upandishwaji wa mishahara kwa watumishi walio na kiwango cha degree moja!

Hivi hiyo 1m unaongelea gross au net??Kama ni gross,basi kazi ipo.....!!!!
 
Ni kweli tumepandisha mishara mpaka 1m,pia na kodi imeongezeka hivo katika 1m tutakata laki 6.
 
Ni kitu ambacho hakiwezekani kwa serikali hicho ni kiwango kikubwa mmno kumlipa. kama wakifanya hivyo itakua vizuri itasababisha watu wengi wasiache kazi serikalini na watafanya kazi kwa uhaminifu pia rushwa ndogo ndogo zitakwisha huduma kwa wateja maofisini zitaboreshwa kwa kiasi kikubwa.
 
Mimi naunga unga tu mjini hapa na hiyo mishahara, hapa nawaeleza ukweli wadogo zangu,,

Watanzania kibao ni wezi as mishahara tunayolipwa ni almost hela za kula tu, but watu wanajenga, magari wanaendesha na mwengineyo, ukikua utayaona ndugu,,, kiukweli asilimia 80 ya watanzania ni mafisadi, ukilinganisha mshahara na mali zao haziendani.

Kiukweli ukipata kazi ya mashahara may be 1m mnayoisema na hiyo kazi haina ujanja ujanja wowote wala marupurupu yeyote ni balaaa... Maana pesa ya Jk haina nguvu kabisa. Nawakaribisha kwenye corporate world mje mjioneee hali ilivyo

daaaah kama hali ndo ilivyo bora kufungua kanisa
 
ila maisha kupanda yamepanda kwa watu wote; inakuwaje tena makamishna na wakuu wengine wenye mishahara mizuri wazidi kuboreshewa wao tu na kuwwasahau watz watumishi wa kada za kawaida? nadhani ndo walistahili kuanziwa ktk kupandisha mishahara huku
 
Na imani haujakua bado, na ni bado tegemezi, mi nimeuliza kama huo mshahara ni mkubwa? Na sijasema kama mshahara wa laki 2 nao ni mkubwa, but kwa kukusaidia tu mdogo wangu mshahara wa million 1 ni wa kawaida sana na bila ujanja ujanja au kusaidiana na mwenzako hutoki kwa huo mshahara, kwa kukadiria kama 1m gross net salary inakuwa lak 7, sasa igawe kwenye kodi, nauli, chakula na mengineyo kisha unipe jibu,, wakati natoka chuo nilikuwa na mawazo kama yako but ukweli nikaja kuujua hali ilivyo, hiyo ni hela ya ndogo sana kwenye majukumu labda uwe mwizi ofisini

Kwa hiyo unataka kusema nini? Kwa sisi walimu hata mianya ya kuiba hatuna tukisomesha wadogo zetu na kujenga ni mafreemason au?
 
Back
Top Bottom