Mpira umekwisha simba imefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu na goli moja lililofungwa dakika ya 24 kwa shuti ilililopigwa na Echesa nakumaliziwa na beki wa Azam kwa bahati mbaya, ilikuwa mechi ngumu sana. sasa tuna msubilia Yebo Yebo... Maji Maji 1 Africa Lyon 1...
Hongera Azam FC kuwa na tovuti tena anayokuwa updated mara kwa mara. Club kubwa na kongwe kama Simba na Yanga zimeshindwa kuwa na tovuti licha ya kuwa na uwezo wa kuajiri waamuzi wa kimataifa na kusajili wachezaji wa kimataifa. Uswahili ndo umetawala.
Yanga Asili ilikuwa rahisi sana kuiibia timu hasa pesa ya getini, ndiyo maana akina Mzimba na wanzake walikataa kabisa Yanga kuwa kampuni ampaka alipopewa pesa Manji na JK na kuanza kuzunguka Tanzania nzima kuonyesha umoja!? baada ya kupata chake nasikia alipata mtaji wa kupasua mbao... lakini Yanga kama kampuni wanafanya biashara gani pale maana hata bamia huwa sizioni au wako kwenye mchakato, walisema watauza hisa sijawasikia tena au nikimya kimya...nilikua nikishangaa sana eti watu wakati ule wanapinga Yanga kuwa kampuni, wakati ni jambo la kisasa kabisa...eti yanga asili, ulikua ni ujinga sana.
Ala kumbe ligi inaendelea mimi nilifikiri tushatwaa Ubingwa
Hahahaaa, we acha tu, sa hii watu wanafukua maiti huko kuroga mechi za raundi ya pili!!!
Leo Simba na Mtibwa sijui matokeo huko vipi?
Simba 3 Mtibwa 1...Simba Bingwa hamtakiiii?
ligi ya darts ndo huwa inaamuliwa kwa mechi chache hivyo...
Msikurupuke waungwana...
Kwanza ingekuwa jambo la kheri mngejichangisha ili mpake rangi jengo lenu.
duh simba bingwa tena....ushindi wa mezani huo
Hata Sielewi mkuu, ngoja tuvute mkuu Mafuluto na Mastau nadhani soon watakuja na Data