Malsa, hebu niambie sisi tulijifunza nini kwa hawa wenzetu
Zambia, maandamano (sio ya vyama vya siasa) kupinga kupanda kwa bei ya mkate
Uganda , "walk to work"
Congo, Maandamano na Mishumaa ya usiku
Nigeria, Maandamano kupinga, ongezeko la kodi kwenye mafuta
Halafu angalia Tanzania sasa
Mgao mkuu wa umeme, watu kimyaa
Kupanda kwa bei ya mafuta (gasolin), watu kimyaa
Kupanda kwa gharama za maisha, watu kimyaa
Kupanda kwa mafuta ya taa, watu kimyaa
Kupanda kwa gharama za umeme, watu kimyaaaa
Kuporomoka kwa thaman ya shilingi watu kimyaaaa
Matumizi mabaya ya rasilimali na ufisadi watu kimyaaa
Na hapa niwashukuru CDM kwa kuonyesha njia, lakini maandamano yale yangekuwa na nguvu zaidi kama yasingekuwa na chembe ya siasa (si mnawaona MAT)
Tatizo watanzania hawaoni uhusiano wa mambo haya na serikali iliyapo madarakani. Until then, mambo yatazidi kuwa magumu sana
Bora umeliona hilo Mkuu,Watanzania sisi ni waoga.
Kuna mtua aliwahi kuniambia TANZANIA NA INDIA NDO NCHI PEKEE AMBAZO WANACHI WAKE NI WAOGA KAMA NINI, INDIA HUWEZI KUTA MAANDAMANO WAHINDI NI WAOGA SANA, NA BONGO NDO HIVYO HIVYO,
BACK TO THE POIN
1. Hili la maisha kuwa magumu nalo ni fundisho kwetu, wewe unazania ni kwa nini nchi za ulaya population yao inashuka? Mfano Urusi imeamua kutoa motisha kwa wamama watakao jifungua serikali itale, ni kwamba wazungu baada ya maisha kuwa magumu wameamua hata kuzaa hawazai tena, mzungu anazaa mtoto mmoja basi.
2- SAA ZINGINE SISI WENYEWE NDO TUNAFANYA MAISHA YAWE MAGUMU WALA SI SERIKALI,
-SIMU YA MKONONI- Wazungu hawawezi kupigia mtu simu kama hana ishu ya muhimu sana na kama ni swala la ndugu wanasalimiana kila hata baada ya miezi 3 na siku hiyo wanaweza ongea kwenye simu saa nzima.
Population inaingiaje kwenye mfumuko wa bei?
Mie nimepanga bajeti ya mwezi mzima lakini kila nikienda dukani nakuta bei imepanda,tatizo ni system na sio wananchi!
Ni kweli unalolizungumza mkuu,hapa inabdi kuandamana.kukaa kwentu kimya ndo kunasababisha kuzidi kuumia.Inabidi wananchi tuandamane kushinikiza serekali ijali wnanchi wake na gharama za maisha zishuke.Kila kitu kipo juu mishahara midogo tutafika wapi?Jamani watanzania tuamke tuache uwoga gata middleeast changes zimetokana na wanachi wenyewe. SS tunaumia ila kuna watu wanachezea pesa hapa hapa bongo.
Mkuu napingana na ww kwenye hili,wazungu wenzetu wameshaendelea sana na sio ugumu wa misha ambao umewafanya waache kuzaa.Huko ulaya na chi nyingi zilizoendelea vyakula na vitu kama gas ni rahisi sana.Hapa kwetu serekali inapiga kampeni ya watu kunywa maziwa wakti mtanzania wa kawaida kunywa maziwa ni issue.Yaani hapa kwetu kula chakula kitu ni issue ajili ya bei zilivyo juu. Ss hivi sukari bei ni tsh 2300 kilo moja,kila bidhaa unayoiona ipo juu,dagga nazo kilo mpka elfu nne zile za mwanza na za kigoma ndo hazishikiki je mtanzania akimbilie wapi?Nina msupport mchangia mada pale anaesema watanzania ni waoga,uwoga unatupeleka pabaya kwani kila siku tunazidi kuumia tunanyamaza kimya.
Wanachi inabidi tusemame na kuihinikiza serekali itazame jambo hili kwa kina,kama gas tunaweza kuzalisha hapa kwetu kwa nn inunuliwe kutoka sehemu ingine?kama gas bei kubwa basi acheni tutumie mkaa tupange namna yakutunza mazingira na mkaa tutumie na sio kukutoa kwenye mkaa wakati huko tunakokimbilia hamna wepesi.
niliwahi kusema hapa siku moja, tunahitaji kuingia zaidi ya barabarani. Nkuu wetu ambaye tulimtegemea walau akemee na kutoa mwongozo yuko kimya, na siku akiongea utamsikia akilalamika. Mie nahisi tunahitaji kufanya jambo amabalo, hata hao wakuu wenyewe hatawalisahau na watakapolikumbuka, watakumbushwa kuwa hii nchi ni yetu sote na sote tuna haki ya kuishi kwa neema. By the way, mie naona tunaongea sana na keyborad with no sparks, sie ni kama majibwa yanayobweka saana, bali hayana meno ya kung'ata. Ni wazi kuwa kuorganise maandamano ndio issue kubwa, kila mtu ni mwoga wa maandamano, eti tunaogopa kuuawa.
Kuna njia moja inayoweza kusaidia hapa, sie ambao tuna uwezo wa kukutana walau hapa twaweza initiate kitu na wengine wakafuata. Ingawa tuko katika sehemu tofauti za TZ, ni wazi twaweza fanya jambo. tushauriane ni kipi tufanye, twaweza andaa vipeperushi, na kila mmoja wetu mwenye uwezo wa kuptint na kupata kopi walau 50, avitumie hivyo kutoa elimu kwa jamii, iliyo nje ya mitandao hii, huo utakuwa mwanzo mzuri. Elimu kwanza mengine huja automatically
Tulikuwa na nafasi ya kuleta mabadiliko, miezi kama 15 iliyopita na tukaichezea. Sasa ngoja kwanza Somo liwaingie vizuri. Anyway dawa ni rahisi sana, kwa kuwa sisi (wananchi) ndio waajiri wa serikali, basi dawa yake ni kuiondoa madarakani. Lakini wakati tunasubiri hiyo 2015 ni lazima tuwe na mipango ya muda mfupi.
Mipango hii ipo mingi sana, but nitajikita kwenye miwili tu
Njia moja wapo ni kuwasilisha malalamiko yetu kwa wabunge wetu, ili wayasemee bungeni (sijui nao bado wanasimamia maslahi yetu) na ikiwezekana wasiunge mkono budget ya serikali mpaka kodi kwenye vitu vya msingi kama hivyo itakapoondelewa kama si kupunguzwa.
Njia ya pili na rahisi zaidi ni kuingia barabarani, mpaka kieleweke. Unakumbuka, kilichotokea Zambia, kipindi mkate ulivyopanda bei? (tatizo watanzania ni watu wa ajabu sana)