Mchaga wa ukwel
Member
- Jul 16, 2011
- 26
- 1
Watoto wa wakulima Tanzania wamekua wakighilibiwa haki zao za msingi katika chuo kikuu maarufu nchini cha SUA. Moja ya haki hizo ni AFYA.Wanafunzi hua wanalipishwa shiling laki moja kwa ajil ya afya. Haijalishi mwanafunzi huyu kaumwa au la ni lazima hela hii ilipwe kwa kila mwaka. Chakushangaza zaidi ni kwamba endapo mwanafunzi ataugua,haijalishi ana hali gani kama hajalipa hela hiyo hakuna matibabu,kwa maana hiyo SUA inafacilitate vifo vya kizembe. Mbaya zaidi,kwakua mwanafunzi husika anadaiwa,hivyo kwa kuokoa maisha yake analazimika kutibiwa nje ya chuo kwa garama zake,na bado ataendelea kudaiwa na chuo. Kama hiyo haitoshi,hata yule aliyelipa huduma anayopatiwa haimridhishi kias kwamba afya za wanafunzi ziko hatarini. Mfano mtu anaweza akafikishwa hospitali ya chuo jion lakin atahitajika asubiri hadi kesho yake kwa huduma,bila kujali ana hali gani. Hali hii inawatia watu wasiwas wakuhudumiwa na zahanati hiyo ya chuo japokuwa wamelipa laki zao. Je hii ni haki? Yako mengi yanayofanywa na taasisi hii ya afya chuoni SUA ambayo ni kinyume na haki za binadamu na watoto wa wakulima. Tusaidiane watanzania kutetea watoto wa wakulima.. NAOMBA KUWASILISHA.