Uongozi wa Chama Kipya Ukiingia; CCM kifutwe?

This is exactly what is wrong with Africa. Mkifute ili nini? Kinachotakiwa nikwaonyesha jinsi yakuendesha serikali ili wawe opposition wajifunze. Dejure and De facto lazima watakuwa the main opposition party in the short to medium term. How can you have an adversarial system of government bila kuwa na opposition. Itakuwa one CCM for one CDM. Wataiba tuu... Its a fact kwasababu ndio watanzania wenyewe sisi. Lazima kuwa na balance of power. Tusifanya makosa ya kufikiri kuwa kuna chama fulani ambacho kimetumwa na Mungu or something. Wote hawa wanasiasa ama angalau wengi wao ni wale wale.

wakijifunza halafu iweje??ulisikia wapi mwanafunzi anajifunza miaka 50 bila kuelewa??waingie tena madarakani wazidi kutufilisi na kile ambacho tulishakianza kukijenga...??kifutwe
 
Tunisia wamekifuta kilichokuwa chama chao tawala ili nchi nzima ianze upya; nadhani serikali ya chama kingine itakapokuja kushika madaraka itabidi suala la usajili wa CCM liangaliwe upya. Hii ikiwemo uwezekano wa kukifuta ili mashabiki wake na wanachama wake waanzishe chama kipya kabisa.

Naamini kosa kubwa alilolifanya Nyerere wakati wa kurudisha vyama vingi ni kuiacha CCM kama de fact ruling party na hivyo hawakutakiwa kuanza moja. Nadhani itapaswa waanze moja kabisa kwa chama hicho kufutwa.

Hivi kweli tuambiane ukweli kulikuwa na nia ya kweli ya kuanzisha multipartism? Vipi eti chama ambacho wanachama wake ndiyo waamuzi wakuu; viongozi wote wa vyombo vya dola walikuwa makada na resources zote za nchi zilikuwa zinamilikiwa chini ya chama hicho alafu gafla mnabadilisha sentensi mbili kwenye maandishi huku practice inaendelea kuwa vile vile na watu wote wanapiga makofi ....asante baba kutupatia multi-party! Hicho chama chenye kuweza kuishinda hicho chama kilichokuwa na hatamu zote lazima ndo kiitwe chama cha mapinduzi; ndiyo maana kila anayefanya siasa ya kweli either chama au mtu lazima aonekane mhaini maana practice yake ni tofauti na formal and informal rules zilizopo na zilizojenga atitude ya wengi.....Tuko kwenye struggle ya kuleta multiparty in practice na kuiondoa from abstract!
 
CCM ni sehemu ya dola kwani viongozi wengi wa CCM ni mawakala wa vyombo vya usalama (hasa usalama wa Taifa). Huwezi kutenganisha CCM na Dola halafu ukasema CCM ipo! Hayo ndo matatizo ya muundo wa vyama vilivyokulia kwenye mfumo wa chama kimoja au Chama dola. Kimuundo na kiutendaji chama kinabaki kuwa sehemu ya dola. Kuondoa dola mikononi mwa chama ni kuondoa chama!

Ni vigumu kurekebisha huo muundo kwani ili kufanya hivyo itakuwa ni kama kufanya mapinduzi. Hakuna anayefanyaga mapinduzi ya kujipindua mwenyewe! Hivyo CCM haiwezi kujirekebisha!!

Nilikuwa sijasoma post yako kabla ya ku post yangu-we are precisely in the same line of thinking...Huwezi kujipindua hata siku moja; lakini pia kama walivyogusia wengine ung'ang'anizi wao utasababisha watu kukosa uvumilivu na kuanza kuwatoa kwa nguvu...

Kama ningekuwa mimi CCM ingetafuta exit strategy nzuri kwa kuondoa mamluki wote wa chama then ku recruit serious people na huku wakiendelea kufanikisha smooth transition kwenye true multipartism...ninachoona CCM inazidiwa na wachache wenye maslahi ambao wanahofu kama wakikosa madaraka basi na maslahi yao yatakosa legitimacy na hivyo kuwa cost hao wachache so wengi wangependa transition but wachache hawako tayari na wana nguvu.

Cha kusikitisha hao wachache cost ya kuendelea kung'ang'ania ya weza kuwa kubwa kuliko kukubali ni bora wangeangalia jinsi ya kuleta smooth transition na huku wakiangalia kuweka maslahi yao independent na utawala....All in all hakuna kitakachorudisha nyuma changes maana wengi wamesha kuwa awere and unfortunately economy is not good enough to hold this pressure back!
 
Mkuu chama ni watu tu hakuna cha ziada. Ni kama Tanzania tunge badilisha jina bado watu wangeendelea kuwa wale wale, tamaduni zile zile na maendeleo yale yale. Sasa kama chama kikifutwa na watu hao hao wakaanzisha chama kingine bado wata kuwa na itikadi zile zile na agenda zile zile mkuu.
 
Tunisia wamekifuta kilichokuwa chama chao tawala ili nchi nzima ianze upya; nadhani serikali ya chama kingine itakapokuja kushika madaraka itabidi suala la usajili wa CCM liangaliwe upya. Hii ikiwemo uwezekano wa kukifuta ili mashabiki wake na wanachama wake waanzishe chama kipya kabisa.

Naamini kosa kubwa alilolifanya Nyerere wakati wa kurudisha vyama vingi ni kuiacha CCM kama de fact ruling party na hivyo hawakutakiwa kuanza moja. Nadhani itapaswa waanze moja kabisa kwa chama hicho kufutwa.

Nadhani kujaribu kuifuta CCM ni makosa. ni udikteta. nadhani kitakachotokea ni kwamba CCM ikishaenguliwa tu, basi wale watu maslahi ndani yake, ambao ndio wanatupa shida, watajiengua, na ccm itabaki na watanzania wenzetu waliokuwa wameporwa chama chao cha wakulima na wafanyakazi. hao watajipanga upya. of course kurejesha mali ambazo CCM imezikamata kinyume cha sheria, kama viwanja vya mpira, hiyo ni kwa mujibu wa taratibu tu. hivyo vitafutiwe miliki ya umma.

Tatizo kubwa zaidi ninaloliona ni kwamba mara tu ikishaonekana kwamba CCM inaenguliwa, yale mafisadi, ama moja kwa moja, ama kwa kutumia makuwadi, yatawekeza katika hiki chama kinachoingia madarakani. na hapo bila kuwa waangalifu, utakuta tunapigwa bao tena la kisigino. nadhani hapa umuhimu wa katiba mpya ndio unaonekana. tunahitaji kujenga misingi ambapo hakitatokea tena chama cha kujijenga namna hii na kutupoteza sisi wote
 
Hakuna haja yoyote ya kuifuta CCM.
Kwanza chama chenyewe sasa hivi kiko mahututi bin taabani. Genge linalokiongoza limekitoa mikononi mwa wanachama na kukiweka reheni mikononi mwa mafisadi na mumiani wachache wasiojali chochote zaidi ya maslahi yao. Hao walioko huko kwa sasa wako kwa ajili ya maslahi tu, wala siyo kupenda sera na mipango ya chama.
Pili, by the time chama kingine kinashika dola maana yake ni kuwa CCM kitakuwa kimeshakufa tayari. Kifo cha CCM hakiko mbali. We subiri uone.
Ila chama kingine kikiingia madarakani, lazima mali za wananchi (Viwanja vya michezo, majengo nk) zidaiwe na kurudishwa mikononi mwa wananchi.
 
Tunisia wamekifuta kilichokuwa chama chao tawala ili nchi nzima ianze upya; nadhani serikali ya chama kingine itakapokuja kushika madaraka itabidi suala la usajili wa CCM liangaliwe upya. Hii ikiwemo uwezekano wa kukifuta ili mashabiki wake na wanachama wake waanzishe chama kipya kabisa.

Naamini kosa kubwa alilolifanya Nyerere wakati wa kurudisha vyama vingi ni kuiacha CCM kama de fact ruling party na hivyo hawakutakiwa kuanza moja. Nadhani itapaswa waanze moja kabisa kwa chama hicho kufutwa.

Haina haja kuhangaika nayo.
CCM itakufa natural death, hata autopsy haina haja kufanyika. Kaburi lake litachimbwa na MABOMU.
 
Tunisia wamekifuta kilichokuwa chama chao tawala ili nchi nzima ianze upya; nadhani serikali ya chama kingine itakapokuja kushika madaraka itabidi suala la usajili wa CCM liangaliwe upya. Hii ikiwemo uwezekano wa kukifuta ili mashabiki wake na wanachama wake waanzishe chama kipya kabisa.

Naamini kosa kubwa alilolifanya Nyerere wakati wa kurudisha vyama vingi ni kuiacha CCM kama de fact ruling party na hivyo hawakutakiwa kuanza moja. Nadhani itapaswa waanze moja kabisa kwa chama hicho kufutwa.
mi sioni sababu ya ccm kufutwa kwani nina hakika kitajifia chenyewe kimya kimya
 
Mi naona kama kikishindwa na kuondoka madarakani kitakachako fuata ni kukizika maana kilishakufa siku nyingi kichobaki ni kukitoa madarakani tu!
 
Wazo zuri hilo lkn haliwezekani kwa CCM maana ni kijiwe chao cha kuchumia, mafisadi ndio wanamokimbilia maana kuna ulinzi na kipindi cha uchaguzi kikifika wanalipa fadhila kwa kulindwa.
Hakuna lisilowezekana chini ya jua. Chama kingine kikishika hatamu CCM itanyang'anywa mali zake zote maana haikuzipata kihalali. Usajili wake lazima ubatilishwe. Viongozi wake wakuu ni lazima wapewe RED CARD ili washiriki kabisa siasa kwa maisha yao yote ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali zao.
 
This is exactly what is wrong with Africa. Mkifute ili nini? Kinachotakiwa nikwaonyesha jinsi yakuendesha serikali ili wawe opposition wajifunze. Dejure and De facto lazima watakuwa the main opposition party in the short to medium term. How can you have an adversarial system of government bila kuwa na opposition. Itakuwa one CCM for one CDM. Wataiba tuu... Its a fact kwasababu ndio watanzania wenyewe sisi. Lazima kuwa na balance of power. Tusifanya makosa ya kufikiri kuwa kuna chama fulani ambacho kimetumwa na Mungu or something. Wote hawa wanasiasa ama angalau wengi wao ni wale wale.

Kuelekea kwenye Katiba Mpya ninaamini ni lazima CCM ifutwe ili ianze upya kama cha cha siasa. Vyama vingine vyyote vilianzia moja kwa kutafuta usajili wa muda na baadaye wa kudumu kwa kupita na kuomba wanachama wapya isipokuwa CCM. Aidha kianze moja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 na hivyo kwenda kwenye uchaguzi huo kama chama kipya au kisubiri kufutwa kama walivyofanyiwa Tunisia ili kukipa nafasi ya kuanza moja.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Ni chama kipi tena hicho?

Nasikia kuna watu (fulanifulani) wana mpango wa kuanzisha hicho chama na kwa kutumia mlango wa pembeni kuingia kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Sasa katika hali ya sasa ya UFISADI uliotapakaa kila mahala hicho chama si kitakuwa ni CCM B? au CCM Light?

Chama mbadala Ni CHADEMA tu na ndio chama makini cha kukichemsha CCM.

Tunisia waliamua kuanza upya mambo ya siasa kwa kuvifuta vyama vyote vya siasa na kuandikisha upya. Baada ya zoezi hilo ambalo bado linaendela mpaka sasa pamepatikana vyama vya siasa 31 na hakuna chama kikuu isipokuwa Tunisia Liberals Party ambacho ndio kinaonekana kina mvuto.

Kwahio tunaweza kuifuata Tunisia kwa mtindo wa kufuta vyama vyote na kusajili upya.
 
Sioni sababu ya kukifuta wala sidhani kama ni Democrasia maana ingekua Chama kingine kikiingia madarakani kinatakiwa kikifute kilichokuwepo awali, sijui Hali ya Marekani au England ingekuwaje saa hizi. Ninachokiona mimi wanachotakiwa kufanya Serikali mpya ni kuwafilisi woote waliohusika kuhujumu mali zetu(mafisadi) then wakaozee Jela maana hawana tofauti na wauaji. Na wasipofanya hivyo mjue lao Moja.
 
CCM KIANZA CHOKOCHOKO JUU YA CHADEMA NA VYOMBO VYA DOLA KUTEKELEZA
AZMA YENU NA BASI SISI WANANCHI TUTAMALIZIA KWA
UFASAHA ZAIDI PICHA NZIMA HIVI KARIBUNI

Mheshimiwa Kikwete kidogo kachanganya mada hapa: kati ya Chama (CCM) kilichoshiriki, kupanga na kutekeleza njama za kuwapora wananchi HAKI YA KUCHAGUA viongozi wanaowapenda , upande mmoja, na kwa upande kuna chama (CHADEMA) kinachotekeleza wajibu wake wa kikatiba kushiriki kwenye kupiga mayowe kwa njia ya maandamano ya amani kote nchini kwa kudai kwa uchungu mkali kwamba Watanzania TUMEPORWA HAKI YETU YA MSINGI kikatiba; mpaka hapo ni chama gani kinastahili kufutwa usajili na kuchukuliwa hatua zote na vyombo vya dola???

Mbele ya 'Nguvu ya Umma' hakuna cha John Tendwa na ukada wake kwa CCM, Mrema na fadhila yake kwa uenyekiti wa kamati ya bunge, wala hakuna cha Maswahiba kama Said Mwema wala nani. Tunawasubirini kwa hamu muanze mchezo mzima ili mtakapoandika moja sisi tutaandika kumi na kuendelea.

Chonde msikose kutekeleza amri na busara za Kanali Kikwete, Kapteni Chiligati na Luteni Kanali Makamba maana hiyo ni HARUSI AMBAYO tumekua tukiisubiri kwa muda mrefu sana mpaka hivi sasa sisi Vijana Nguvu kamili ya Umma.
 
wakijifunza halafu iweje??ulisikia wapi mwanafunzi anajifunza miaka 50 bila kuelewa??waingie tena madarakani wazidi kutufilisi na kile ambacho tulishakianza kukijenga...??kifutwe

wataingiaje madarakani kama cdm tunafanya vizuri?? wataingia madarakani km walioshika dola wanazembea kuleta ustawi wa jamii; na ndo maana ya ushindani wa vyama kisiasa!! kwa msingi huo, vyama vyote vitaendelea kuwepo kujiuza kwa wananchi ki sera na wananchi wataendelea kuchangua chama waonacho kinaweza waletea ustawi zaidi.
 
Back
Top Bottom