Updates za yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA

Updates za yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Mwenyekiyi wa Chadema anakaribia Makao Makuu ya Polisi muda mfupi atakuwa anaingia hapo. Police wameanza kukamata watu waliojitokeza kumsindikiza Mwenyekiti. Huku waandamanaji wanapambana na askari wa FFU vikali. Mji mzima ni balaa.
c1.jpg

Jeshi la polisi jijini Dar es Salaam limetumia mbwa na virungu kuwatanyama mamia ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Manendeleo Chadema ambao walifurika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa lengo la kumsindikiza Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye aliitwa kwa mahojiano.

Chanzo: ITV

i1.jpg

Dodoma Maandamano ya kupinga Bunge la Katiba

dodoma2.jpg

maandamano.jpg

Nipo hapa makao makuu ya polisi jijini Dar es Salam,nimekuja kumsindikiza mwenyekiti wangu Freema Mbowe akahojiwe na hawa polisi,watu ni wengi sana hapa,polisi wametanda kila eneo,pia sura za makachero naziona pia,

kamanda Mnyika kamaliza kuongea na wandishi wa habari na makamanda wengine,anasema mpaka sasa Mwekiti Mbowe hajahojiwa na polisi ,amewakatalia na kuwagomea polisi kuandikisha maelezo kwa shitaka la kutoa maneno ya uchochezi,kuna mabishano makubwa ya kisheria,Mbowe amekubali kuandika kwamba amegoma kutoa maelezo mpaka pale utata wa kisheria utakapoisha.

cha kusikitisha polisi wamewapiga vibaya na kuwaumiza waandishi wa habari wa Daily News na Josephat Isango wa TanzaniaDaima,waandishi hao walijikuta wakipokea kipigo kikali kutoka kwa polisi licha ya kuonesha vitambulisho vyao vya kazi,bt polisi waliendelea kuwapiga mpaka pale mkuu wao alipotokea na kuwazuia,polisi hao waliwapga watu kadhaa walihisi ni wanachama wa CHADEMA.

mtikila.jpg
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA na Mwenyekiti wa chama cha UDP Mch. Mtikila, alifika kwenye viunga vya Makao Makuu ya polisi akiwa ndani ya pikipiki ya mataili matatu maarufu kama Bajaji,huku akipunga mkono wa vidole vi3 kuashiria UKAWA, lakini polisi walimzuia kuingia ndani ya jengo na Mtikila kuwaambia "laiti mngejua kwamba tunachokipigania UKAWA ni kuwakomboa nyie na Watanganyika kwa ujumla msingenizuia"
 
Attachments

  • mnyika.jpg
    mnyika.jpg
    27.9 KB · Views: 1,963
Last edited by a moderator:
naona hapa polisi waliojihamu kwa mabomu ya machozi na silaha za moto wanajaribu kuwakabili vijana waliomsindikiza kamanda mbowe
 
Mwenyekiyi wa Chadema anakaribia Makao Makuu ya Polisi muda mfupi atakuwa anaingia hapo. Police wameanza kukamata watu waliojitokeza kumsindikiza Mwenyekiti. Huku waandamanaji wanapambana na askari wa FFU vikali. Mji mzima ni balaa. .Tutataheshimiana tu

hizi ni BROKEN NEWZ. umesimama kwenye mnara gani hadi uione dsm nzima?
 
FFU wanagawa kichapo, kuna magari machache ya CDm hapo Makao Makuu ya Polisi...
 
Mwenyekiyi wa Chadema anakaribia Makao Makuu ya Polisi muda mfupi atakuwa anaingia hapo. Police wameanza kukamata watu waliojitokeza kumsindikiza Mwenyekiti. Huku waandamanaji wanapambana na askari wa FFU vikali. Mji mzima ni balaa. .Tutataheshimiana tu

Nawakumbuke Tumeanza na Mungu tupo na Mungu na tutamaliza na Mungu
 
Mwenyekiyi wa Chadema anakaribia Makao Makuu ya Polisi muda mfupi atakuwa anaingia hapo. Police wameanza kukamata watu waliojitokeza kumsindikiza Mwenyekiti. Huku waandamanaji wanapambana na askari wa FFU vikali. Mji mzima ni balaa. .Tutataheshimiana tu

Pambaneni makamanda hakuna kulala ukombozi uko karibu.....Oparesheni Pamoja Daima..

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom