Upendo Nkone-Usifurahi Juu Yangu

Upendo Nkone-Usifurahi Juu Yangu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638


Usifurahi juu yangu eeeh adui yangu
Niangukapo mimi nitasimama tena
Kumbuka niwapo gizani bwana ni nuru yangu
Hawezi kuniacha bwana mimi niangamie ×2


Si vyema kunisema vibaya nipatapo tatizo
Shetani wampa nafasi ndani ya moyo wako
Kumbuka kwa maobi yako nitasimama tena
Na utapata baraka kutoka kwake mungu ×2


Maana heri mtu yule ambaye kinywa chake
Ni kuwabariki wenzake na kiwaombea
Maana maneno mabaya huchafua moyo
Ukiwekwa mbali na mungu ni vyema uwe safi
Ukiona niko kwenye shida niombee
Ndoa yangu imevunjika wewe niombee
Nikifukuzwa kazini ndugu niombee
Magonjwa yananiandamaa niombee
Biashara haina faida niombee
Nikikawia kupata mtoto niombee
Nimekuwa mtoto yatima niombee
Ata nijapo kuwa mjane niombee


Ujue kwa maobi yako mimi nitasimama tena
Ujue kwa maobi yako nitabarikiwa ×4
 
Back
Top Bottom