumkandamiza kimaendeleo?" anahoji mwanasiasa huyo ambaye kwasasa anajiendeleza na elimu ya juu.

Shirikisho la Afrika Mashariki
Anasema misingi ya kuanzisha shirikisho hilo ni zuri lakini halitakuwa na maana kama wananchi hawatapewa elimu ya kutosha juu ya faida na hasara zake kuliko kuwashinikiza au kuwalazimisha wakubali kulianzisha.

Anabainisha kuwa serikali za Kenya na Uganda kwa muda mrefu zilitilia mkazo suala la elimu na hivi sasa kiwango chao kipo juu tofauti na Tanzania inayosuasua kwenye sekta hiyo, jambo linaloweza kuwapa wakati mgumu wananchi wake kukabiliana na soko la ajira.

Anasema elimu inaweza kuwa silaha pekee itakayowasaidia vijana wa Tanzania kupambana na wenzao kutoka Uganda au Kenya, hivyo ni vema serikali ikaendelea kuboresha vyuo vya ufundi na vinginevyo kwa lengo la kupatikana kwa wataalamu waliobobea.

Anasema vijana wapatiwe mitaji mapema ili waanze kujiendeleza katika biashara ya ujasiriamali kwa lengo la kujijenga kiuchumi kuepuka hatari ya kuwa vibarua kwa wageni watakaokuja kuwekeza hapa nchini.
Uwepo wa viti maalumu
Anabainisha kuwa uwepo wa viti maalumu ni sehemu ya kuwajengea wanawake uzoefu wa kisiasa na kuwaonyesha kuwa wakipewa nafasi ya uongozi wanaweza lakini nafasi hizo zisichukuliwe kuwa kigezo cha wanawake kutokuwa na uwezo wa kupambana na wanaume katika majimbo.

Anasema wanawake wanao uwezo wa kuachana na utegemezi wa viti hivyo kama wakiamua, kwa kuwa kura nyingi wanazozipata wanaume majimboni zinatoka kwa wanawake.

"Tunahitaji kuwa na idadi kubwa ya wanawake kutuwakilisha bungeni lakini hatutaweza kufanikiwa kama tutaendelea kung'ang'ania viti maalumu badala ya kujielekeza majimboni," anasema.
Anasema kuwa hivi viti maalumu vimesaidia kuondoa dhana katika jamii kuwa hata ushirikiano wa wanawake una tija katika jamii yetu, kwani ukiwaendeleza wanawake unaendeleza taifa.

Kuzilinda ndoa
Anasema baadhi ya wanawake hasa walioolewa wamekuwa wakipambana na vikwazo mbalimbali, ikiwemo kutoka kwa wanaume wao ambao huwa wagumu kuwapa ruhusu ya kushiriki siasa.

Anaweka bayana kuwa mwanamke aliye kwenye ndoa kushiriki katika siasa si tiketi ya kumdharau mumewe au kuitelekeza familia yake kwa kisingizio cha kuwa na majukumu mengi, bali anapaswa ajipangie ratiba nzuri ili aweze kuyatekeleza kwa wakati husika.

Anawashauri wanawake kujitambua kwa uwezo wao hasa watoto wa kike wanaosoma kuzingatia elimu ambayo itawasaidia kukabiliana na changamoto za maisha na familia zao.

"Wanawake tujijenge katika mazingira ya kupigania haki zetu za misingi katika jamii, mfano huduma za afya, maeneo mengine hakuna sehemu nzuri ya kujifungulia&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];hivyo ni wajibu wetu kupigania sehemu kama hizo ziboreshwe," anasema.

Anaongeza kuwa wale ambao ni viongozi wasimamie vizuri matumizi ya fedha zinazotengwa kwa huduma hizo na kuwa watetezi wazuri.

Upendo anamalizia kwa kuwapa wanawake wote wosia kuwa kamwe fursa sawa za uwakilishi katika ngazi za maamuzi haziwezi kufikiwa kama hawatashirikiana kuutokomeza mfumo dume ambao kwa muda mrefu umekuwa ukimuweka kando mwanamke katika mambo mbalimbali.

mia
 
Yote haya unayasema hapa yanatufanya tu pay attention na tukuheshimu na kuku wish all the best.

But ole wako katika safasri yako hiyo uanze 'kuwavulia watu chupi' ili ufanikiwe tutakuja kukuponda na kukudharau na yote mazuri yako tunaweza shindwa kuyaona ...all the best
 
Hongera sana kamanda,
Mfano wako mzuri, somo zuri kila rakheri mkuu
 
Yote haya unayasema hapa yanatufanya tu pay attention na tukuheshimu na kuku wish all the best
but ole wako katika safasri yako hiyo uanze 'kuwavulia watu chupi' ili ufanikiwe tutakuja kukuponda na kukudharau na yote mazuri yako tunaweza shindwa kuyaona ...all the best
Mkuu, maccm ndio zao hizo, wanawake mpaka wavue ch**p ndio wapate nafasi,

Mabungr yote ya maccm viti maalum yana hilo tatizo.

Ukitaka kujua muulize mangula na mpambe wake wa hapa JF watakwambi.
 
Kila la kheri Furaha. Kadri tunavyoendelea mbele na saa ya ukombozi ikikaribia hatutakuwa na msamaha kwa msaliti yeyote bila kujali cheo chake. Karibu ktk mapambano haya. Nilisema post zilizopita kuwa kinachoendelea hivi sasa kuhusu BMK na ushirika wa UKAWA ni mchujo wa aina yake kutokea. Wasliti wote tutawajua na haitazuia mwendelezo wa mapambano ya kweli ktk kulikwamua taifa hili. Tuko pamoja.
 
Asante Mutakyamirwa,saa ya ukombozi ni sasa
 
NAAMINI kwamba vijana wanaweza kuleta mabadiliko hapa nchini, lakini mabadiliko hayo hayawezi kuonekana kwa sasa kama vijana hawataingizwa kwenye taasisi mbalimbali na kushirikishwa katika vyombo vya kutoa maamuzi."

Hivyo ndivyo anavyoanza kuzungumza na safu hii, mwanasiasa chipukizi, Upendo Furaha Peneza, ambaye mwaka jana alishiriki katika shindano la mchezo wa Maisha Plus akiwakilisha Mkoa wa Mwanza.

Upendo alijizolea umaarufu zaidi katika shindano hilo aliloshika nafasi ya tatu, mrembo huyu ameamua kujiingiza katika medani ya siasa akiwa na imani kuwa vijana wana uwezo mkubwa wa kutawala endapo vyama vya siasa vitawajengea misingi mizuri ya kufikia mafanikio.

anasema kama vyama vya siasa vitaanzisha mifuko ya kukusanya fedha zitakazotumika kuwawezesha vijana watakaohitaji kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi mbalimbali.

Peneza anasema kuwa wapo vijana wengi wenye uwezo wa kuongoza ambao wakipewa nafasi wanaweza kuonyesha vipaji walivyonavyo lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa kukosa usaidizi.

"Vijana wenyewe kwanza wajitambue, waipende nchi yao kwa uzalendo na vyama vya siasa vianzishe mifuko ya kuwasaidia vijana waweze kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa mwaka huu," anasema.

Anabainisha kuwa iwapo vyama vya siasa havitatenga mifuko ya kuwasaidia vijana, kamwe kundi hilo halitaweza kupata uzoefu unaohitajika katika medani ya siasa ya vyama vingi ambayo imejaa mikikimikiki ya hapa na pale.

Upendo anasema vijana wanaweza kuanzisha utaratibu wa kuchangishana fedha zitakazotumika kuwasaidia wenzao wenye ari ya kuingia katika medani ya siasa lakini hawana uwezo wa kiuchumi kufanya kampeni zitakazowawezesha kufikisha ujumbe wao kwa wapiga kura.

Anasema ana uhakika mazingira ya siasa yakiwa mazuri pamoja na vijana kuwezeshwa kundi hili litajitokeza kwa wingi kuwania nafasi za serikali za mitaa, udiwani, ubunge na kiti cha urais.
Anabainisha kuwa nguvu za vijana katika vyama ni chachu kubwa ya mafanikio kwa kwa kuwa kundi hilo kwa muda mrefu limekuwa halishiriki kikamilifu kwenye chaguzi.

"Vijana wakipewa nafasi wanaweza, ile nadharia kwamba vijana hawawezi imepitwa na wakati labda wazee wachukuliwe kwa sababu ya uzoefu tu," anasema.

Chipukizi huyo katika siasa pamoja na kuanika ushiriki wake kwenye medani hiyo amegoma kutaja ni mwanachama wa chama gani, ila anasema siasa ipo kwenye damu yake na anaamini ipo siku atashika nafasi za juu za uongozi nchini.

Upendo anasema moja kati ya mambo yanayomkera ni vigezo vinavyotolewa na baadhi ya taasisi, wizara, kampuni na viwanda za kuwataka vijana wawe na uzoefu wa miaka fulani katika kazi ili waweze kuajiriwa.

Anasma katika maisha ya kawaida vijana wengi hawana uzoefu wa kutosha kwa sababu ya kutoka vyuoni ambako kwa kiasi kikubwa hujifunza kinadharia kuliko vitendo vifanyikavyo ofisini.

"Kijana amemaliza chuo leo anataka kazi halafu unamwambia awe na uzoefu kwanza, sasa atautoa wapi kama si kumkandamiza kimaendeleo?" anahoji mwanasiasa huyo ambaye kwasasa anajiendeleza na elimu ya juu.

Shirikisho la Afrika Mashariki
Anasema misingi ya kuanzisha shirikisho hilo ni zuri lakini halitakuwa na maana kama wananchi hawatapewa elimu ya kutosha juu ya faida na hasara zake kuliko kuwashinikiza au kuwalazimisha wakubali kulianzisha.

Anabainisha kuwa serikali za Kenya na Uganda kwa muda mrefu zilitilia mkazo suala la elimu na hivi sasa kiwango chao kipo juu tofauti na Tanzania inayosuasua kwenye sekta hiyo, jambo linaloweza kuwapa wakati mgumu wananchi wake kukabiliana na soko la ajira.

Anasema elimu inaweza kuwa silaha pekee itakayowasaidia vijana wa Tanzania kupambana na wenzao kutoka Uganda au Kenya, hivyo ni vema serikali ikaendelea kuboresha vyuo vya ufundi na vinginevyo kwa lengo la kupatikana kwa wataalamu waliobobea.

Anasema vijana wapatiwe mitaji mapema ili waanze kujiendeleza katika biashara ya ujasiriamali kwa lengo la kujijenga kiuchumi kuepuka hatari ya kuwa vibarua kwa wageni watakaokuja kuwekeza hapa nchini.
Uwepo wa viti maalumu
Anabainisha kuwa uwepo wa viti maalumu ni sehemu ya kuwajengea wanawake uzoefu wa kisiasa na kuwaonyesha kuwa wakipewa nafasi ya uongozi wanaweza lakini nafasi hizo zisichukuliwe kuwa kigezo cha wanawake kutokuwa na uwezo wa kupambana na wanaume katika majimbo.

Anasema wanawake wanao uwezo wa kuachana na utegemezi wa viti hivyo kama wakiamua, kwa kuwa kura nyingi wanazozipata wanaume majimboni zinatoka kwa wanawake.

"Tunahitaji kuwa na idadi kubwa ya wanawake kutuwakilisha bungeni lakini hatutaweza kufanikiwa kama tutaendelea kung'ang'ania viti maalumu badala ya kujielekeza majimboni," anasema.
Anasema kuwa hivi viti maalumu vimesaidia kuondoa dhana katika jamii kuwa hata ushirikiano wa wanawake una tija katika jamii yetu, kwani ukiwaendeleza wanawake unaendeleza taifa.

Kuzilinda ndoa
Anasema baadhi ya wanawake hasa walioolewa wamekuwa wakipambana na vikwazo mbalimbali, ikiwemo kutoka kwa wanaume wao ambao huwa wagumu kuwapa ruhusu ya kushiriki siasa.

Anaweka bayana kuwa mwanamke aliye kwenye ndoa kushiriki katika siasa si tiketi ya kumdharau mumewe au kuitelekeza familia yake kwa kisingizio cha kuwa na majukumu mengi, bali anapaswa ajipangie ratiba nzuri ili aweze kuyatekeleza kwa wakati husika.

Anawashauri wanawake kujitambua kwa uwezo wao hasa watoto wa kike wanaosoma kuzingatia elimu ambayo itawasaidia kukabiliana na changamoto za maisha na familia zao.

"Wanawake tujijenge katika mazingira ya kupigania haki zetu za misingi katika jamii, mfano huduma za afya, maeneo mengine hakuna sehemu nzuri ya kujifungulia…hivyo ni wajibu wetu kupigania sehemu kama hizo ziboreshwe," anasema.

Anaongeza kuwa wale ambao ni viongozi wasimamie vizuri matumizi ya fedha zinazotengwa kwa huduma hizo na kuwa watetezi wazuri.

Upendo anamalizia kwa kuwapa wanawake wote wosia kuwa kamwe fursa sawa za uwakilishi katika ngazi za maamuzi haziwezi kufikiwa kama hawatashirikiana kuutokomeza mfumo dume ambao kwa muda mrefu umekuwa ukimuweka kando mwanamke katika mambo mbalimbali.

mia
 
Uwepo wa viti maalumu
Anabainisha kuwa uwepo wa viti maalumu ni sehemu ya kuwajengea wanawake uzoefu wa kisiasa na kuwaonyesha kuwa wakipewa nafasi ya uongozi wanaweza lakini nafasi hizo zisichukuliwe kuwa kigezo cha wanawake kutokuwa na uwezo wa kupambana na wanaume katika majimbo.

Anasema wanawake wanao uwezo wa kuachana na utegemezi wa viti hivyo kama wakiamua, kwa kuwa kura nyingi wanazozipata wanaume majimboni zinatoka kwa wanawake.

"Tunahitaji kuwa na idadi kubwa ya wanawake kutuwakilisha bungeni lakini hatutaweza kufanikiwa kama tutaendelea kung'ang'ania viti maalumu badala ya kujielekeza majimboni," anasema.

Anasema kuwa hivi viti maalumu vimesaidia kuondoa dhana katika jamii kuwa hata ushirikiano wa wanawake una tija katika jamii yetu, kwani ukiwaendeleza wanawake unaendeleza taifa.
She got brain,big brain l swear
 
Kila la kheri Furaha. Kadri tunavyoendelea mbele na saa ya ukombozi ikikaribia hatutakuwa na msamaha kwa msaliti yeyote bila kujali cheo chake. Karibu ktk mapambano haya. Nilisema post zilizopita kuwa kinachoendelea hivi sasa kuhusu BMK na ushirika wa UKAWA ni mchujo wa aina yake kutokea. Wasliti wote tutawajua na haitazuia mwendelezo wa mapambano ya kweli ktk kulikwamua taifa hili. Tuko pamoja.

Hatukatishwi tamaa na wasaliti daima
 
Never give up, you can do better than you think and I believe that u can. The only thing which you can do quickly is to increase self confidence which you have.
 
Ungetuambia na Elimu yako pia ingeongeza nguvu kwenye waraka wako huu

Elimu kitu gani wewe hao mnaowaita wasomi si ndo hao wanaiangusha nchi kinachohitajika ni ule moyo wa uzalendo na kujitambua hao wasomi mbona ndege zinakuja beba mchanga wa dhahabu ha pa kwetu na kwenda kupima huko ulaya ina maana wazungu wamewadharau wasomi hakuna wengi jua kali tu.
 
Hongera sana kwa kuthubutu na moyo wako wa uzalendo. Usikate tamaa ili uweze kutimiza malengo yako. Pamoja na yote uyafanyayo jaribu kuwaelimisha wanawake wenzio waone umuhimu wa mabadiliko nchini kwani wao ndio mtaji wa magamba.
 
Katika mambo yote umenifurahisha sana kuitambua chadema kama taasisi na sio kikundi cha watu ama mtu binafsi kama ilivyo tafasiri kwa watu fulani,Asante sana and nakuwish mafanikio mema katika safari yako,uongozwa na dhamira ya kweli na mafanikio yake utayaona

Vijana wengi wanapenda kutengenezewa njia na wao wapite tu ila ww umeitengeneza njia yako mwenyewe,naiona nyote yako ikig'hara......Inshaallaah mungu atakuongoza na kuepuka vishawishi vya wale wasiopenda watanzania tujielewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom