kibokomchapaji
Senior Member
- Aug 18, 2017
- 165
- 307
Leo tarehe 25/11/2020 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika ameongea na waandishi wa habari mambo mengi yakujibaraguza kuhusu wabunge wa viti maalum walioapishwa siku ya jana tarehe 24.11.2020 na Mhe. Spika Job Ndugai Jijini Dodoma.
Kama ulipata bahati ya kumsikiliza Mnyika vizuri basi utaelewa kuwa CHADEMA wanawachezea mchezo wa mind-game wafuasi wao kuwa hawahusiki na tukio hilo la kuteua wabunge hao wakati hali halisi ni kuwa wanahusika kwa asilimia zote.
Mambo haya ni uthibitisho kuwa CHADEMA inahusika moja kwa moja na uteuzi wa wabunge hao:-
1. Kamati kuu ya CHADEMA ingekutana kwa dharura tangu jana (hata kwa kufanya online meeting kama walivyowai kufanya kipindi kile walivyokimbia vikao vya bungeni kwa kudai kuwa wanajilinda na COVID-19) na leo wangekuja na jibu la moja kwa moja kuhusu wabunge hao kwasababu ni tukio kubwa mno ndani ya chama hicho.
2. Tutaaminije kama tukio hilo halina Baraka kutoka uongozi wa juu wa chama, makaratasi aliyoyaonesha Mnyika eti hajayajaza what if ni copy ambazo anatuonesha kabla ya kuzijaza?
3. Kauli ya kuwaomba wadau mbalimbali watoe maoni juu ya hatua za kuwachukulia walio apa pia ina ukakasi, inatoa mwanya wa kuja kuwaadaa tena wafuasi wao kuwa watu wengi wameshauri kuwa wawaache waendelee na majukumu yakibunge.
4. Kauli za walio apa jana zinadhihirisha wazi kuwa uongozi wa juu unahusika katika mchakato mzima na sasa chama kinatumia nguvu nyingi kuwaaminisha wafuasi wao kuwa hawahusiki na hii ndiyo ilikuwa game plan ya CHADEMA.
5. Press ya leo ilikuwa tayari ni sehemu ya plan kuwa waende kuapa alafu chama kitajitokeza kujisafisha kwa wafuasi wao ili kisikose uaminifu kwa wafuasi wake, ili chama kiendelee kupata ruzuku na ile michango ya kila mwezi, na mpaka mwisho wa mind-game hii ni kuwa akina Mdee hawatafukuzwa uanachama na maisha yataendelea kama kawaida.
Mwamuzi mzuri wa mambo haya ni muda tu, tutashuhudia mengi sana kabla ya mwaka huu kuisha, bado tunasubiria huko Zanzibar Maalim Seif awe Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. Tuendelee kujiandaa kisaikolojia.