UPDATES: US midterm election results

Ila yote kwayote mi katika marais wote namkubali Trump huyu wala sio mnafiki nyeusi nyeusi nyeupe nyeupe kwan huyo Obama sindio alivamia Libya nakumuua Gaddafi asaiv anajifanya watu hawataki vita.....dunia lazima tuheshimiane kwamtutu wabunduki
 
CCM inafanya wizi wa kura ambao umeonekana dhahiri shahiri. Ni mpumbavu tu ndio atapinga hilo.
Pia hakuna tume huru ya uchaguzi,umeona wapi tume ya uchaguzi inasimamiwa na chama tawala!?
Na bado mkashinda ubunge
 
Hizi wiki 2 zimekua tamu sana huko Bibi Nyau chaliii na huku Orange man chalii pia. Walimwengu kwa ujumla walishamchoka kushindwa huko ni msumali wa mwisho kwenye jeneza. wamuimpeach now na Epstein files zitoke kwa uwazi. Jinga sana hili jamaa. Kila kitu lenyewe ni personal tu.
 
yeah, mimi ni pro republican ...
US walichokitafuta watakipata mapema sana maana naamini uchumi wake lazima aunguke mwakani, next pandemic inaenda kuipiga US na hizo states walizochagua hao social democrats hakika watajuta na kukumbuka lakini itakuwa too late states za Democrats zinaenda kuwa na hali mbaya kiuchumi na watu kibao watamove kwenda Republiban states. Hiki walichokofanya kitawarudia kwenye maisha yao ya siku za mbele na watajutia uhuru wanaotake for granted very soon utaanza kupigia kelele za kubadilishiwa sheria ili uhuru huo wasiwe nao tena. Muslims Brotherhood wanasongesha kete taratiibu na US citizens wamelala usingizi wa pono sasa ngoja waanze kupata shida waone US yao ikiwa na chaos kama France au UK ndiyo wataelewa why Trump na conservatives wengine hawapendelei siasa za Democrats. Democrats taratiibu inakuwa taken over na Muslims Brother Hood na hawa jamaa watafanikiwa kuiangusha USA na USA itacollapse mazima.
 
Kwa wale waliochukizwa na matokeo ya uchaguzi kuna five stages of grief mtapitia

Denial โ€“ Refusing or struggling to accept the reality of the loss.
Anger โ€“ Feeling frustrated, resentful or asking why it happened.
Bargaining โ€“ Wishing things had happened differently or imagining alternative outcomes.
Depression โ€“ Experiencing deep sadness, loneliness and emotional pain.
Acceptance โ€“ Coming to terms with the loss and learning to move forward.

Muende kwa step msifikie depression, muiruke muende kwenye Acceptance
 

Kwakweli tulijua No3 mtu Mzima Trump anaenda kudondosha taulo Ukweni

Na Netanyahu kupoteza kwake
Kwasasa kwasasa wote wawili ni Washindwa

Trump muhimu leo anadai yeye hakuwa mgombea!!!

Mshangao kafanya kampeni kuwaombea kura wagombea wa Republicans
Leo anadai wameshindwa wale sio Mimi ๐Ÿค 

Trump zaidi ya muhuni wa
kawaida ๐Ÿค 
 
Uko sawa ingawa sidhani kama ni suala la unafiki labda ni la unyonge wa nafsi/roho kwa upande wake Nyerere.

Yule Mzee legacy yake au tuite tunu zake kuu (kama alivyoona yeye) zilikuwa tatu: (1) Azimio la Arusha, (2) Muungano, na (3) CCM. Ni mambo ambayo, kwa mtazamo wangu binafsi, aliyalazimisha kwa jamii ya Watanzania. Nionavyo ni mambo aliyoyashikilia sana katika nafsi yake kiasi cha kutotaka kuona yakifutika mbele ya macho yake.

Haikupita muda, Azimio la Arusha hasa kuhusu maadili ya viongozi likazikwa na Azimio la Zanzibar. Baadaye kidogo kundi machchari ya G55 likiongoza na Njelu Kasaka likaendesha kampeni kali ya kudai serikali tatu na kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika. Nyerere alirejea kwa kasi toka Butiama na kutoa hotuba kali kadhaa kupinga kundi hilo na kutishia kujitoa CCM ikibidi. Nguvu ikatumika kulizima lile kundi. Kukatulia. Muungano wa serikali mbili ukabaki ulivyo.

Baada ya kukubali vyama vingi Nyerere mwenyewe akazungumzia jinsi katiba yetu inavyoweza kumfanya Rais kuwa dikteta mbaya sana na kuumiza watu. Lakini badala ya kushughulikia mabadiliko ya katiba, akahangaika kumtafuta mgombea wa CCM anayemuamini kupambana katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Akampata Mkapa aliyemuita "Mr. Clean". Hakutaka tena kusumbuka na katiba.

Bila shaka Nyerer alikuwa anajua vizuri kuwa katiba ikirekebishwa ikawa "safi", CCM iliyokwishachokwa sana inaondolewa madarakani mchana kweupe. Hakuwa tayari kushuhudia tukio hilo katika uhai wake. Na wengi wakati ule hawakuweka msukumo wa kutosha kwa jambo hilo. Sasa majuto ni mjukuu.
 
Senate and House going blue
Wakipata Senate 67 wanamngโ€™oa Trump
67 wanazipataje wakati zimebaki 2 tu kuhesabiwa! Kati ya Senate zote zilikuwa kwenye midterm nafikri ni hizo 35 zinazoonekana kwenye bango la kuhesabu kura!
 
Kilichomwalibia Trump ni kutokuwa na uamuzi wa moja kwa moja kwenye Vita vya Iran kitu ambacho kimesababisha gharama za maisha kupanda kutokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta.
Kuhusu kudeport Alien hakuna nchi ambayo inaweza achilia watu waingie kiholela. Ila kwa vile wewe ni mhamiaji ndo maana unaongelea masuala la uhamiaji tu
 
Hizo ni ndoto tu kama ccm wanavyojifurahisha kwamba watatawala nchi hii milele.

Uislamu ni utamaduni wa kiarabu ambayo kamwe haiwezi kukubalika kwa jamii ya kizungu ambao kwanza utamaduni wao ni tofauti kabisa na ule wa kiarabu na pia isitoshe wanaamini kwamba waarabu ni jamii ya watu duni kwao.

Mfumo wa utawala katika nchi za magharibi ambao unafanya mambo ya imani kuwa ni mambo ya mtu binafsi unafanya uislamu ukose nguvu ya kuweza kuenezwa zaidi huko kwa sababu nguvu haiwezi kutumika kuineza kama ilivyokuwa zama hizo.

Ni sawa tu na hapa ambapo uislamu umebaki zaidi mijini maeneo ambayo yaliyokaliwa zaidi na jamii ya kiarabu wakati wa biashara yao haramu ya utumwa na waumini wake wakiwa hawawezi kutumia mabavu kuueneza katika maeneo mengine hasa ya vijijini kwa sababu ya dunia ya sasa hivi ilivyo.
 

View: https://x.com/TheNawazish87/status/2117975730672070890/video/1%5B/URL

Cry%20some%20more%20river!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ