Uongozi wa juu wa CHADEMA unahusika moja kwa moja na uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum walioapa tarehe 24/11/2020

kibokomchapaji

Senior Member
Aug 18, 2017
164
500
Leo tarehe 25/11/2020 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika ameongea na waandishi wa habari mambo mengi yakujibaraguza kuhusu wabunge wa viti maalum walioapishwa siku ya jana tarehe 24.11.2020 na Mhe. Spika Job Ndugai Jijini Dodoma.

Kama ulipata bahati ya kumsikiliza Mnyika vizuri basi utaelewa kuwa CHADEMA wanawachezea mchezo wa mind-game wafuasi wao kuwa hawahusiki na tukio hilo la kuteua wabunge hao wakati hali halisi ni kuwa wanahusika kwa asilimia zote.

Mambo haya ni uthibitisho kuwa CHADEMA inahusika moja kwa moja na uteuzi wa wabunge hao:-

1. Kamati kuu ya CHADEMA ingekutana kwa dharura tangu jana (hata kwa kufanya online meeting kama walivyowai kufanya kipindi kile walivyokimbia vikao vya bungeni kwa kudai kuwa wanajilinda na COVID-19) na leo wangekuja na jibu la moja kwa moja kuhusu wabunge hao kwasababu ni tukio kubwa mno ndani ya chama hicho.

2. Tutaaminije kama tukio hilo halina Baraka kutoka uongozi wa juu wa chama, makaratasi aliyoyaonesha Mnyika eti hajayajaza what if ni copy ambazo anatuonesha kabla ya kuzijaza?

3. Kauli ya kuwaomba wadau mbalimbali watoe maoni juu ya hatua za kuwachukulia walio apa pia ina ukakasi, inatoa mwanya wa kuja kuwaadaa tena wafuasi wao kuwa watu wengi wameshauri kuwa wawaache waendelee na majukumu yakibunge.

4. Kauli za walio apa jana zinadhihirisha wazi kuwa uongozi wa juu unahusika katika mchakato mzima na sasa chama kinatumia nguvu nyingi kuwaaminisha wafuasi wao kuwa hawahusiki na hii ndiyo ilikuwa game plan ya CHADEMA.

5. Press ya leo ilikuwa tayari ni sehemu ya plan kuwa waende kuapa alafu chama kitajitokeza kujisafisha kwa wafuasi wao ili kisikose uaminifu kwa wafuasi wake, ili chama kiendelee kupata ruzuku na ile michango ya kila mwezi, na mpaka mwisho wa mind-game hii ni kuwa akina Mdee hawatafukuzwa uanachama na maisha yataendelea kama kawaida.

Mwamuzi mzuri wa mambo haya ni muda tu, tutashuhudia mengi sana kabla ya mwaka huu kuisha, bado tunasubiria huko Zanzibar Maalim Seif awe Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. Tuendelee kujiandaa kisaikolojia.
 

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,364
2,000
Hiyo namba 3 wenye akili washajua kinachoendelea badala aseme watafanya maamuzi kulingana na katiba ya chama anasema eti wadau watoe maoni hatua za kuchukua.
Poleni sana wanaopeteza muda wenu kuwafuatilia nyumbu ila mjue mchezo umeshaisha
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,909
2,000
Baada ya Chama technically kukubaliana na msimamo wa Aida kuingia Bungeni, lilikuwa suala la muda tu kwa akina Bulaya kufollow suit.

Mnapaswa kumove on na maisha yenu tu sasa maana hili game limeshakwisha. Hii ni issue ya maslahi (binafsi kwa wabunge na kwa Taasisi yenyewe).

Wazungu wanasema ni ‘win-win situation’. CHADEMA wanapiga hela, CCM inajimwambafi kifua mbele kwa wafadhiili kwamba kuna bunge la vyama vingi na wananchi wanapata faraja kwamba wapinzani wapo Bungeni japo wameshakuwa compromised
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,233
2,000
Chadema lazima wachukue hatua za kueleweka katika suala hili.

Bila kuwafukuza uanachama wasaliti hawa tutajua uongozi wa Juu unahusika!

Maneno ya Mnyika si mabaya lakini hatua za kinidhamu kali za kufukuzwa chamani Wasaliti hawa ni lazima zichukuliwe ikiwemo kuripoti kosa la kufoji mihuri na nyaraka zozote za chama polisi.

Chadema isiporipoti suala hili polisi bila kujali polisi watalipokea au la tutaweka question mark kubwa kwenye utetezi wa Mnyika!
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,581
2,000
Chadema lazima wachukue hatua za kueleweka katika suala hili.

Bila kuwafukuza uanachama wasaliti hawa tutajua uongozi wa Juu unahusika!

Maneno ya Mnyika si mabaya lakini hatua za kinidhamu kali za kufukuzwa chamani Wasaliti hawa ni lazima zichukuliwe ikiwemo kuripoti kosa la kufoji mihuri na nyaraka zozote za chama polisi.

Chadema isiporipoti suala hili polisi bila kujali polisi watalipokea au la tutaweka question mark kubwa kwenye utetezi wa Mnyika!
Mkuu na wewe huna akili kama hawa kina salary slip na genge lake?

Mbona toka jana nakwambia walichofanya kina Mdee kina baraka zote za akina Mbowe?
 

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,533
2,000
Viongozi wa CDM walijuaje kama Nusrat ataachiwa tar 23 ili tar 24 akaapishwe?Kama hilo haikuambii kitu basi na wewe ni fampa!
Ndio ujiulize ilikuwaje Nusrat baada ya msukosuko wote ule akaungana na wenzake, tena bila bashasha akaenda kuapa? Walikutana wapi? Walimwambia lini? Viongozi wa CDM walifahamu, habari zilizagaa, hata humu JF zilikuwepo. Jibu la leo la Mnyika ni like lile la siku nne zilizopita, eti msimamo ni ule ule na ikibainika wapo walioenda kuapishwa uchunguzi utafanyika na kama kuna usaliti hatua zitachukuliwa.

Maana yake wapo watakaoapishwa, kuna uwezekano wakawa wamefuata utaratibu, kwa hiyo kuona kama hawajafuata utaratibu watachunguzwa! Kama wamefuata utaratibu lakini kuna usaliti hatua zitachukuliwa! Lakini pia kama wamefuata utaratibu na usaliti hakuna basi wataachiwa kulitumikia bunge japo CDM haikupeleka majina yao tume.

Ndio tunasemaga akili ndogo haiwezi kuiongoza akili kubwa!
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
12,976
2,000
Wamepewa haki ya kusikilizwa,tusubiri baada ya kikao!
Jambo lililowazi ni kuwa hao wanawake wameshirikiana na serikali ya CCM kufanya walichokifanya!Wamekihujumu chama na wamewezeshwa na Ndugai pamoja na NEC!
Sakata hili linanikumbusha lile la Lipumba!
 

King Kisali

JF-Expert Member
Nov 20, 2019
772
1,000
Acha kuchafua viongozi na hutafaulu , sisi tunajua hawahusiki kwa asilimia Mia moja , Jiwe tunajua vizuri sana , Kama aliweza kufanya vitimbi vya ajabu kwenye uchaguzi mkuu ndio atashindwa kwenye viti maalum ? Kwahiyo Chadema ndio wanahusika kumtoa Nusrat Hanje jela usiku tarehe 23 ili akaspe Jana tarehe 24 ? Tumia basi hata akili za punda kuweka mzigo mgongoni bila kuanguka .
 

Mwamba 777

Senior Member
Nov 23, 2020
155
250
Mh Magufuli apunguze posho na mishahara ya wabunge, ili kusudi pesa hizo zipelekwe kwenye mambo ya maendeleo. Pia kuhusu swala la usafiri kila mbunge apewe gari lisilokunywa mafuta sana, wote wapewe noha. Kwahayo tu watakuwa wamesaidiwa ktk swala la utiifu wa matumizi ya rasilimali za taifa na ung'ang'anizi wa viti vya ubunge.

Vilevile na wale wabunge wanaokwenda bungeni kwaajili ya lengo la kupata/kupiga pesa na kutanguliza maslahi yao binafsi kupitia yote hayo tajwa hapo juu watakuwa wamepata fundisho na somo tosha kwao.

Chamsingi Mh Magufuli awanyooshe kwelikweli.
 

mputa

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
1,153
2,000
Kwa anaefahamu, kwa idadi hiyo ya wabunge CHADEMA itakuwa na ruzuku kiasi gani
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,828
2,000
Teh teh teh
Nyie raia mambo ya siasa achaneni nayo
Ishini maisha yenu

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom