Bramo
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 13,230
- 10,201
MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma tatau.
"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili"alisema Sabas.
Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo.
Lema alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.
Mbune huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.
My Out Look:
Nazidi kuyasadiki Maneno ya Rafiki yangu SSP Chuwa kuwa Tatizo sio Mulongo.
Yeye ana execute to Matakwa ya Mkulu Dhidi ya Lema.
Ile Issue ya Lema kumpa Live Mkulu kuwa analea Udini imemchoma sana Mkulu.
Rafiki Yangu SSP Chuwa Akaongeza, "CCM ni Wepesi Mno na Weupe Suala linapofika Mahakani"
Wao wana Mamlaka na Fedha, Lema ana Mungu
===================
Kinachojiri Mahabusu

MODS naomba muache Thread hii,nitaitumia kuleta Updates za kinachojiri:
Salaam WANAJF,
Taarifa za uhakika muda huu kutoka Mahabusu kituo cha polisi Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha Mh.Godbless Lema ameendelea kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji alipopelekewa kifungua Kinywa na ndugu zake asubuhi hii
UDHALILISHAJI
-Mke wake alimpelekea Mswaki na Dawa ya meno lakini polisi wamekataa kabisa kwamba hairuhusiwa.Kama mjuavyo Mswaki hauruhusiwi kuingia nao ndani mahabusu kwa hiyo Lema alikua ametoka kwenye chumba cha mahabusu na kanuni hazimfungi au kumzuia kutumia Mswaki katika kujiweka katika mazingira mazuri kiafya.Hili ni jambo la kawaida kwa mwananchi yeyote na ni haki ya mahabusu
-Pia wakati huo huo askari walianza kuikagua chai aliyoletewa kwa kutumia fimbo aliyokua nayo jambo lililomchukiza Leman a kuhoji hii humiliation ni ya nini?Kama vile haitoshi askari akaendelea kumshinikiza kuwa wamempa dakika mbili za kunywa chai kitu ambacho kimezua mabishano na Lema akagoma na kudai kwamba ni lazima sasa Mwanasheria wake aje kwanza amfafanulie kama kweli haki zake hazijakiukwa.
-Pia ameletewa magazeti na akiwa ameshika gazeti la Mwananchi askari polisi alimnyang'anya na kumwambia ahairuhusiwi hata kupata taarifa zozote
Lema amemuta Mwanasheria wake
KESI YA MAUAJI INASUKWA KUTUMIA UJUMBE ALIOTUMA RC
Wakati huo huo kuna taarifa nyeti kabisa na za uhakika kwamba muda huu jeshi la polisi likishirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wanafanya jitihada za kubadili uamuzi wa kumfungulia kesi ya uchochezi kama nilivyoweka hapa jana baada ya kuongea na mwanasheria wake jana na sasa wanataka kumfungulia kesi ya mauaji kwa kuzingatia ujumbe ule wa simu uliotumwa na mkuu wa mkoa.
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu na JF kitakua chombo cha kwanza kabisa kuhabarishwa yanayojiri.Katika muda wote huu nitalinda heshima ya JF kwa habari za ukweli na uhakika kama nilivyofanya nilipothibitisha taarifa za kufuatiliwa gari ya Dr.Slaa ambazo zimekuja kuthibitishwa baadae kuwa ni kweli.
CC: Moderator, Paw, PainKiller, Invisible na WanaJF wote