Update: Lema kufikishwa Mahakamani Jumatatu

Update: Lema kufikishwa Mahakamani Jumatatu

Akili yako ndio imeishia hapo ?? Kweli tuna kazi kubwa sana ya kufuta ujinga hapa nchini .

Mnafuta ujinga kwa kufuata theory za Sheikh Yahya na mawazo ya Prof.maji marefu.....
 
Wapiga kura wa Arusha mjini,you have to fight for your MP!

Mkisubiri Mungu awasaidie mnajidanganya.
 
Wafata mkumbo wa CDM hamuwezi kunielewa hata siku mmoja maana vichwa vyenu vimejaa viroba .

Bado ni tunaitwa binadamu....sisi ubinadamu na haki za binadamu ndio nguzo kuu...nyie mnaowatenga watu kwa sababu ya wanachokula,wanachokunywa,wanachofanya endeleeni!
"Ubinadamu kazi"
 
Badala ya mimi kutafuta hela niisaidie familia yangu eti nikaandamane . Huu ni upuuzii uliotukuka . Wajinga ndio wafuate mawazo yako .

Upumbavu wako umwishi Lumumba kwenye buku 5 unazo lipwa
 
Yule first lady mwalimu alimchota mpiga muziki yule wakizaire. Yule msanii akatunga wimbo wenye jina la mwalimu. Of course alikuwa bado hajawa first lady. Ushuhuda unaonyesha mwalimu akimpatia kijana zawadi keme kem hasa akienda kwenye show zake. Fastjet akiwa anakula bata mitaa mbali mbali mama akaamua kumega kijana.

Habari zikamfikia mwenye mali, bahati akawa rais na kama utani vile, familia yote ikafungwa maisha. Huyu ndie fastjet aliyeletwa kwetu na sisi wenyewe. Nakubaliana na wewe mkuu, presida ana chuki, na visasi zaidi ya Boko haram.

Naitwa mdudu , mtu mwenye kuishi kwenye nyumba pekee yenye choo ndani kwa ndani.

"KAZI YA MOYO NI NINI, KUISHI AU KUFA'' HAAHAHH napenda kuimba leo jamani. Muungano etii.

Salima ooh salima ooh. ULINIDANGANYA , NIKAKUPENDA WEWE , OOH SALIMA WANGU EEH,,,,,,

Mkuu, Kwenye RED and Bold, Kipindi hiko kwani alikuwa na Tabia za Ki Fastjet Fastjet?
 
KUKAMATWA KWA LEMA: MKUU WA MKOA ARUSHA ALISTAHILI KUZOMEWA
Nimefuatilia kwa karibu suala la kuzomewa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha na kitendo cha “kuvamiwa” kwa mheshimiwa Lema na kisha kuwekwa ndani. Nimetazama pia video inayoonyesha jinsi mheshimiwa Lema alivyofanya juhudi kubwa sana za kutuliza hasira za wanachuo wa Uhasibu waliokuwa wakijiandaa kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa.
Nimemtazama pia mkuu wa mkoa (kwenye video) jinsi alivyoingia pale chuoni na kutoka, kisha kuongea na wanachuo. Kwa mtazamo wa haraka haraka, huyu mtu hana sifa ya kuwa kiongozi wa watu.
Kwanza, alivyoingia na kuondoka kwa kisingizio cha kukosa kipazasauti na “kukerwa” na kelele (sio zomeazomea) za wanachuo (wenye uchungu na majonzi) ni ushahidi wa wazi kuwa amelewa madaraka. Yeye alitarajia nini kutoka kwa watu wenye ghadhabu? Alitarajia kupigiwa makofi na kuimbiwa nyimbo na utukufu? Kama ilivyo kawaida ya viongozi wetu.
Pili, ikafuata zomeazomea. Kuzomea ni dalili kuwa wanachuo hakuridhika na maongezi yake. Na kwa fikra zake za “kizamani”, akadhani watanzania wa sasa ni wale wa “kale” wanaoabudu viongozi hata kama ni “mbumbumbu”. Kwa hiyo matarajio yake ya kubudiwa yakazikwa papo kwa papo. Yeye hakupaswa kuogopa wala kushangaa kuzomewa. Lakini kwa kukosa kwake busara kaligeuza suala dogo kuwa kubwa sana. Si kwa manufaa ya wanachuo wala taifa, ila kwa manufaa ya “utukufu” aliouzoea.
Tatu, anatumia neno “serikali” kuonyesha kuwa yeye yuko juu ya kila kitu. Ati anawaamia wanachuo kuwa wameiita “serikali”, na kisha baadaye anatumia neon hilo kwenye ujumbe ambao Lema anasema alimtumia: “…nitakuonesha kuwa mimi ni serikali…” Kwa mtazamo wake serikali ni wale walioko madarakani. Na kwa kwa mtazamo huo huo wa “kikale”, serikali lazima iabudiwe kama Mungu-mtu. Pengine ni kwa kuwa inashikilia vyombo vya dola ambavyo tunshuhudia vikiamrishwa kutekeleza matakwa ya hao wanaojiita “serikali”.
Haikubaliki, na wala haikutarajiwa, kuwa kuzomewa kwa mkuu wa mkoa (aliyeshindwa kuongea na wanachuo) kukawa chanzo cha kuvunjika kwa amani Arusha. Nasema hivyo kwa sababu sioni kosa lolote alilofanya Lema lenye kuhidhinisha “uvamizi” nyumbani kwake. Kwa kuwa huyu ni mwakilishi wa wananchi, sitegemei amani iwapo wananchi wa Arusha wanainuka kumtetea mbunge wao.
Kwa hakika, hata Lema asingekuwa shupavu na mvumilivu, hata yeye angeghadhibika kwa kuwa kelele za wanachuo ziliendelea akiwa anaongea. Kwa kuwa yeye ni kiongozi wa watu (sio mtawala) alifanya juhudi kuwatuliza ili walau wapete ujumbe wake wa amani. Hakuwa na kipazasauti na wala hakusema wanachuo hawana nidhamu ati kwa kuwa wanapiga kelele!!! Hapo ndipo tunapotofautisha ya “kiongozi” na “mtawala”. Mtawala anakuja na askari wake na kiburi cha kuwa analindwa na hapaswi kupata misukosuko! Kwake yeye misukosuko ya kawaida (kama kuzomewa) ni kuvunjiwa heshina na kudhalilishwa hadhi yake ya “utukufu”.
Isitoshe, nguvu iliyotumiwa na polisi pale chuoni (kurusha mabomu ya machozi) ilikuwa kubwa kupita kiasi. Pengine hiyo ndiyo tafsiri ya neno “serikali” analotumia mkuu wa mkoa kuonyesha mabavu yake kwa raia wanaodai haki. Hata hivyo hatumshangai kwa kuwa anaendelea kuuonesha umma wa watanzania jinsi “serikali” yao ilivyo. Ndivyo ilivyo na itaendelea kuwa hivyo hadi hapo watanzania watakapogundua kuwa wao ndio hasa “serikali halisi”.
Hizi ndizo dalili za kuanguka kwa “serikali”. Hata Africa Kusini, wakati wa kudai haki dhidi ya ubaguzi wa rangi “serikali” zilikandamiza raia na hata kuwaua. Lakini ukandamizaji siku zote haushindi nguvu ya watu kudai haki. Waafrika Kusini waliishinda “serikali”. Tuliyaona hayo Yugoslavia, Libya, Misri, na kwingineko. Tujiandae kuyaona pia Tanzania.
 
Dah, Lema again. Kwa ile video clip niloiona mtandaoni akiongea na wanachuo, kama wanasema kachochea kweli mgomo basi ni Mungu tu anayeweza kutenda haki wala si mwanadamu!!!!
 
Ukweli watu wengi hawamwelewi kamanda Lema vizuri. the man rocks. He has untold powers.
 
Hili suala halitawaacha salama.Haki isipotendeka basi serikali ijiandae kukabiliana na nguvu ya umma
 
amani ya nchi inavunjwa na viongozi wenyewe, wanazidi kupandikiza chuki kwa jamii. Lema ni mwiba kwao, ipo siku kitanuka.
 
Badala ya mimi kutafuta hela niisaidie familia yangu eti nikaandamane . Huu ni upuuzii uliotukuka . Wajinga ndio wafuate mawazo yako .

watanzania si wajinga kama unavofikiri sindo maanda t aliposikia mtoenje askari alitii amri bila shuruti
 
Hivi mamlaka inapokuwa haitendi haki unaishitaki kwa nani?
 
Badala ya mimi kutafuta hela niisaidie familia yangu eti nikaandamane . Huu ni upuuzii uliotukuka . Wajinga ndio wafuate mawazo yako .

una akili mbili tu.ya kuvalia nguo na kuvukia barabara.hata hivyo mapinduz huwa haya letwi na watu wanafik kama ww.we lala ndani na mkeo si tipige kazi
 
Hujui kuwa kama system ikiwa nzuri hata hauitaji kutoa jasho ili kufanikiwa? . Jiunge na wenzako uboreshe maisha yako na ya kizazi chako.Hii ni kama uko sincere na wewe siyo imposter!
Usimdanganye wewe. Hakuna mafanikio yanayokuja kupitia vyama vya siasa. Wote ni waganja njaa tu
 
Acheni sheria ifuate mkondo wake jamani. Kama walimrudishia ubunge, ni wazi kuwa kama hana kosa mahakama itamuacha huru.

Huwezi kufanya Tanzania kama Libya; ni cases mbili tofauti. Kule kulikuwa na dikteta lakini Tanzania si unaona bhana, Lema amekamatwa na atafikishwa mahakamani J3 sio ikulu!
 
Back
Top Bottom