Upande wa pili wa Mizengo Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upande wa pili wa Mizengo Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Jan 13, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF
  Nimekuwa nikimsikiliza waziri mkuu Pinda kwenye hotuba zake na anapotoa hoja mbali mbali, nilichogundua ni kwamba waziri mkuu wetu mara nyingi huwa nachagua maneno ambayo yatamfanya abaki neutral kwenye hoja husika, asiiudhi serikali na asiwaudhi wananchi, anataka kufurahisha pande zote, hili haliwezekani kwa siasa za nchi yetu kwa sasa kwa madudu yanayoendelea, na hili ndilo limemfanya Pinda ambaye alikuwa kipenzi cha watu baanda ya kuchaguliwa, kupoteza kabisa ile sifa yake kwa sababu ameonekana ni mnafiki na si mtendaji.

  Ni mtu ambaye siku zote anahakikisha analinda kibarua chake hata ikibidi kwa kutoa machozi mbele ya camera.

  Mfano mmoja wa unafiki wa Pinda ni kauli yake kuhusu malipo ya Dowans, nakumbuka yeye alisema, suala la Dowans ni gumu, na wanasubri hukumu isajiliwe mahakama kuu ya Tanzania ili wajue kama ni halali basi Dowans walipwe. Tangu wakati huo hajaongea kitu tena hata baada ya kauli za kutaka Dowans ilipwe kabla ya kesi kusajiliwa mahakamani kuu. Ukimuuliza leo Pinda atakwambia yeye hakusema ilipwe, atasema "nilichokisema tusubiri hukumu isajiliwe mahakama kuu tuangalie uhalali wake" na labda atakuja na blabla nyingine nyingi ili tu aonekana mzuri kwa wananchi kwamba hajatamka solidly kwamba Dowans walipwe lakini pia aonekane hapingani na serikali kwa sababu hajasema Dowans wasilipwe. Huyu ni mnafiki mkubwa. Huwa simwelewi.

  Vile Vile mheshimiwa Pinda aliwahi kukataa gari mpya aliyonunuliwa lakini akakubali apewe mtu mwingine, yaani yeye aonekane hapendi anasa za magari ya kifahari lakini anaacha wengine wayatumie, huu nao ni unafiki ili aonekane mzuri kwa wananchi lakini asiwaudhi wenzake. Yeye kama waziri mkuu hapaswi kuwa peke yake anakataa magari bali apige marufuku ununuzi wake.

  Mh Pinda kuna gazeti moja la kila wiki aliandikwa kuwa anamiliki hisa kwenye kampuni ya usafirishaji abiria ya Sumry based in Sumbawanga, sijasikia akikanusha hivyo inawezekana ni kweli ana hisa, lakini alipotaja mali zake hakusema kuhusu hisa hiza kwa hiyo alitupiga changa la macho?

  Mh Pinda soma alama za nyakati, watu siku hizi akikuangalia anajua mpaka unachowaza, kutafuta huruma za wananchi kwa kujiita mtoto wa mkulima au kulia mbele ya camera hakuwasidii watanzania.

  Hili la Arusha nalo hatujakusikia zaidi ya kusoma kwenye magazeti kwamba sijui umwemweka kiti moto Mwema, tunataka ufumbuzi wa jambo hili mapema, kitu ambacho waziri mkuu mtendaji angeshafanya. Angalia usijekukaa muda wote na ukaondoka hapo bila cha kukumbukwa, utachekwa kwa kuwa hata Lowasa na skendo zake zote pamoja na kuhalalisha uwepo wa kampuni ya kutuibia ya Richmond lakini kwa kipindi kifupi alichokuwa waziri mkuu alihamasisha ujenzi wa shule na zinaonekana, so far wewe mizengo umetufanyia nini unachojivunia?

  Mwenye maoni kuhusu Mh Pinda anakaribishwa. Naomba kuwakilisha.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  dah
   
 3. k

  katiba Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatuna PM...mbona hilo linajulikana siku nyingi..hii nchi haina viongozi kwa jinsi mambo yanavyokwenda..kama ni gari basi dereve na tingo wameruka, gari linaenda lenyewe, tunasubiri kupinduka tu..Inauma sana! we need change!
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Mtoto wa mkulima huyo - neither East (?) nor West (?)!

  Practically yupo neautral na ndiyo maana kila mara statements zake uanza na neno "Mimi binafsi nadhani...." na sio "Msimamo wa Serikali ni ..."
   
 5. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Achague moja he is with us or against us. Mi kwa upande wangu najua yeye yuko pamoja na mafisadi anatuzuga tuu, kama anataka ani prove me wrong aonyeshe kwa matendo! Bora fisadi (lowassa) unayemjua kuliko yule usiyemjua!
   
 6. m

  mzambia JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  pinda jamani mbona ni msanii sana.
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  Simple man or Simplified man?

  [​IMG]
   
 8. Baiskeli

  Baiskeli JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ukweli hakuna jambo la kukumbukwa mpaka sahii zaidi ya kulia hadharani . hana uwezo wa u-pm, ok sio fisadi nini unachotusaidia wananchi? kuwalipa downs? bei ya umeme? bei ya gesi? tena mnafiki sana anajificha kwa kujiita mtoto wa mkulima. yupoyupo tu.
   
 9. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mnafiki bora dume la kazi lowasi
   
 10. G

  GAMA LUGENDO Senior Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  As a human being, prime minister Pinda is a polite man, and i like his politeness and humble behaviour.As far as his leadership capability especially since he became the premier, I can frankly say that he evasive in handling controversial public affairs,also not strong and tough in decision making.In short he is indecisive.
   
 11. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  simplified
   
 12. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,043
  Likes Received: 3,950
  Trophy Points: 280
  on point umeuma bila kutema
   
 13. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Haiwezekani kuwa na na kiongozi safi kutoka ccm,pinda sio msafi hata chembe kwenye fomu za maadili ya viongozi,wanapaswa kutaja mali pamoja na za watoto,mke,pinda hakutaja mali za mtoto wake wa kike ambaye kwa sasa ni MP viti maalum,huyu bintiye pinda alihonga uvccm arusha zaidi ya milion kumi,wakati wa mchakato ndani ya ccm,je alipata wapi ela nyingi hivi mtoto wa mkulima?
   
 14. m

  moma2k JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Namuunga mkono na miguu Edward Lowassa:
  -Lowassa ni mchapa kazi
  -Mpenda elimu
  -Muwazi
  -Upande wake unafahamika
  -Mpenda maendeleo. siyo bla bla
  -Ana uchungu na nchi(ushauri mzuri ktk tukio la Arusha)
  Let me tell you the truth: Kama tunataka maendeleo ya kweli katika nchi Tanzania, mwaka 2015 tumchague Edwald Lowassa kuwa Raisi wetu wa Tanzania. Lowassa Edward our next President, whether you like or not, he is placed to win the Presidency 2015. Let us pray for him.Atatufaa sana! Akina Pinda hawaeleweki misimamo yao, ndumila kuwili.
   
 15. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwenye mojawapo ya threads zangu nimewahi kuuliza uhalali wa Pinda kujiita mtoto wa mkulima. Nilijadili na kuhitimisha kuwa hilo ni jina lenye lengo la kukudhi matakwa ya kisiasa. Kinachoonggelewa kwenye thread hii ni ukweli mtupu. Mwandishi amejitahidi kuonyesha kwa ufasaha sura halisi ya Pinda ambayo kwa neno moja tunaweza kumwita ni MNAFIKI. Anapoongea majukwaani anahakikisha kwamba haudhi upande wowote iwe serikali au wananchi. Yeye anacheza na mdomo tu. Matokeo yake, leo hii ukimuuliza mwananchi yeyote mitaani kwamba ni jambo gani specific alilofanya Pinda kiasi cha kumkumbuka, atakwambia hakuna.

  Kwa ujumla, kwa sasa nchi hii haina waziri mkuu.
   
 16. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  HAta mimi siipendi tabia ya unafiki ya Mizengo Pinda, tunahitaji mtendaji mkuu wa serikali sio mtu mzima anayelia hovyo bila kuchukua hatua za hakika, kama hayawezi madaraka si akae pembeni, kwangu mimi huyu ndiye Waziri Mkuu mbovu kupita wote katika historia ya Tanzania, hana legacy yoyote utendaji wake uko very weak, tena ni mtu aliyekaa ikulu miaka mingi, hana jipya!
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
   
 18. k

  kiche JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Chonde chonde udhaifu wa pinda usijeukasababisha kumpa mbwa kazi ya kulinda nyama,lowasa tumwache aendelee na mishemishe zake,kwenye urais hafai hata chembe ulka yake kiutendaji hafai achilia mbali ufisadi unaomwandama.

  Kuhusu pinda huyo ni mnafiki mkubwa na hana msaada kama waziri mkuu,majibu yake siku zote yanaanza kama ifuatavyo mimi nadhani..................,tutakuwa na waziri mkuu wa kudhani mpaka lini?nachowaomba msitegemee jipya toka kwake hata kidogo kama waziri mkuu,haiwezekani maelekezo yake hayafuatwi kila siku na watendaji wake,mfano suala la ununuzi wa magari ya kifahari alikataza muda mrefu lakini mpaka leo yanaingia,mbona rwanda na kenya waliweza?kwanini tanzania ishindikane?huo ni mfano mmoja tu wa utendaji wake kama waziri mkuu.
   
 19. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  amefanywa na wala hayuko hivyo

  huyu ni masikini ,jinga ,takataka,hana maana wala msimamo hana sijui alisoma wapip hiyo sheria isiyompa misimamo,kifuuu tuu huyu hana lolote analinda hal=ki za mafisadi ilhali hawampi hata shilingi,amengangania tulipe DOWANS wakati hawampi hata kumi shenziiiiiii
   
 20. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Re: Upande wa pili wa mizengo pinda

  Namuunga mkono na miguu Edward Lowassa:
  -Lowassa ni mchapa kazi
  -Mpenda elimu
  -Muwazi
  -Upande wake unafahamika
  -Mpenda maendeleo. siyo bla bla
  -Ana uchungu na nchi(ushauri mzuri ktk tukio la Arusha)
  Let me tell you the truth: Kama tunataka maendeleo ya kweli katika nchi Tanzania, mwaka 2015 tumchague Edwald Lowassa kuwa Raisi wetu wa Tanzania. Lowassa Edward our next President, whether you like or not, he is placed to win the Presidency 2015. Let us pray for him.Atatufaa sana! Akina Pinda hawaeleweki misimamo yao, ndumila kuwili.

  kha chonde chonde mama! kumbuka hii nchi ina watu zaidi ya 42 million!! yaani ushasikia rotten egg smell unauliZa hivi hii ni HYDROGEN SULPHIDE?
   
Loading...