Michelle
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 7,621
- 3,513
Naona sasa tunaanza kushabikia uozo. Ni kweli pinda amekuwa so passive kiasi kwamba amekuwa mnafiki. Anaongea tu maneno ambayo hayaelekei kutusaidia zaidi ya kupuliza kidonda ili mtu asisikie maumivu wakati huo hata kama kisu kinazidi kuchimba. Hapa yeye hajashika kisu, anawapulizia wengine. Pamoja na hayo, huyu Lowassa hatutaki kumsikia kabisa. Ufisadi ambao amehusika nao unatosha kabisa na ameshakuwa tajiri. Hatumhitaji, nina hakika tutapata rais bora kuliko hawa wanaotunyonya na kutuonea kila siku.
Sidhani kama ni kushabikia uozo,kuliko mtu dhaifu kama JK,asiye kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi,ambaye tunajiuliza ni president au celebrity kwa kuwa hatuoni analofanya,nafikiri tu bora na huyo mwizi ambaye anajua tunamjua,yeye na rafiki zake.Suluhisho la hawa watu ni katiba na sheria zinazowabana na kuwataka wawe accountable na wanayoyafanya na mali wanazomiliki......CHADEMA watupe mtu tough,si hatuna neno tutamuunga mkono but not just anybody!Kama kuna mmoja alisema anafikiria kugombea....akiwa huko aliko tayari ana kashfa sijui akiwa Rais itakuwaje..............lol