Upandikizaji wa kichwa sasa unawezekana.

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,617
32,723
150226150040_kichwa_640x360_bbc_nocredit.jpg
Upandikishaji wa kichwa cha binaadamu hadi katika mwili mwengine sasa unawezekana kulingana na wanasayansi
Unaposikia habari hii utadhani ni maudhui ya filamu ya kutisha ,lakini wanasayansi wanaamini upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwengine huenda ukafanikiwa.

Madaktari watazindua mradi huo katika kongamano wakati wa msimu wa joto ,kwa lengo la kuanzisha utaratibu huo mnamo mwaka 2017.

Mtu atakayeongoza mpango huo ni daktari raia wa Italy Sergio Canavero kutoka kundi moja la wanasayansi mjini Turin.

Anaamini kwamba upandikishaji wa vichwa vya watu utawasaidia wanaosumbuliwa na magonjwa ya misuli na saratani.

Baada ya kutoa wazo hilo mnamo mwaka 2013,daktari Canavero anaamini vikwazo vikuu vya upasuaji huo vimekabiliwa ,kulingana na ripoti mpya ya wanasayansi.

Vikwazo hivyo ni pamoja na usimamizi wa uti wa mgongo kuingiliana na kichwa kipya pamoja na kuhakikisha kuwa kinga ya mwili haikikatai kiungo hicho kipya.

Daktari Canevaro alichapisha taarifa iliokuwa na nadharia kuhusu vile anavyoamini upasuaji huo unaweza kufanyika.

Chanzo: BBC
 
Nisichokielewa katika nadharia hiyo ni kwamba: Katika kukamilisha nafsi ya mtu, moyo hutegemea ubongo.
Sasa hapo tuseme, mwenye kichwa cha mwili 'A', kikachukuliwa kupandikizwa mwili 'B', je mwili 'B' utakuwa ni nafsi ya mwili 'A' au mwili 'B' utaendelea kuwa nafsi ya mwili'B'?
Maana hapo ni utata!
 
Hii kitu niliona kwenye series ya Netflix inaitwa altered carbon, wao walkua hawaamishi kichwa bali ni kitu flani kinaitwa stack kina store memory za matukio yote uliofanya, so ukifa au ukiwa huutaki huo mwili wako wao wanaamisha hiyo stack kwenda kwenye mwili mwengine.
 
Nasubiri kuona binadamu hybrid; kama walivyo ngombe na kuku.

Binadamu hybrid F1 inasemekana atakuwa na akili nyingi na ataishi miaka zaidi ya 200.
 
Mkuu nikwel hizi tafti wanafanya ili kuwaongezea hawa great minds mda mrefu wakuishi sasa hawa donors wa hio miili tunawapataje
labda kuna watu watajitolea maisha yao lakini familia zao zitalipwa pesa ndefu. unakuta mtu amekata tamaa na maisha anaona bora yeye atangulie ili wanaobaki wale maisha mizuri.
 
Mkuu nikwel hizi tafti wanafanya ili kuwaongezea hawa great minds mda mrefu wakuishi sasa hawa donors wa hio miili tunawapataje
Hakuna donor wa hiari hapo. Nadhani inachukuliwa miili ya wahanga wa vifo vya kunyongwa ama vifo vinavyofanana na hivyo.
Sasa kichwa 'me' kikapata donor wa mwili 'ke' hapo inakuwaje!
 
Nawaza,kichwa cha mtu kama Steve Job kingepandikizwa kwa mwili wa kilaza sijui kungetokea nini ..?
 
Back
Top Bottom