Updates: Mbowe ndani ya Kanda ya Ziwa Victoria

Updates: Mbowe ndani ya Kanda ya Ziwa Victoria

The Leo mwenyekiti wa chama Taifa kamanda Freeman Mbowe yuko kanda ya ziwa Victoria inayo undwa na mkoa wa Mwanza, Kagera na Geita kanda hii pia inafahamika kama kanda ya ziwa Magharibi, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kuimarisha mfumo wa kanda za kichama chini ya CHADEMA.

Ziara hii ni muendelezo wa ziara iliyo anzia kanda ya Pwani (Dsm na Pwani), kanda ya ziwa Serengeti ambayo pia inafahamika kama kanda ya ziwa Mashariki (Mara, Simiyu na Shinyanga), ikafuatiwa na kanda ya kati (Dodoma, Sindiga na Morogoro), kisha ziara kama hii ikafanyika pia kanda ya kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara), na kanda ya Nyanda za juu Kusini (Ruvuma, Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa).

Ziara hii ya kanda ya ziwa Victoria itakuwa na vikao vitatu muhimu ambavyo ni kikao cha kamati tendaji ya kanda, kikao cha baraza la uongozi la kanda na kisha kikao cha wadau wa kanda. Leo mwenyekiti Taifa kabla ya kuanza kikao cha baraza la uongozi la kanda alipata fursa ya kufungua kongamano la vijana kupitia program ya FTP200 inayo husisha vijana wa redbrigade kutoka maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa Victoria ambapo watapata mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali, ulinzi shirikishi na elimu ya stadi za maisha.

Kesho kabla ya kikao cha wadau wa kanda ya ziwa Victoria kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara utakapo fanyika katika uwanja wa Furahisha kuanzia saa tisa mchana, mkutano huo utaongozwa na mwenyekiti wa chama Taifa na Naibu katibu mkuu Zanzabar kamanda Salum Mwalim pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa chama.

Tutaendelea kujuzana...

Akihutubia waandishi wa habari wakati wa ufunguzi Mheshimiwa Mbowe alitoa kauli zifuatazo kuhusu mauwaji ya Albino.

"...Wanao uwa wana chama wa Chadema au kuwabambikizia kesi za ugaidi na kuwatesa wanapandishwa vyeo, huku ndugu zetu Albino wanauwawa waziri mkuu analia lia bungeni hakuna hatua za dhati zimesha chukuliwa mpaka sasa huku mauwaji yakizidi kuendelea kila mara..."

"...Hatuwezi kukubali kuwa Taifa lenye viongozi wanao kubali kuona Albino wana uwawa kinyama halafu bado tukajiona tuko salama, lazima tufanye maamuzi magumu kuokoa kizazi cha Taifa hili, Haiwezekani Albino waishi kwa kuwindwa kama wanyama kwenye nchi inayo jiita huru..."

"...Bado hakuna jitihada za dhati za kukomesha mauwaji, kuna mauwaji ya vikongwe ambayo ni sawa na laana kama kuua Albino kwenye Taifa hili yamekuwa yanafanyika... Hatuwezi kuwa na Taifa lenye raia wanaofikiria kuishi au kupata ridhiki kwa kuua wanzao halafu bado serikali haionyeshi nia ya dhati kukomesha mauwaji hayo..."

Kuhusu BVR.

"...Mpaka sasa tume wameshindwa kuandikisha wapiga kura kwa ufanisi kwenye mkoa wa Njombe mji wa Makambako kwenye kata tisa, watu wana Ari ya kwenda kujiandikisha wanaamka saa tisa usiku kwenda kupanga foleni wanakaa kwenye foleni kwa muda mrefu bila kuandikishwa... "

"..hatuta kubali kuona tume ya Taifa ya uchaguzi inafanya hila za kuto kuwaandikisha watu wenye sifa kwa sababu zozote zile, tume wajue kuwa Chadema haiko tayari na haita kuwa tayari kuona wananchi wenye sifa za kuandikishwa wanaachwa kwa kuwa kuandikishwa ni haki ya kikatiba...."

Nimeshahamasisha wenzangu hapa kata ya butimba na sasa naelekea huku mahina kanyerere mkuyuni. Hakika kesho tutakua nyomi.
 
Najivunia kuwa mwanachama hai wa chadema...nahidi sitokiacha chama hata kama dr. Slaa na mbowe wakikisaliti mi ntabaki chadema...mungu nisaidie.AMEN.

hakika hicho ni kiapo kitakatifu.
 
hivi mbowe kwenye hizo ziara zake analipwa posho kiasi gani kwa siku?
 
Naipenda sana Chadema,hongera sana kamanda Mbowe kwa uongozi uliotukuka.Ila ninapenda kujua kama kwenye Ziara hiyo na Bukoba imo?
 
Taarifa hii ni murua sana mkuu Mohamedi Mtoi.
Nilisikia tar 02/03/15 atakuwa tena Ziwa Mashariki pale Shy,
nijuze kamanda maana niko mbali ndio napapasa papasa nauli ya kufikapo.
Na haka kajina "Ziwa Serengeti "kaufafanuzi kidogo!!
 
Last edited by a moderator:
Walisema Chama Cha Msimu na kwamba kitakufa kabla ya 2012 wapo wapi?

Sasa CHADEMA kipo tayari kushika Dola.

Mipango inapangika hadi raha na tunapendeza ma mavaz yetu ya chama.
 
Ahsante kwa Kazi nzuri kamanda Mbowe Mungu akubariki na akupe nguvu ya kuelimisha jamii
 
Wakuu Mnipe tenda ya kuwaletea Uniform za RED BRIGADE na hata KUbuni kama mmeshindwa mnipe pia ni Buni na ni wauzie.


attachment.php
attachment.php
 
Hapa ndio namwona prof Kitila,Mwigamba na Zitto low thinkers.
Hivi unataka kumpindua Mbowe kwa lipi wakati kama huu?
 
Taarifa hii ni murua sana mkuu Mohamedi Mtoi.
Nilisikia tar 02/03/15 atakuwa tena Ziwa Mashariki pale Shy,
nijuze kamanda maana niko mbali ndio napapasa papasa nauli ya kufikapo.
Na haka kajina "Ziwa Serengeti "kaufafanuzi kidogo!!

Mkuu.

Ni kweli ilikuwa tarehe 2/3/2015 mwenyekiti Taifa arejee tena kanda ya ziwa Serengeti au ziwa Mashariki kama inavyojulikana lakini imembidi aaharishe kutokana na sababu zisizo zuilika ila atarejea tena kukamilisha kazi iliyobaki baada ya tarehe na Utaratibu kupangwa.

Ziwa Serengeti ni jina mbadala litakalo tumika baada ya jina la "Kanda ya ziwa Mashariki" kwenye mifumo maalum ya chama ambayo inaenda kuzinduliwa leo hapa kanda ya ziwa Victoria ikiwa ni muendelezo wa kilichotokea Serena hotel mwaka jana.
 
Last edited by a moderator:
Huyo Mbowe aje jimboni kwake wapiga kura hawana maji yy anazurura huko. Huku shida ya maji inatisha, sasa yy anafaida gani kama mbunge?
 
Back
Top Bottom