UPDATE ya Matokeo ya Kura ya Maoni Jimbo la Kongwa

UPDATE ya Matokeo ya Kura ya Maoni Jimbo la Kongwa

mtotofisi

Member
Joined
Aug 24, 2020
Posts
27
Reaction score
47
Matokeo ya awali katika kata 14, matokeo yanaonyesha Isaya Mngulumi anaongoza kwenye kata zote kati ya kata 22 za Wajumbe waliopiga kura siku ya Leo.
Ikumbukwe kuwa Isaya Mngulumi alishika nafasi ya pili akitanguliwa na Hayati Ndugai. Hapa ni kata ya Kibaigwa
 

Attachments

  • VID-20250817-WA0028.mp4
    12.5 MB
Matokeo ya awali katika kata 14, matokeo yanaonyesha Isaya Mngulumi anaongoza kwenye kata zote kati ya kata 22 za Wajumbe waliopiga kura siku ya Leo.
Ikumbukwe kuwa Isaya Mngulumi alishika nafasi ya pili akitanguliwa na Hayati Ndugai. Hapa ni kata ya Kibaigwa
Da ila hali za wapiga kura zinatia huruma.sana..wana maisha.magumu sana
 
Uzuri ukipitishwa na CCM jimboni wewe tayari ni Mbunge! Miaka yote kuna geresha za uchaguzi lakini safari hii hata kugeresha hawataki!!
 
Mchakato wa kura za Maoni Jimbo la kongwa hatimaye Leo Umefika mwisho baada ya Aliyeongoza kura za Maoni awali Hayati Job Ndugai kufariki Dunia .
Isaya Mngulumi anaongoza"ushindi wa awali wa kura za Maoni Jimbo la kongwa!
Anayefuatia kwa kura ni Dr Samora Mshang'a kwa kuwa mshindi wa pili wa kura za awali katika Jimbo la kongwa!
Wagombea walikuwa 13 ambapo mgombea mmoja ambaye ndo mshindi hakuweza kufanya kampeni kutokana na kufiwa na kaka yake.
Jimbo la kongwa Lina kata 22.
Tarafa 3 Yani mlali Ina kata 10 ,Kongwa Ina kata 5
Zoisa Ina kata 7
Ukitizama wagombea wawili namba 1 na 2
Kwa kura walizopigiwa na wajumbe wa CCM wa mkutano mkuu wa Jimbo la kongwa
Kila mmoja ameshinda kwenye tarafa yake !
Mshindi wa kwanza amepata kata 12 kata 9 ni za Tarafa anayotoka yeye na kata mbili ni tarafa ya Zoisa na kata Moja tarafa ya Kongwa .
-Mshindi namba 2 yeye anatoka kata ya Sejeri tarafa ya Kongwa yenye kata 5 .Ameshinda kata 4 ,huku Tarafa ya Zoisa ameshinda kata 3 na tarafa ya mlali kashinda kata Moja .
Ukitizama hapo utagundua kura zilikuwa zinapigwa kwa ukanda!,
Kwa matokeo ya Jumla ya kura zote mshindi wa kwanza anaongozaa na kwa matokeo ya tarafa mshindi wa kwanza anaongoza tarafa Moja tu ya mlali .
Kwa matokeo ya kata Wingi mshindi wa kwanza anaongoza

Kwa matokeo ya Ushindi wa Tarafa Dr Samora anaongoza tarafa ,2 yani tarafa ya Kongwa na Zoisa .
 
Weka hapa jedwali la matokeo ya kura za maoni, uchaguzi wa ndani CCM katika jimbo la Kongwa
 
TATHIMI YA KURA ZA MAONI ZA UBUNGE NDANI YA JIMBO LA KONGWA

Jumla ya kura ni 9801
Fadhili C Bwagalilo. 96 sawa na 0.98%
Robi R Gairigi 97 sawa na 0.99%
Baraka D mkanwa 120 sawa na 1.22%
Michael G Chidaga 160 sawa na 1.63%
Dr Rose Mbijima. 164 sawa na 1.67%
Ngaya D Mazanda 167 sawa na 1.70%
Balozi Mbennah. 181 sawa na 1.85%
Philip E Chiwanga 210 sawa na 2.14%
Henry Msunga 212 sawa na 2.16%
Dr Simon Ngatunga 508 sawa na 5.18%
Elias Mdao. 616 sawa na 6.29%
Dr Samora mshang'a 2834 sawa na 28.92%
Isaya Mngurumi. 4436 sawa na 45.26%
 
Back
Top Bottom